Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

Kumekucha CCM ajenda za kumfukuza chama Lowassa karibuni kutimia

MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.

Hakuna Wa Kumvua Uanachama Rais Mtarajiwa Lowassa Ndani Ya CC Ila Wanachama Wanaweza Kumkataa Na Kumwondoa Madarakani Rais Kikwete Kwani Matendo Yake Ndiyo Sasa Yanakigharimu Chama. Ukitaka CCM Kife Kibudu Ngoja Sasa Hiyo Jumanne Huko Visiwani Zanzibar Watamke Kumng'oa Rais Mtarajiwa Wa Watanzania Mheshimiwa Ndugu Edward Ngoyai Lowassa Kisha Uone Mziki Wake Na Patachimbika Kuanzia Humo Ukumbini Hadi ktk Ofisi Zote Za CCM. Thubutuni Muone!
 
Ukitaka kuua ccm wafanyehuo ungese s wenu

Amekufa Nyerere,mwanzilishi wa CCM ,na haijakufa ,sembuse huyo baba yako,angekuwa anajiamini angekuwa anahangaika kutoa rushwa kila sehemu utadhani Ruge.Mtu anayejiamini hatoi rushwa,mumeufanya uraisi kama bidhaa ya kununua sokoni.
 
kumbuka kauli ya jk jua yeye na bwana EL hawajakutana barabarani sasa sijui ichokikao kifanyike kichocholoni cha kutaka EL afukuzwe huo uanachama
 
Lowasa ni mdau wa ufisadi kama alivyo kikwete na wanajuana na ndiyo maana hana anayeweza kumkataza jambo akatii.

Mangula alipomwambiaga kikwete kwamba yeye chama hakikumwandaa kuwa mgombea wa uraisi, nani asiyefahamu yaliyomkuta? Jamaa alikuwa na fedha za kununua ikulu na mtu wa kwanza kumshughulikia baada ya uchaguzi alikuwa ni Mangula.

Lowasa akiwa mpambe wake wa karibu na wakishirikiana almost kila kitu, anafahamu ni namna gani anaweza kupitishwa hata kama kuna watu wanaleta unoko na ndiyo maana jamaa na madhambi yake halina hata aibu.

BTW,kwa nini mnaongelea makosa madogo madogo ya kupiga kampeni kabla ya muda yale mengine mnayaficha?

Nilitegemea mtaongelea swala lake la kukumbatia nguvu ya rushwa anavyopitapita kununua watu hasa wal influential.

Nilitegemea mtaongelea swala la maswali ya utajiri wake ambalo hajawahi kuliongelea na pamoja na kwamba hakuna chombo cha kimaadili cha ccm ama serikali kimewahi kutaka maelezo yake rasmi, hata yeye hatakagi kuliongelea.

Nilidhani mtakuwa mnaongelea msimamo wake ambao umekuwa ukikubaliana na ufisadi,rushwa, ukosefu wa democrasia, hujuma kwa jamii, ukiukwaji wa katiba na haki za binadamu ambayo ni matatizo makubwa kwa sana kwa sasa katika nchi yetu. Ni dhahiri kwamba hata alipokuwa seriklilni hadi leo hakuna siku moja lowasa ameonyesha kukerwa na mambo haya ambayo yamekuwa yakifanyika mchana kweupe. Yeye amekaa kinafiki kama mbweha muwinda mbuzi.

Nilidhani mtakuwa mnahoji uzalendo wake ambao haupo kutokana na ushiriki wake katika wizi wa richmond na hadi leo amegoma kuwataja wamiliki wa kampuni hiyo fisadi.

Nilitegemea kwa sasa ndio muda wa kila mtu kumwambia jamaa lowasa kwamba yuko uchi na hafai kuwa kiongozi wa mtu kwa taarifa ya Mwakyembe iliyofupishwa na kuyaficha ficha maovu mengine ya lowasa na kikwete kwa kisingizio cha usalama wa nchi.

LAKINI, LOWASA NA KIKWETE HAWANA TOFAUTI NA HUU MPANGO WALIPANGA PAMOJA BAADA YA KUFARIKI MWALIMU. KIKWEETE ALIVYOTUFANYA WATANZANIA, NI BINADAMU GANI ANAYETAKA TENA KUWA NA RAISI WA DIZAINI ILE?

TUMIENI VIUNGO VYENU VIZURI KATIKA MAAMUZI KABLA HAJAANZA KUWAITA WAZAZI WENU AMBAO NI MAREHEMU!.

Lowasa Rais ajaye nani wa kumzuia c upinzani hadi magamba yenyewe kwasababu jadi yako kubisha nategemea uzi mrefu wa ubish
 
Mtanyooshea vidole sana Lowassa lakini mjuwe ndiyo anayeweza kuikoa Tanzania hapa ilipo lazwa icu
 
CCM hawezi kufanya bahati nasibu ya namna hiyo.
 
kumbuka kauli ya jk jua yeye na bwana EL hawajakutana barabarani sasa sijui ichokikao kifanyike kichocholoni cha kutaka EL afukuzwe huo uanachama

Huyo mkwere ndo wa kumwamini? naona mkuu hujachanganya za kwako hapo
 
We mpuuzi ccm siyo Lowasa kama anamakosa hata akitimuliwa sawa ila ccm haiwezi kufa unajidanganya tumia hoja zingine ila siyo eti lowasa akifukuzwa chama kife siyo kweli umepotoka.

Mimi si mwanachama wa ccm, lkn naamini hawawezi kumfukuza huyu jamaa, wote wachafu ndani ya chama, we wakati ule wa kuondoa magamba nini kiliwafanya wanywee? Kama si nguvu ya huyu jamaa, we subiri tuone kama wataweza kumwondoa.
 
PUPA! PUPA! PUPA! NA UNWISE ZA CCM NI LAZIMA ZITAWATOKEA PUANI /waache ujinga huu na kufuata mambo ya mitandao vikao vyake na marafiki zake vina ihusu nini ccm/NJAMA ZA WAGOMBEA WA KITI HICHO ZISIIUMIZE KICHWA ccm "ccm imara"/LOWASSA ETI LEO HII ANYIMWE HAKI HATA YA KUJUMUIKA NA NDUGU NA MARAFIKI KISA ETI KILA ANAPOKAA AJENDA NI URAIS ALLS IS AGAINST HUMAN RIGHT
 
Nachojua EL ni mtu wa mipango..mpaka sasa ameweza kuji brand..sas akishapita kama mgombea wa ccmm basi hamna jinsi wote waliompinga chaman itawalazimu wamuunge mkono kuokoa chama.
 
Ahaaaaaa ahhhhhhha ahaaaaaaa source. Kubenea. Hizo zitakuwa habari za uvumi tu ccm hawawezi kufanya hivyo kwani hawajipendi wajalibu waone

Amekufa Nyerere,mwanzilishi wa CCM ,na haijakufa ,sembuse huyo baba yako,angekuwa anajiamini angekuwa anahangaika kutoa rushwa kila sehemu utadhani Ruge.Mtu anayejiamini hatoi rushwa,mumeufanya uraisi kama bidhaa ya kununua sokoni.

Nina kati ya watangazania ndani ccm asiyetoa rushwa? Iwe m/kiti S/mtaa ,diwani,ubunge na uraisi wote kitu kimoja hamna haja ya kumsakama EL hakuna msafi hata mmoja
 
Mzunguko wa pesa utaongezeka zenjibar mpaka hao vimwaga waondoke loooh
Full urojo
 
Wajing'oe wao, watuachie LOWASSA wetu, p*twbv hao.
 
Back
Top Bottom