Kumekucha!

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
Kumekucha sasa kumekucha,
Majogoo vijijini yanawika,
Hata na jua mbinguni limetoka,
Wazalendo amkeni, tufanye kazi sasa!

Ooh, ooh, mamaa
tusonge mbele

Ooh, ooh, mamaa
tusonge mbele sasa tusonge mbele,

Na majembe mabegani, tusonge mbele
Na mapanga mikononi, tusonge mbele
Sote tutoke vijijini, tukalime sasaa!



Ahh! Enzi hizo tulikuwa na moyo na nchi hii! Lakini kwa sasa? Natafuta "reverse song"!
 
Hahahahahaha nilikuwa nauchukia sana huu wimbo maana mara nyingi kila nikiamka around 6.00am ukiweka RTD basi ni lazima utausikia tu. Ilifikia mahali kila ukianza tu basi nilikuwa nabadilisha station LOL!
 
Bubuu! Utauchukiaje wimbo unaohimiza watu kuamka. Yaani baada ya hapo lazima uanze safari ya mzigoni, kabla majira haijaanza!
 
Yaani huu wimbo nauchukia kama nini. ulipokuwa unapigwa tu RTD ile saa 6.00 am kama bado hatujaamka basi baba alikuwa anakuja na stiki kutoa dozi tuamke tujiandae kwenda shule!
 
Mrijani rajab, supa

The reverse tafuta mwimbo wa msondo kuna verse mzee masharubu anaimba

jama ee ooo jama ehhh
hali hii mpaka lini jamani eeehhh
ukiamka na shida ya jana eeeh
na ya leo inaongezekaaa x2
 
Kumewiya sasa kumewiya
Majogoo vijiji yamenyamaza,
Hata jua mbinguni limezima,
Wakolini amkeni, tunyonye sasa watz!

Ooh, ooh, mamaa
turudi nyuma

Ooh, ooh, mamaa
turudi nyuma sasa turudi nyuma,

Na majembe tuweke chini, turudi nyuma,
Na mapanga tuwapokonye watz mashamba, turudi nyuma
Sote tuingie vijijini, tukalale!


Ahh! Enzi hizo tulikuwa na moyo na nchi hii! Lakini kwa sasa? Natafuta "reverse song"![/QUOTE]
 
nlikuwa nasoma shule moja ya sekondari basi asubuhi lazima tukapailie japo hatua nne kwa 120 kabla ya kuingia darasani asubuhi dar nimesisimka
 
nikiusikia wimbo huu najua tayari kwenda shuleni (primary), na kama weekend au tupo likizo basi najua muda si mrefu mama anakuja kutuamsha chumbani kwetu - sikuupenda kabisa.

Tatizo ki band Mbili National Matshusta cha Mshua alikuwa anakifungulia makusudi - hulali ukiusikia wimbo huu.
 
Kumekucha sasa kumekucha,
Majogoo vijijini yanawika,
Hata na jua mbinguni limetoka,
Wazalendo amkeni, tufanye kazi sasa!

Ooh, ooh, mamaa
tusonge mbele

Ooh, ooh, mamaa
tusonge mbele sasa tusonge mbele,

Na majembe mabegani, tusonge mbele
Na mapanga mikononi, tusonge mbele
Sote tutoke vijijini, tukalime sasaa!



Ahh! Enzi hizo tulikuwa na moyo na nchi hii! Lakini kwa sasa? Natafuta "reverse song"!

nyie mnaleta mizaha ya kukariri verse, wenzenu huku nyuma wamewasha mitambo ya Dowans.
 
Bubuu! Utauchukiaje wimbo unaohimiza watu kuamka. Yaani baada ya hapo lazima uanze safari ya mzigoni, kabla majira haijaanza!

Hahahahahahah ulikuwa unapigwa kila leo hasa asubuhi (Monday to Friday) kiasi ambacho nikajenga chuki kubwa dhidi ya huu wimbo. Nilikuwa sina tatizo la kuamka mapema hata kidogo lakini huu wimbo mhhhhh! we acha tu LOL!
 
BAK na Elnino,

Mmenikumbusha mbali sana sana. Huwa sipendi kuamka mapema hadi leo na siwezi kulala mapema.

Sasa nilikuwa nikisikia huo wimbo, hasira zinanipanda. Ni kama siku ya pili kulala JKT, niliona kama nimelala kutoka saa nne hadi saa sita usiku. Nilikuwa siupendi na nafikiri hadi leo sidhani ntaupenda.

Siku hizi kuna wimbo siupendi. Ni Alarm ya simu yangu ya mkononi. Wenye SAMSUNG watakuwa wanaifahamu. Imekaa kizembezembe na huwa nikiisikia, inanikumbusha kipindi nilikuwa nalala saa moja na nusu na inabidi kuamka.......na ninakuwa busy siku nzima na tena usiku mzima. Ninakuja kulala kwa masa 3 na kuamka tena na hapo nikija kulala, nalala masaa 24. Hii Sauti ya simu, ahh, naona kizunguzungu. Itabidi niibadili hata simu yenyewe ili milele nisisikie tena hiyo sauti.

Nikiwa Primary School, kuna siku tulikuwa tunakwenda na baba Sikonge madukani kuuza bidhaa kama nyanya, vitunguu, kabeji nk. Sasa kulikuwa na jamaa tunashindana naye kufika hapo madukani kwa Waarabu. Mzee atakuamsha saa 11 alfajiri na kuniambia kwa Kinyamwezi "......wewe Kiyungi, amka bwana, Samora (kwa ajili ya Madevu) kashafika Ikulu........" Ikulu ni sehemu anapoishi Mtemi wa Sikonge.

Mkaa Mweupe kweli umenirudisha mbaali sana.

Kipindi nilichokuwa nakipenda ni "JAMBO....." maana hapo ni miziki poapoa. Hata kama umechoka, ukimsikia Bichuka au Maneti anatesa redion basi unaamka na kuanza kucheza au kuimba. Huu wimbo kama upo, basi Marehemu Mzee ujuwe hata kufoka ataacha. Atausikiliza hadi uishe na ukiisha, basi uwe umejiandaa tayari kwenda shamba au kwenye majukumu mengine siku za weekend/likizo.

 
Last edited by a moderator:
leteni mipango ya kukusanya watu tuifanye jangwani au mnazi mmoja tahrir square sio mambo ya shambani, utalima mvua zenyewe ziko wapi? kilimo kwanza hela zote washagawiana hawa hamna mkulima hata mmoja aliyeambulia
 
nyie mnaleta mizaha ya kukariri verse, wenzenu huku nyuma wamewasha mitambo ya Dowans.

Utamzuia mtu kufanya service gari yake?
Nasikia vijiweni kwamba mwenyewe kaja na ndege kuichukua ila wanamvunjia magoti ili ibaki kuna dilg pia la vibaka kuiba stata ila soko hakuna.
 
Enzi hizo nilikuwa najivunia kuitwa mtanzania nakumbuka 80-83 niko primary kamanda wa Chipukizi wa wilaya siku hizi hata nikiziona picha zake naona kichefuchefu.
 
Njema sana hii mkuu, ikipigwa asubuhi lazima kiranja mkuu niwahi shule-primary school kuhimiza namba na mchakamchaka. Wimbo wa mchakamchaka. "chama cha mapinduzi x2, chama cha mapinduziiiiii dumisha ujamaa. Mwenyekiti nyerere x2, mwenyekiti nyerereeeee, dumisha ujamaa. Makamu ndugu jumbe...
 
Hahahahahahah ulikuwa unapigwa kila leo hasa asubuhi (Monday to Friday) kiasi ambacho nikajenga chuki kubwa dhidi ya huu wimbo. Nilikuwa sina tatizo la kuamka mapema hata kidogo lakini huu wimbo mhhhhh! we acha tu LOL!

Redio ilikuwa RTD ulikua unaweka idhaa ya kingereza au ulikuwa unaweka SW kwa ajili ya redio za nje? wewe ulikuwa kiboko maana zaidi ya RTD kiswahili na External Service au Sauti ya redio unguja lazima uvuke mipaka kwa SW.Maisha yanabadilika siku hizi chaguo lako RTD haipo na nivigumu kuisikiliza TBC,For emergency case only.
 
Asante sana Mkaa Mweupe, umenikumbusha kuamka asubuhi, kutafuta ufagio, na kuelekea skuli primary, siku hizo hazitakuja tena.
 
hilo nalo ni wazo,
leteni mipango ya kukusanya watu tuifanye jangwani au mnazi mmoja tahrir square sio mambo ya shambani, utalima mvua zenyewe ziko wapi? kilimo kwanza hela zote washagawiana hawa hamna mkulima hata mmoja aliyeambulia
 
Back
Top Bottom