Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

Mangungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
2,404
Reaction score
3,061
MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.
 
Ukitaka kuua ccm wafanyehuo ungese s wenu
 
Nape anaweza kwa akili zake fupi ila ccm hawaweI kufanya hivi
 
Ukitaka kuua ccm wafanyehuo ungese s wenu

Mkuu unajua chaguo la JK kua ni Pombe Magufuli??
Je unaikumbuka kauli ya Riz 1?? Rais wa tano wa tanzania hatoki kasikazini
 
Nape anaweza kwa akili zake fupi ila ccm hawaweI kufanya hivi

Wazo sio la Nnape ni la sisiemu wote,unazani Laigwanan akitimba magogoni,atalipiza kisasi balaa,unazani hawajui hicho kitu??
 
Lowasa ni mdau wa ufisadi kama alivyo kikwete na wanajuana na ndiyo maana hana anayeweza kumkataza jambo akatii.

Mangula alipomwambiaga kikwete kwamba yeye chama hakikumwandaa kuwa mgombea wa uraisi, nani asiyefahamu yaliyomkuta? Jamaa alikuwa na fedha za kununua ikulu na mtu wa kwanza kumshughulikia baada ya uchaguzi alikuwa ni Mangula.

Lowasa akiwa mpambe wake wa karibu na wakishirikiana almost kila kitu, anafahamu ni namna gani anaweza kupitishwa hata kama kuna watu wanaleta unoko na ndiyo maana jamaa na madhambi yake halina hata aibu.

BTW,kwa nini mnaongelea makosa madogo madogo ya kupiga kampeni kabla ya muda yale mengine mnayaficha?

Nilitegemea mtaongelea swala lake la kukumbatia nguvu ya rushwa anavyopitapita kununua watu hasa wal influential.

Nilitegemea mtaongelea swala la maswali ya utajiri wake ambalo hajawahi kuliongelea na pamoja na kwamba hakuna chombo cha kimaadili cha ccm ama serikali kimewahi kutaka maelezo yake rasmi, hata yeye hatakagi kuliongelea.

Nilidhani mtakuwa mnaongelea msimamo wake ambao umekuwa ukikubaliana na ufisadi,rushwa, ukosefu wa democrasia, hujuma kwa jamii, ukiukwaji wa katiba na haki za binadamu ambayo ni matatizo makubwa kwa sana kwa sasa katika nchi yetu. Ni dhahiri kwamba hata alipokuwa seriklilni hadi leo hakuna siku moja lowasa ameonyesha kukerwa na mambo haya ambayo yamekuwa yakifanyika mchana kweupe. Yeye amekaa kinafiki kama mbweha muwinda mbuzi.

Nilidhani mtakuwa mnahoji uzalendo wake ambao haupo kutokana na ushiriki wake katika wizi wa richmond na hadi leo amegoma kuwataja wamiliki wa kampuni hiyo fisadi.

Nilitegemea kwa sasa ndio muda wa kila mtu kumwambia jamaa lowasa kwamba yuko uchi na hafai kuwa kiongozi wa mtu kwa taarifa ya Mwakyembe iliyofupishwa na kuyaficha ficha maovu mengine ya lowasa na kikwete kwa kisingizio cha usalama wa nchi.

LAKINI, LOWASA NA KIKWETE HAWANA TOFAUTI NA HUU MPANGO WALIPANGA PAMOJA BAADA YA KUFARIKI MWALIMU. KIKWEETE ALIVYOTUFANYA WATANZANIA, NI BINADAMU GANI ANAYETAKA TENA KUWA NA RAISI WA DIZAINI ILE?

TUMIENI VIUNGO VYENU VIZURI KATIKA MAAMUZI KABLA HAJAANZA KUWAITA WAZAZI WENU AMBAO NI MAREHEMU!.
 
Nasema; Nape si saizi ya Lowasa, hakuna wa kumvua uanachama wake. Mtaanzia wapi?? CCM hakuna mwenye uwezo wa kumfungia paka kengele. Woote walionyamazishwa labda January tu ndo sijamsikia wazi wazi, lakini wametoke na wengine wapya ka Mtoto wa mkulima (bwana nyuki) pia Wapo kina Wasira na wengine kina Chemba sijui wengine unao wajua weye. Mbona kimyaa wala hakuna anayepiga chafya?
Lowasa hasemi sana, anawazawadia takrima watu tu. Kwa kuwa hajafika kwenyu ndo maana mnatuzibia pumzi si tuliokuwa tunangojea kukumbukwa naye?
Kwetu tunasema ni "wivu wa kike" huo. CCM hakuna aliye salama. Hakuna atakaye chaguliwa aache kumwaga mihela. Acheni tule, mla mla leo si mla jana wala kesho.
 
Ukitaka kuua ccm wafanyehuo ungese s wenu
We mpuuzi ccm siyo Lowasa kama anamakosa hata akitimuliwa sawa ila ccm haiwezi kufa unajidanganya tumia hoja zingine ila siyo eti lowasa akifukuzwa chama kife siyo kweli umepotoka.
 
Tarifa hii inakosa uhalali kwa kuwa mwandihi ni kibaraka wa lowasa hapo wanatengeneza mazingira ili asifukuzwe kwa akili yake anawahadaa watanzania na wenye chama ili wasifanye maamuzi kubenea zuzu kweli.
 
MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.

Ccm awana ubavu wa kumfukuza lowass,mbona wasimfukuze pinda wakati ameiba pesa nyingi kuliko lowasa
 
....."Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu....

I hope hii ni tetesi isiyo na chembe ya ukweli. Otherwise, huu utakuwa uzuzu na ujuha wa kiwango cha ajabu sana. Badala ya kuwashughulikia wanachama waliokwapua pesa ya ESCROW na kukisababishia chama kichapo kwenye uchaguzi wa S/M, wao wanataka kuhangaika na Lowassa. Chama hakina vision.
 
CC waanze na wale waliochota Stanbic bank

Nasikia Pinda amewagomea wazee wa CCM kwa maana kuwa kama wanamnyooshea kidole waanze na mkuu wa nyumba na familia yake inayomwandaa Membe awe rais wa Vijana mafisadi wa CCM.

Lowasa ajipime hawa jamaa anaoshindana nao wameshika makali kwani ndio walioko kwenye madaraka ya chama na serikali. Kama Vipi ajitoe CCM na kugawa mali zake zote kwa UKAWA ili ziwarudie watanzania.
 
CC chini ya uenyekiti wa Kikwete haina ubavu kumvua uanachama EL.

Kama JK anaburuza miguu kumfukuza kazi Prof. Muhongo, anaweza vipi kuongoza kikao cha kumvua uanachama EL.

Kama CCM wanashindwa kumfukuza uanachama Mtemi Chenge ambaye kwenye kashfa zote yumo, wanawezaje kumvua uanachama EL ambaye tuhuma zake zoote hazijawahi kuthibitishwa na chombo chochote cha ndani au nje?

Vv
 
nawe nae mawazo ujenzi kumbe ni mawazo ubomozi...unamsikiliza na kumuamini kubenea? mtu huyu muongo na ni stadi wa kutunga uzushi na kuukuza kupitia gazeti lake na mtandao wake..miaka mingi kubenea alijigeuza mnajimu na kuandika kwa kujiamini kabisa kuhusu viongozi ambao mtu wake anayemtumia anawaona ni tishio kwa mustakabali wa biashara zake. lakini yote aliyokuwa akiandika yamebainika kuwa ni uongo na uzushi mkubwa halafu bila haya hata haombi radhi. Sas nikwambie tu kuwa kubenea ametumwa awapandishe joto wana ccm na ajenge chuki kusudi wana ccm waichukie serikali yao na chama chao. lakini hiyo ni janja ya nyani tu sisi kwisha gundua.. Hakuna kikao cha kumjadili na kumfukuza Lowassa, hakuna madai yoyote dhidi ya Lowassa tangu alipoonywa na ametulia, sasa kubenea na wenzake ukiwemo mawazo ujenzi mjiandae kisaikolojia kwani mtapata mshangao wa mwaka na hamtaweza kuamini.....ccm tumejipanga na tuna hakika tutaweka chaguo la wananchi...
MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

"Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki," ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, "Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu."

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, "Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu."

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa "onyo" kwa kile kilichoitwa, "kuanza kampeni kabla ya muda kufika."

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, "mkakati wa Lowassa wa kusaka urais."

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.
 
Ahaaaaaa ahhhhhhha ahaaaaaaa source. Kubenea. Hizo zitakuwa habari za uvumi tu ccm hawawezi kufanya hivyo kwani hawajipendi wajalibu waone
 
Back
Top Bottom