Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,900
- 19,628
Morning jamiiforum.
Dunia haina usawa,
Dunia ni katili sana.
Dunia haina huruma
Hizi ni sentensi kadhaa ambazo husikika midomoni mwa watu baada ya kukutwa na yale yanayowaelemea.
Unaweza kuchukua hatua na kukabiliana na unayoyamudu na kuyaweza ikiwa unaweza kupambana nayo mwenyewe bila kutegemea mtu yeyote lakini jambo likishakuwa kwenye watu wengi liamue Kwa busara mno.
Hebu tushuke na hizi.....................
1.Usitumie Sheria panapotakiwa Busara
Naam,watu wengi huingia mtego mbaya ni sawa huenda Sheria iko upande wako,na Una haki lakini mazingira bado yanakuona mwenye hatia.fikiri mara mbili.
2.Sikiliza kwanza kabla ya kuongea.
Inawezekana unajua vingi,unafahamu mambo mengi,lakini ni vizuri kuwapa nafasi wengine,ili uishi Kwa Amani
3.Kubali kushindwa.
Kushindwa ni aibu,fedheha na udhaifu,haswa kama unataka kuwaaminisha watu kwamba Jambo fulani unaliweza, lakini ukweli ni kwamba kuna vitu kadri unapoving'ang'ania na kutafuta ushindi ndipo unapozidisha maumivu,aibu na majuto.
4.Usishindane na mamlaka.
Iwe mtu binafsi,iwe taasisi,ni kweli mamlaka nyingi hutumia nafasi zao,kisa tu zina nguvu ,kukandamiza,kuonea na kutoa upendeleo wa wazi.huku wanaostahili wakiachwa aidha Kwa husuda au wivu au Kwa hujuma na roho mbaya .
5.Toka sehemu usiyoheshimiwa.
Yote haya ni kulinda Uhuru wa nafsi na Amani ya moyo,
Iwe kazi,kikao, shughuli au tukio lolote lenye kukutanisha watu wengi,usikubali kudharauliwa,usitumie nguvu kubwa watu ama umma ujue unaweza au kujua kitu fulani,hapana step back kwasababu, mtu asipokubali matendo yako ni ngumu kukubali maneno yako.
6.Kubali huwezi kukubalika na kila mtu
Inawezekana,watu wengi na makundi tofauti yanakukubali,na watu wengi wanakuelewa lakini anaweza kutokea mtu mmoja au kikundi fulani kikawa tofauti na wewe,usione ni Jambo la kushangaza, usilazimishe watu wote wakuelewe.
6.Ridhika na maisha.
Pesa,utafutaji hauna mwisho hakuna namba ya mwisho ya utafutaji,kila siku watu wanazindua project na biashara mpya,kila siku watu wanaishi vizuri tofauti na jana lakini ni vema kuelewa kuwa ipo setup watu wamefanya kiasi kwamba pesa inaingia tu,so usikurupuke kutaka kufanana unaweza kupoteza hata kidogo ulichonacho.
7.Saidia wasiojiweza ikiwa unaweza.
Usitoe ili watu wakuone,usitoe ili uonekane mwema na mwenye roho nzuri.toa kwasababu kuna mtu umeona ana uhitaji na wewe unaweza kumsaidia.usizidishe kama huna uwezo mkubwa
8.Jipende,jikubali
Hakuna yeyote na hatokaa atokee,anayefanana na wewe.hata mapacha wanafanana cover tu siyo siha na haiba,hivyo wewe ni wa pekee, Mungu alikuumba kiupekee ndiyo maana hufanani Mawazo na mtu mwingine,vaa vizuri,Kula vizuri ishi maisha mazuri.
9.Weka mipaka na kiasi.
Iwe mazoea,ukaribu ,urafiki na Vitu vingi kuwa na kiasi ,siyo mtu akikwama tu laki moja ,hapigi hata simu anakimbilia kwako kama vile aliiweka kisa tu anajua huwa huna mipaka,hujui kusema hapana.
10.Usikubali Unyonge.
(Kwa wanaume)Kila mwanaume ni mpambanaji,kila mwanaume ni kama yupo jeshini,kila mwanaume ni mfungwa mtarajiwa.kila mwanaume ni muwajibikaji,mlinzi,mtoa matumaini,ni anategemewa,usikubali kila kitu Kwa kigezo cha kutaka Uhuru Na amani, ndiyo maana zipo mamlaka na vyombo vya kisheria,mengine tutakutana mahakamani.
Bonus
USITEMBEE NA MKE,MUME AU MPENZI WA MTU NI HATARI KULIKO TINDIKALI.
Uwe na asubuhi njema.