Kumekucha TRA

Jambo lipo mana huyu Assad jana baada ya kuapishwa ametamka eti kufanya tathmini tena kama pesa ni za umma ama la., kuna kamchezo flani ccm wanajaribu cijuwi itaishia vipi hii movie. let c..

Kweli mkuu halafu sasa hawa ccm wanataka kutumia njia ya kipumbavu sana kwa kumtumia huyu Assad, nimeskia anajichanganya anaoneka katumwa kabisa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
hivi kwanini aliekua anakaimu nafasi ya cag hakuteuliwa cag badala yake akateuliwa mtu ambaye alikua nje ya taasisi?

Hata Utouh alitolewa nje (NBAA) wakati kulikuwa na mtu ndani anakaimu. Hiyo kazi siyo mchezo kwamba umpe mtu yeyote ati kwa sababu tu ni wa ndani au alikuwa anakaimu.

Lakini pia kama unataka kuhusisha na ripoti ya CAG ya Escrow ni vyema ukajua kwamba Utouh alishamaliza hiyo kazi kwa asilimia 95 kabla ya kustaafu
 
Wakuu naomba kuweka wazi kinachoendelea.

Gazeti la Mwananchi limechapisha habari jana kuwa Bodi ya TRA (TRAB) imemsimamisha Kamishan wa TRA kutofuta hati za mauziano ya hisa kati Mechmar na Piperlink na Piperlink kwenda PAP.

Hii imetokana na ripoti ya TRA kuonyesha kuwa uuzaji wa hisa hizo ilikuwa ni uongo. Sasa Kamishna jana ameamua kufuta hizo hati na kilichonishangaza zaidi ni baada ya Zitto kutweet kuwa bodi ya TRA (TRBA) haikukaa na kutoa hili zuio kwa Kamishna. Kwa maana nyingine habari zilizochapishwa na Mwananchi jana hazikuwa za kweli.

Sasa kinachoendelea PAP na IPTL ndio wamemfungulia mashtaka Kamishner kwa kufuta hati hizo kwani alikiuka agizo la bodi ya TRA yaani TRAB)
Aksante mkuu.
Hii Nchi sarakasi haziishi, ila fedha zetu lazima warudishe.
 
Hata Utouh alitolewa nje (NBAA) wakati kulikuwa na mtu ndani anakaimu. Hiyo kazi siyo mchezo kwamba umpe mtu yeyote ati kwa sababu tu ni wa ndani au alikuwa anakaimu.

Lakini pia kama unataka kuhusisha na ripoti ya CAG ya Escrow ni vyema ukajua kwamba Utouh alishamaliza hiyo kazi kwa asilimia 95 kabla ya kustaafu
Utouh alishamaliza kila kitu , CCM tu wamechakachua tukaletewa ripoti baridi.
 
Jambo lipo mana huyu Assad jana baada ya kuapishwa ametamka eti kufanya tathmini tena kama pesa ni za umma ama la., kuna kamchezo flani ccm wanajaribu cijuwi itaishia vipi hii movie. let c..
.
Ikulu ya kikwete imethihirika kwa wizi.
Wizi ulikuwepo kwa viwango tofauti na kwa usiri tangia awamu ya kwanza hadi ya nne. Hii awamu ya nne ya kikwete ndio wizi mkubwa zaidi umetokea halafu kibaya zaidi ikulu inahusika moja kwa moja.
Mgombea urais atakae jinadi kwa kuifanyia uchunguzi familia ya Kikwete hasa Riz1 Nitampa kura yangu bila kujali anatoka chama gani
 
Naona kizunguzungu, naomba wafadhili wasitoe hela zao mpaka kieleweke
 
Wabia wa maendeleo walishaweka msimamo. Hawatoi fedha hadi wahusika wawajibishwe. Kwa jinsi serikali ilivyo na uhaba wa fedha za bajeti lazima watake wasitake wahusika wawajibishwe.
 
Kama tanesco wamekiri kwamba invoices walizokuwa wanapelekewa zilikuwa zina VAT basi hakuna shaka ye yote kuwa FEDHA ZA VAT ni fedha za umma.
Kihasibu kama IPTL alifanya manunuzi makubwa yeye VAT kuliko MAUZO yenye vat,IPTL wanawajibika kisheria kuiomba tra iwalipe IPTL tofauti ya vatput na vatinput.Kinyume pia ni kweli kwamba kama IPTL walikuwa na makusanyo MAKUBWA KWA MAUZO YENYE VAT kuliko MANUNUZI yenye VAT waliwajika kuilipa TRA tofauti ya vatoutput na vatinput.
 
Invoices ziko overcharged, automatically na VAT nayo Itakua overcharged pia maana yenyewe ni 18% ya exclusive amount.

Overcharged amount ni Mali ya TANESCO,Vat component ni ya TRA na mwisho exclusive amount ni Mali ya wamiliki halali wa IPTL.

Court iliagiza kufanyike ukokotozi sahihi (recalculation) ili kujua hapo exclusive sahihi ambayo itapelekea kupata VAT sahihi na kisha Total sahihi. Baada ya hili zoezi ndio wafananishe kiwango kitakachopatikana against kilichokwishalipwa ili wajue nani anamdai mwenzie na Tshs ngapi??

Matokeo yake, no recalculation, Hela zishakombwa zote, Singh bado anadai alipwe, Hakuna kodi iliyolipwa TRA, e.t.c
 
Jambo lipo mana huyu Assad jana baada ya kuapishwa ametamka eti kufanya tathmini tena kama pesa ni za umma ama la., kuna kamchezo flani ccm wanajaribu cijuwi itaishia vipi hii movie. let c..
Prof. Mussa Assad ni mtu mweledi na msomi mwenye msimamo thabiti, hawezi kufanya ujinga wa aina yoyote. Yeye ni professional aliyebobea. CAG alituachia swali gumu ambalo linatakiwa kupatiwa majawabu: kwamba kwenye pesa za escrow huenda kuna pesa za serikali, je ni kaisi gani ama angetupatia scenerio analysis ya kuonyesha hizo pesa za serikali na ambazo si za serikali ni zipi.
 
Back
Top Bottom