Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.


ngoja tuone, lakini mie niko amani zanzibar hapa kwenye sherehe za mapinduzi naona kapokelewa vizuri tu na prado kali sana za magamba na ni mgeni mualikwa, sasa tuone manake kubenea ana sources sana huyu mtu,
 
Kwa upande mwingine usikute huu ni mpango tu wa CCM kumpa umaarufu lowassa ili mwisho wa siku ashinde hizi wanazoita upinzani dhidi yake na watz tumwone shujaa,mwisho wa siku aingie magogoni.
 
We mpuuzi ccm siyo Lowasa kama anamakosa hata akitimuliwa sawa ila ccm haiwezi kufa unajidanganya tumia hoja zingine ila siyo eti lowasa akifukuzwa chama kife siyo kweli umepotoka.

inawezekana wewe hujui kuwa mavi yakikubana unatakiwa ukanye
 
Siamini taarifa hii Nawafahamu ccm hawawezi kumuengua kwa approach hiyo, nachojua tu ni kwamba ccm watatuteulia candidate anayekubalika na watanzania wengi kama ilivyokuwa kwa Mh Kikwete.
 
Sio kuvuliwa Uanachama labda kama wanataka kumpa Baraka zote za kuwa mgombea pekee anaye UZIKA ndani ya CCM ni LOWASA na wagombea wengine wamuunge mkono EL.
 
Back
Top Bottom