Kumnyima mume unyumba ni kumuua?

Mtu B

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
919
51
Ni mjadala niliousikia leo kwenye daladala nilipokuwa nakuja kazini. Wanawake wawili walikuwa wameketi viti vya mbele yangu na walikuwa wanamjadili mwenzao ambaye walikuwa wanamtaja jina mara kwa mara kuwa ndiye aliyesababisha kifo cha mumewe kutokana na kumnyima unyumba.

Ati wakuu mwanaume anaweza kufa ati kisa tu kunyimwa unyumba na mkewe?
 
Hiyo inawezekana, lakini indirectly..
Siyo kwamba mwanaume asipofanya basi anakufa, nooop!
Ila kwamba huenda baada ya kunyimwa alienda kutangatanga huko mabarabarani, na aidha akakanyaga waya wa shoti, au alifumaniwa mahala, akapigwa na kupelekea mauti!

Yawezekana kabisa!

Mwenzio alikuwa anakupa ile kitu katika namna ambayo huwezi kuielezea halafu ghafla tu anakatisha huduma; hamna maelezo wala shutuma; kila ukiuliza anakwambia hakuna tatizo; lakini ndoa unaendelea kunyimwa; lazima ushikwe na kihoro na ukikosa ushauri mwafaka presha inakupanda na hapo kama hakuna huduma lazima uzimike!
 
mmmh!!! si ungewauliza. labda walimaanisha jamaa alikuwa napiga nje akapata ngwengwe ikamchukua...
 
weeeee! hafi mtu hapa! walahi bilai ndugu yake balali!!
 
labda akakanyaga miyawa jee! mke kamuua mumewe hapo na familia ya mume walitakiwa wam sue mwanamke :D
 
Inawezekana kafa kwamawazo ya kunyimwa ndoa. Labda aliwaza sana kwa nini siku hizi sipewi! Labda kuna mtu mwingine anapewa instead. Hayo mawazo ndo mpaka kifo.
 
Siyo kummua.lakini usimnyime kwa kumkomoa au kwa vile kidumu chako kimekuchosha
 
mmmh!!! si ungewauliza. labda walimaanisha jamaa alikuwa napiga nje akapata ngwengwe ikamchukua...

Kuwauliza isingewezekana ndugu yangu, kinamama wa mjini wana mambo, wangeweza kuanza kunisuta kwa kuwaingilia kwenye umbea wao. Mie nilikaa kimya tu kama nasikiliza redio vile.
 
Ni mjadala niliousikia leo kwenye daladala nilipokuwa nakuja kazini. Wanawake wawili walikuwa wameketi viti vya mbele yangu na walikuwa wanamjadili mwenzao ambaye walikuwa wanamtaja jina mara kwa mara kuwa ndiye aliyesababisha kifo cha mumewe kutokana na kumnyima unyumba.

Ati wakuu mwanaume anaweza kufa ati kisa tu kunyimwa unyumba na mkewe?

sijui kama lina ukweli hili kwamba kunyimwa unyumba Mume anaweza kufa, lakini kwa maoni yangu kunyimwa unyumba ni sababu tosha kabisa ya kuvunja ndoa especially hata kama ulimkosea mwenzako ukamuomba samahani naye akatamka amekusamehe lakini wakati huo huo akiendelea kukuadhibu kwa namna yake.
 
Yawezekana kabisa!

Mwenzio alikuwa anakupa ile kitu katika namna ambayo huwezi kuielezea halafu ghafla tu anakatisha huduma; hamna maelezo wala shutuma; kila ukiuliza anakwambia hakuna tatizo; lakini ndoa unaendelea kunyimwa; lazima ushikwe na kihoro na ukikosa ushauri mwafaka presha inakupanda na hapo kama hakuna huduma lazima uzimike!

Mie presha ya hivyo sipati ng'o. Tena nasema hapa wazi hata siku nikipata mchumba nitamwonesha hii post. Mke akininyima bila sababu ya maana na mie namyima, tit for tat. Na sitamuomba tena. Na tena hali ikiendea hivyo bila reconciliation, nadhani hizo ndio zile irreconcilable differences ambazo kwazo ndoa inavunjwa rasmi, kila mtu ajue hamsini zake, hakuna haja ya kutesana.
 
Ni mjadala niliousikia leo kwenye daladala nilipokuwa nakuja kazini. Wanawake wawili walikuwa wameketi viti vya mbele yangu na walikuwa wanamjadili mwenzao ambaye walikuwa wanamtaja jina mara kwa mara kuwa ndiye aliyesababisha kifo cha mumewe kutokana na kumnyima unyumba.

Ati wakuu mwanaume anaweza kufa ati kisa tu kunyimwa unyumba na mkewe?

Hata mimi ningekufa, tena after three days.
 
Back
Top Bottom