Email. nipenguvu@gmail.com
Instagram. nipenguvu
“Ee bwana wangu! Nisahidie mimi mja wako”. Ilisikika sauti ya hofu kutoka kwa mama mmoja akiwa kanisani huku akiwa anatetemeka.Siku hiyo ilikuwa siku ya jumapili katika kanisa moja lililopo kijijini, pembezoni kabisa mwa mji uliozungukwa na ziwa. Siku hiyo mvua ilionekana ikiwa inanyesha sana na kuongezeka kadri mda unavyozidi kwenda. Ndani ya kanisa walipata kuonekana baba na mama wakiwa wameshikana mkono huku wakipata kuombewa na mchungaji mbele ya mathabau, na mama alikionekana ni mjamzito aliyekaribia kujifungua. Basi mvua ikiwa inaendelea uko nje, upepo na mingurumo ya radi nayo ilionekana kurindima na kusikika kila pembe ya kanisa hilo.
Huku wahumini nao wakionekana wenye wasiwasi na hofu kubwa, wakati mchungaji akiwa anaendelea kuwaombea akiwa ameshika biblia, ghafla radi ilipiga na kupasua upande wa kushoto mwa kanisa hilo na kusababisha mlipuko na moto mkali kufatia, kasheshe ilianza pale ambapo radi hiyo ilifanya hivyo mfululizo na kuzua taaruki kwa watu waliopo ndani ya kanisa na kuanza kukimbiakimbia pasipo muendekeo, mama na baba yule waliopo kwenye yale mathabau walivyoona hivyo walimuomba sana mchungaji apate kumalizia sala yake ya kumbariki mtoto aliyopo tumboni kwa mama,walionekana kama wanajua kinachoendelea.
Basi radi ilizidi kupiga kwa nguvu mpaka kufikia pembezoni mwa madhabau yale, na kabla mchungaji hajamalizia maombi yake alipatwa kupigwa na radi ile na kumfanya kuanguka chini kifudifudi. akiwa pale chini ameshika biblia yake kwa nguvu, Mchungaji huyo alionekana bado kutaka kumalizia sala yake, lakini alishidwa kwasababu hali yake ilizidi kuwa mbaya sana, lakini kabla ajaaga maisha alisema maneno machache kuwa “ Mtoto huyu ni chagua lake, Mungu awe pamoja nanyi” na palepale kupoteza maisha.Mama na baba walihuzunika sana wasijue cha kufanya, lakini mama akiwa pale naye alizidiwa na uchungu na kumuomba mumewe msahada kwamba hasingeweza kunyanyuka mahali hapo.
Baba harakaharaka alifanya kila namna kumsahidia mke wake na kuomba msahada kwa watu waliopo sehemu hiyo bila mafanikio yeyote. Watu walikataa kwa kuwa waliofia maisha yao zaidi kwa kujificha, radi na mvua zilizokuwa zikiendelea ziliwafanya kushidwa kutoa msahada, mahali hapo palikuwa na radi isiyo ya kawaida. Ndipo baba akaamua kupambana mwenyewe kumsahidia mkewe ili apate kujifungua, baada ya muda kwa bahati nzuri mama yule aliweza kujifungua palepale mathabauni mtoto wa kiume.
Siku hiyo ingeweza kuwa ya furaha lakini badala yake ilikuwa ya kushangaza zaidi pale walipoona na kustaajabu kuwa mtoto huyo mchanga aliyekuja hapa duniani siyo wa kawaida, kwani alikuwa ni mwenye nywele nyeupe, macho ya bluu huku akiwa na uzito usiokuwa wa kawaida, pembeni ya mgongo wake kukiwa na mbavu mbili mbili kila upande wa ubavu. Wakiwa wanaendelea kushangaa na kustaajabu mara kwa mbele kilitokea kitu chenye mwanga mkali na mlio wa ajabu kisha kuzima na hapohapo mvua pamoja na radi zilikata ghafla. Ilo lilikuwa jambo la kushitua na kushangaza sana kwao, na kwa wale waliojibanza kwenye ubao wa bati kujizuia na radi na mvua nao walishuudia tukio lile. Baba na mama kuona hivyo walikimbilia nyumbani kwa ajili ya kujisitiri na mtoto wao.
Lakini kwakuwa majirani walishuudia tukio hilo ndipo taratibu taarifa zilianza kusambaa kijijini hapo na siku baada ya siku taarifa zile zilimfikia chifu katili wa kijijini hapo na kumpelekea kutoa amri kuwa mtoto huyo akamatwe na kuuwawa popote pale alipo. Huku mama na baba wakiwa nyumbani walipopata hizo habari waliamua kukimbia na mtoto wao kuepukana na mikono ya chifu huyo aliyekuwa katili sana kijijini hapo, walikimbia kuelekea upande wa kaskazini mwa ziwa, kule ambapo upepo ungevuma kuelekea kusini mwa kisiwa.
Walipofika bila ya kupoteza muda walitengeneza kisanduku kidogo na kuchora halama ya msalaba kisha kumuweka mtoto wao na kukifunga kabisa, walipo maliza kufanya hivyo walifanya maombi machache kuhofia kukutwa na kisha kukisukumiza kisanduku kile kuelekea kusini mwa ziwa. Kutokana na upepo uliotoka kaskazini kuelekea kusini boti lile dogo lilionekana kusukumwa taratibu na upepo huo na kwa mbali kupotelea ziwani huku mama na baba wakiliangalia wakiwa wanatokwa na machozi, walitoa Baraka za mwisho wakisema “Mungu kama kweli upo! Basi tunaomba umlinde mtoto wetu kwenye ziwa hili na umuweke katika falme za juu za hii dunia ili uzibitike kuwa wewe upo”.
Inaendelea.....