Kumekucha: Wanakijiji wachoma matrekta 20 ya wawekezaji Babati

Je wakuwachomea ni hao wahindi tu ? Tulichukua mashamba ya mkonge leo hii kwa mtu yeyote yule mwenye kuyakumbuka mashamba ya mkonge anaweza kutokwa na machozi ,tulitaifisha mabasi mengi tu kwa wanaomkumbuka Hashu Suleiman leo ni sifuri,tulikuwa na KAMATA leo patupu,tulikuwa na uda leo ni dau ,sasa kwa watu hawa kuchoma matrekta na kuharibu mashamba ya miwa ,sidhani kama muhindi atakosa la kufanya ,ila nionavyo wazalendo ambao walikuwa wameajiriwa watakuwa wamepoteza kazi na kipato.

Isiwe tunafurahia tu ni lazima tujiulize je hawa ndio waliotufikisha hapa ? Tunawaona wahindi wanauza ubuyu na jice hadi wanafikia walipofikia ,mwenzangu ukiajiriwa unakaa miezi miwili unamuibia tajiri wako,siku ya tatu unarudia ombaomba si ajabu ukarudi kwa uliemuibia.

Je tatizo ni hawa wahindi ?
 
Kazi ya ukombozi imeanza kwa kasi kabisa ni muda mwafaka kwa ukombozi wa bara la Africa. Babati na Mwanza ni mifano kwa pande zote za tz zinazonyanyasika kuweza kuamka na kuchukua hatua madhubuti.
 
Naunga mkono wananchi kujieleza kwa namna yoyote ile isipokuwa kuharibu mali na maisha. Haki ni kwa kila mtu, walichofanya ni ukatili kwa binadamu wenzao. Tutaishia kwenye maafa na ulipizaji kisasi badala ya ukombozi. Ndicho kinachoitafuna Somalia.

Nalaani na kupinga kabisa kitendo hicho!
wanainchi walishalalamikia muda mrefu wawekezaji hawa ila maofisa wa serikali wakawapuuza.TATIZO NI KWAMBA WENYE FEDHA HAWATAKI KUFWATA SHERIA WANAPORA HAKI ZA WANAINCHI THRU CORRUPT OFFICIALS. KUNDUCHI KUNA MHINDI KAPEWA MAEKARI 2003, wanainchi walishajenga na hati wanazo ila wamewekewa uzio wameambiwa waondoke.
 
Hata vita vya Maji Maji vilianza kwa kuchoma mashamba ya Pamba ya Wakoloni. Na sasa kitakachofuata tutachoma mashine na mitambo yote ya Rostam Azizi, kwa siku moja tu kama Septemba eleven, halafu baadaye mali zote za Fungamtama. Du!!! Naipenda sana Movie ya SARAFINA.
 
halafu eti mnasema hakuna haja ya katiba mpy!!!!???? Huo ndo mwendo wenyewe bado kidogo tuu tutafika walikofkia misri na hapo tutajiita nchi ya amani kiukweli
 
Je unaunga mkono wananchi kupigwa risasi na askari wa mwekezaji?mi nawaunga mkono wanakijiji hao,people's power
 
Kuna mawili hapa:
kuwa kama Somalia au kuwa kama Kenya/Egypt
Tunataka kutawalika? au Tunatafuta vurugu kwa ujumla?
 
Kwa SISI tuliobahatika kujua Kikongo Tunasema

TULE MONDE JIPOZISHOOOOOOOO...........................................Yaani Excellent Gooood Job
 
Hizo shamba zina zalisha sukari guru,hiyo sukari inatumika ku tengaleza pombe haramu ya gongo.wanainche wenge wana poteza maisha,kutumia pombe haramu.wafanyakazi wana teswa na kukosa haki zao.kilimo cha miva inahitaji maji mengi,hizo shamba zina geuzamaji kwa kiwango kubwa sanaa.wanainchi wana kosa maji kwaku tumia katika masamba yaoa.pamaoja na hayo wana kwepa kodi ya mapato. Hayo ni kwa kifupi tu.
 
hivi kwani huko hakuna kiwanda cha sukari? Kama kipo kinaitwaje? mimi sijawahi kufika huko. kama kweli kuna kiwanda cha sukari basi serikali ihakikishe inatafuta chanzo cha gomvi hilo na si kupokea rushwa toka kwa wazalishaji na kuwahukumu wananchi. Kama kweli hakuna kiwanda basi si lazima tufuate kuwa eti mashamba yalikuwepo toka enzi za mkoloni. Thamini chako.
 
Back
Top Bottom