Kumbukumbu za ulimwengu (World Archives)

Kumbukumbu za ulimwengu (World Archives)

Maisha Halisi kijana Mowgli Mvulana Aliyelelewa na Mbwa Mwitu Mnamo 1867 ndani kabisa ya misitu ya India, wawindaji walifanya ugunduzi ambao umetengeneza historia kubwa kabla ya kutengeneza filamu ya jungle book.

Mvulana mdogo, mwenye umri wa miaka sita, akitembea kwa miguu minne, akiunguruma kama mbwa mwitu, na kuishi ndani ya mapango - akizungukwa na kundi la mbwa mwitu. Jina lake alikuwa anaitwa Dina Sanichar.

Alikuwa amelelewa na wanyama pori hadithi hi ni ya kweli
kuhusu mtoto wa msituni. Waokoaji walipomleta kwenye kituo cha watoto yatima huko Agra, walijaribu kumfundisha kuzungumza kama binadamu wa kawaida, kutembea wima na kula chakula kilichopikwa.

Lakini maisha ya polini yalikuwa tayari yamemuathiri.
Alijifunza kusimama na kuvaa nguo, lakini bado alinoa meno yake kwa kutumia mifupa na alipendelea nyama mbichi kuliko kitu kingine chochote.

Dina hakuwahi kuzungumza neno la lugha yoyote.
Alikufa akiwa bado tu kijana anayekaribia umri wa miaka 30 kutokana na ugonjwa wa kukosa kupumua vizuri, baada ya kuanza kutumia sigara kwa kuokota vipisi vya sigara kwa kutokana na kuiga maisha ya wenyeji wake.

Hadithi yake ya kutisha na kusikitisha ilihimiza umakini na ubinadamu mwaka 1942 zoltan kodra alipoamua kutengeneza filamu ya maisha ya huyu jamaa The Jungle Book.
FB_IMG_1761638874247.jpg
 
Back
Top Bottom