Kumekuwa na hadithi na simulizi nyingi nzuri. Lakini hii inaweza ikawa nzuri zaidi. Inaitwa ULIMWENGU WA MATAJIRI

Nipenguvu

New Member
Sep 18, 2019
4
6
ulimwengu wa matajiriiii.png

Email. nipenguvu@gmail.com

Instagram. nipenguvu

“Ee bwana wangu! Nisahidie mimi mja wako”. Ilisikika sauti ya hofu kutoka kwa mama mmoja akiwa kanisani huku akiwa anatetemeka.Siku hiyo ilikuwa siku ya jumapili katika kanisa moja lililopo kijijini, pembezoni kabisa mwa mji uliozungukwa na ziwa. Siku hiyo mvua ilionekana ikiwa inanyesha sana na kuongezeka kadri mda unavyozidi kwenda. Ndani ya kanisa walipata kuonekana baba na mama wakiwa wameshikana mkono huku wakipata kuombewa na mchungaji mbele ya mathabau, na mama alikionekana ni mjamzito aliyekaribia kujifungua. Basi mvua ikiwa inaendelea uko nje, upepo na mingurumo ya radi nayo ilionekana kurindima na kusikika kila pembe ya kanisa hilo.

Huku wahumini nao wakionekana wenye wasiwasi na hofu kubwa, wakati mchungaji akiwa anaendelea kuwaombea akiwa ameshika biblia, ghafla radi ilipiga na kupasua upande wa kushoto mwa kanisa hilo na kusababisha mlipuko na moto mkali kufatia, kasheshe ilianza pale ambapo radi hiyo ilifanya hivyo mfululizo na kuzua taaruki kwa watu waliopo ndani ya kanisa na kuanza kukimbiakimbia pasipo muendekeo, mama na baba yule waliopo kwenye yale mathabau walivyoona hivyo walimuomba sana mchungaji apate kumalizia sala yake ya kumbariki mtoto aliyopo tumboni kwa mama,walionekana kama wanajua kinachoendelea.

Basi radi ilizidi kupiga kwa nguvu mpaka kufikia pembezoni mwa madhabau yale, na kabla mchungaji hajamalizia maombi yake alipatwa kupigwa na radi ile na kumfanya kuanguka chini kifudifudi. akiwa pale chini ameshika biblia yake kwa nguvu, Mchungaji huyo alionekana bado kutaka kumalizia sala yake, lakini alishidwa kwasababu hali yake ilizidi kuwa mbaya sana, lakini kabla ajaaga maisha alisema maneno machache kuwa “ Mtoto huyu ni chagua lake, Mungu awe pamoja nanyi” na palepale kupoteza maisha.Mama na baba walihuzunika sana wasijue cha kufanya, lakini mama akiwa pale naye alizidiwa na uchungu na kumuomba mumewe msahada kwamba hasingeweza kunyanyuka mahali hapo.

Baba harakaharaka alifanya kila namna kumsahidia mke wake na kuomba msahada kwa watu waliopo sehemu hiyo bila mafanikio yeyote. Watu walikataa kwa kuwa waliofia maisha yao zaidi kwa kujificha, radi na mvua zilizokuwa zikiendelea ziliwafanya kushidwa kutoa msahada, mahali hapo palikuwa na radi isiyo ya kawaida. Ndipo baba akaamua kupambana mwenyewe kumsahidia mkewe ili apate kujifungua, baada ya muda kwa bahati nzuri mama yule aliweza kujifungua palepale mathabauni mtoto wa kiume.

Siku hiyo ingeweza kuwa ya furaha lakini badala yake ilikuwa ya kushangaza zaidi pale walipoona na kustaajabu kuwa mtoto huyo mchanga aliyekuja hapa duniani siyo wa kawaida, kwani alikuwa ni mwenye nywele nyeupe, macho ya bluu huku akiwa na uzito usiokuwa wa kawaida, pembeni ya mgongo wake kukiwa na mbavu mbili mbili kila upande wa ubavu. Wakiwa wanaendelea kushangaa na kustaajabu mara kwa mbele kilitokea kitu chenye mwanga mkali na mlio wa ajabu kisha kuzima na hapohapo mvua pamoja na radi zilikata ghafla. Ilo lilikuwa jambo la kushitua na kushangaza sana kwao, na kwa wale waliojibanza kwenye ubao wa bati kujizuia na radi na mvua nao walishuudia tukio lile. Baba na mama kuona hivyo walikimbilia nyumbani kwa ajili ya kujisitiri na mtoto wao.

Lakini kwakuwa majirani walishuudia tukio hilo ndipo taratibu taarifa zilianza kusambaa kijijini hapo na siku baada ya siku taarifa zile zilimfikia chifu katili wa kijijini hapo na kumpelekea kutoa amri kuwa mtoto huyo akamatwe na kuuwawa popote pale alipo. Huku mama na baba wakiwa nyumbani walipopata hizo habari waliamua kukimbia na mtoto wao kuepukana na mikono ya chifu huyo aliyekuwa katili sana kijijini hapo, walikimbia kuelekea upande wa kaskazini mwa ziwa, kule ambapo upepo ungevuma kuelekea kusini mwa kisiwa.

Walipofika bila ya kupoteza muda walitengeneza kisanduku kidogo na kuchora halama ya msalaba kisha kumuweka mtoto wao na kukifunga kabisa, walipo maliza kufanya hivyo walifanya maombi machache kuhofia kukutwa na kisha kukisukumiza kisanduku kile kuelekea kusini mwa ziwa. Kutokana na upepo uliotoka kaskazini kuelekea kusini boti lile dogo lilionekana kusukumwa taratibu na upepo huo na kwa mbali kupotelea ziwani huku mama na baba wakiliangalia wakiwa wanatokwa na machozi, walitoa Baraka za mwisho wakisema “Mungu kama kweli upo! Basi tunaomba umlinde mtoto wetu kwenye ziwa hili na umuweke katika falme za juu za hii dunia ili uzibitike kuwa wewe upo”.

Inaendelea.....
 
Nipe nguvu hii hadithi itaendelea mpaka mwisho au unauz kitabuu tujue maana arosto sio nzuri kabsaa🤔
 
Ile hadithi yetu inaendelea.....

Walifanya hivyo huku wakiwa wamekumbatiana na baada muda kidogo wanakijiji nao walifika mahali hapo na kukuta kila kitu kimeshamalizika, walichoamua kukifanya waliwachukua mama na baba yule na kisha kuwapeleka mpaka kwa chifu ili kupata hukumu yao.
Walipofikishwa kwa chifu, naye bila huruma alitoa hukumu ya kwamba baada ya kuuwawa alisema wawili hao hawatakiwi tena kuonekana kijijini hapo ifikapo kesho na mali zao zote kutaifisha. (Tukirudi nyuma. wawili hao walionekana ni watu waliobarikiwa sana na Mungu kutokana na kujituma kwao na kumjua Mungu, walipata kujikusanyia mali nyingi sana kijijini hapo na kuwa watu maarufu, lakini katika umaarufu huo pia walijitengenezea maadui wengi akiwemo chifu huyo aliyetamani sana mali zao,chifu huyo katili aliwatafutia visa vingi pasipo mafanikio mpaka lilipofika tukio hilo).
Baada ya hukumu kupitishwa usiku ulipoingia mama na baba wale walikushanya virago vyao na kuondoka kuhofia kuuwawa na wanakijiji waliokuwa na hasira kali. Waliondoka nyuma wakaacha shamba lao kubwa pamoja na mali zao zote kama alivyoagiza chifu huyo katili, na kuelekea upande wa mashariki ya mbali hili kuanziasha maisha yao mapya huko.
Wakiwa huko maisha yalisonga na ikawa katika mwaka wa tano walibahatika kumpata mtoto wao mwingine na kumpatia jina la John. Mtoto huyo alionekana mwenye busara na akili kadri muda ulivyozidi kusonga. Pia alionekana mwenye uwezo mkubwa darasani. Japo wao walikuwa maskini wakupindukia lakini waliona umuhimu wa elimu, waliamua kujibana na kujichangachanga hilihali mwanao aendelee na shule. Basi miaka ilizidi kusonga, siku nazo zilikata naye John alikuwa na atimaye kujiunga na chuo “chuo cha veta”. Akiwa chuo alichukua kozi ya mambo ya ujenzi na kuitilia mkazo, baada ya miaka mitatu alimaliza na kuingia mtaani kujishugulisha na mambo hayo ya ujenzi.
Siku moja kwenye njia nyembamba alionekana akipita msichana mmoja aliyejitwisha (kubeba) ndoo ya maji kichwani kutokea mtoni chemchem. Na maji hayo yalikuwa ya matumizi ya nyumbani (huyu ni Janeth). Katika njia hiyo iliyokuwa nyembamba yenye mlima kiasi na matope ya utelezi, kutokana na mvua iliyonyesha mda mfupi uliopita Janeth hakuweza kuupanda mlima ule akihofia kuteleza, kwakuwa alikuwa mwenyewe basi ilimlazimu kuiweka ndoo chini na kusubiri msahada. Basi mpita njia mmoja alietokea ng’ambo ya mto kuelekea kijiji jirani kutafuta kibarua cha ujenzi (huyu ni John).

Njiani alikutana na Janeth, na Janeth alivyomuona hakusita kumuita na kumuomba msahada wa kumpandishia ndoo ya maji, John alichukuwa jukumu hilo la kumsaidia mwanadada huyo mrembo kwa sababu naye alikuwa anaenda njia hiyohiyo, wakiwa njiani walipata kupiga stori mbilitatu na kutambulishana majina huku kila mmoja akionekana kumfurahia mwenzake tena kwa tabasamu zito kwenye nyuso zao, alivyomfikisha Janeth kwao yeye alikunja kona na kisha kuelekea kibaruani. Jioni ya siku moja Janeth kama kawaida yake akiwazake chemchem anachota maji, ghafla walijitokeza vijana wawili nyuma yake, vijana hao walionekana wakimfatilia Janeth toka mapema ya siku hiyo. Basi wakiwa nyuma yake walimwita na Janeth alipowaona alisita kwenda maana walionekana kama vibaka. Vijana wale ndipo walipoanza kwenda zaidi kuelekea upande wa Janeth, Janeth kuona hivyo kwa kuwa alikuwa mwenyewe alijikuta akiangusha ndoo ya maji chini na kuanza kukimbia. Vijana wale kuona vile walihamua nao kuanza kumkimbiza kwa nyuma. Janeth kufika mahali alijikuta amechoka na vijana wale kumkamata. Ndipo Janeth akaanza kupiga makelele “wananibaka, wananibaka, msahada, msahada !!!!!!”.
Bahati nzuri upande wa pili kwa kuwa John naye alikuwa anaelekea hukohuko kama njia yake ya kila siku, basi akiwa njiami alisikia sauti ile, basi akaona akimbilie eneo la sauti inapotokea na kwa kuwa hakuwa mbali basi aliwakuta vijana wawili wakiwa wamemshika Janeth kwa nguvu. John kuona hivyo hakutaka kupoteza muda aliamka na jiwe lililokuwa mbele ya macho yake fasta kama kipanga na kumshindilia mmoja ya aliyemshikilia Janeth na jiwe kichwani mpaka akatoa mlio “kwaaaaaa!!!” hapohapo akaanguka chini na kuanza kugaragara na kulia kama mtoto, basi yule mwingine kuona hivyo akasema “wewe boya umempiga mshikaji na jiwe kichwani, nakuchoma na bisibisi kichwani!” John akamwambia “ni ngumi hiyo, sio jiwe” duh! Yule jamaa alivyosikia hivyo hakutaka kupoteza muda akatimua mbio sana. Basi John akamchukua Janeth na kumsindikiza hadi nyumbani kwao.

Basi huo ndo ukawa mwanzo zaidi wa urafiki wao. Siku kadhaa ikawa kila jioni John akitoka shuguli zake anakutana na Janeth chemchem anapokuja kuchota maji wanapiga stori mbilitatu na kusindikizana mapaka makwao. Janeth alivutiwa sana na ukarimu, ucheshi na ujasiri wa John, ikawa kila siku na kila muda Janeth anatamani kuwa karibu naye huku John naye hivyohivyo alivutiwa sana ya urembo wa Janeth. Urafiki huo ulionekana kuzidi na kuzidi na kujikuta wakipendana na kuwekeana haadi nyingi za kuja kuwa pamoja na kuoana siku moja. Basi Janeth ikawa kila anapomaliza kupika chakula cha mchana anatenga chakula kidogo na kumpelekea John, alifanya hivyo mara kadhaa na kujikuta kuwa anachelewa kurudi nyumbani.
Tabia yake ndo ikawa hiyohiyo kila siku ya kuchelewa kurudi nyumbani. Mama Janeth siku moja alijua tabia ya mwanae baada ya kuambiwa na majirani. Mama Janeth baada ya kufatilia kwa kina aligundua mwenyewe kuwa mwanae Janeth siyo tabia hiyo tu ya kuchelewa kurudi nyumbani pia anamahusiano ya kimapenzi na kijana huyo aitwae John. Kiukweli mama na baba Janeth walitamani sana siku moja mwanao aolewe na mtu mwenye uwezo ili awatoe kwenye dhiki ya umasikini. Mama Janeth aliamua kufatilia historia ya John na kwenda mpaka kijijini kwao na kukutana na jirani wa John anayeitwa Mwamtumu, mama Janeth aliomba kuelekezwa anapokaa John au amueleze japo kidogo maisha yake anayajuaje. Mwamtumu hakusita kumueleza na hivi ndivyo alivyomwambia mama Janeth.
John ni kijana maskini na ametokea kwenye familia fukara sana ambayo wanashindia mlo mmoja kwa siku, katika kijiji hichi wametengwa kutokana na umasikini walionao pia wakiusishwa na ushirikina. Familia hii ni wakuja na huko walipotoka walifukuzwa kwa kudaiwa kuwa ni wachawi.
Mama Janeth alivyosikia hivyo alistaajabu alichoambiawa. kwa jazba na hasira harakaharaka aligeuza na kuelekea nyumbani.

Itaendelea....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom