Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Haya tupe ya Kariakoo...usidandie ya wahamiaji wa Gerezani (Wazulu na Wamanyema) tupe ya Kariakoo ya Watanganyika.
Mag3,
Hawa Wamanyema ni kizazi cha kwanza na cha pili kuzaliwa Tanganyika
ni Watanganyika.

Mbona unataka kuleta ubaguzi?

Nakuwekea hapo chini majina ya Watanganyika ambao walihudhuria
mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo:

''The TANU inaugural meeting was attended by a small crowd of about twenty people, among them Julius Nyerere, Abdulwahid and Ally Sykes (Wazulu), Dossa Aziz, Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan (Mzulu), Marsha Bilali (Mhabeshi), Rashidi Ally Meli (Mngazija), Frederick Njiliwa, Idd Faiz Mafongo (Mmanyema), Idd Tulio, Denis Phombeah (Mnyasa) and others.''

Hapo chini nakuwekea orodha ya waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam:

upload_2017-8-18_21-48-36.png
 
Ungekiri hivyo kutoka mwanzo wala hatungekuwa na ugomvi wowote...ni historia ya wazee wako, period. Ugomvi unakuja pale unapoanza kudai ni historia ya Tanganyika!
Miaka nenda miaka rudi majibu ni hayo hayo, ndiyo leo yamekuingia?

Bravo Alama Mohamed Said, leo yamemuingia huyu anaejiita Mag 3 kuwa ni historia ya wazee wetu. Ma shaa Allah.

AlhamduliLlah.
 
Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.

Si tupe basi ya kwenu? Vipi, kama hakuna, sema tu hakuna.

Wewe ulisikia wapi Nyerere akifanya harakati za kudai uhuru butiama au na wazee wa butiama?

Hao wazee wanaotajwa kwenye harakati za uhuru karibia wote ni wa Dar, 90% wazee wetu wa Kariakoo. Nyerere mwenyewe alipokelewa na kuwekwa Kariakoo kwa kina Abdul Wahid Sykes.

Leta raha za kudai Uhuru kutokea kwenu.

Salamu FaizaFoxy!
Uhuru wa Tanganyika kiini chake kikubwa ni Tanga,Dar es Salaam pamoja na Tabora!( Huko ndiko cheche za mapambano ziliruka sana) lakini huwezi puuza mchango wa watanganyika wote bila kujali Imani zao,kabila zao na unasibu mwingine.
Swali la kujiuliza kwa nini Harakati za Uhuru wa Tanganyika Ziliungwa mkono kwa nguvu kuu sana na Hasa Pale Mwalimu Nyerere alipoongoza TANU?
Unwritten History from Lake zone! UNCLE PASCAL MAYALLA atakuwa alishawahi kusikia au anaijua hii.
Alitokea Mtabiri (Mganga wa Jadi) Kutoka Sukuma Land kwa jina la Chalya( If not mistaken) Aliamka asubuhi moja kabla ya mwaka 1950,akawaaambia jamaa zake! Nalotaga elelo Nabhonaga Nzagamba ya pii elifumela Shashi,ele na Ng'wenda gupozu Eyeneyu Igwenha Butemi bhu Si Eyi Tafsiri( Leo nimeota nimeona Ng'ombe dume mweusi akitokea upande wa Ushashi ( eneo hilo leo ni toka Bunda mpaka Butiama) akiwa na Nguo ya kijani huyo Dume ndiyo atakayeleta utawala huru wa Nchi hii.
Hiyo ndiyo Hsitoria ambayo na sie tulisimuliwa na wazee wetu!( Oral History)
Naomba kuwasilisha.
 
Ungekiri hivyo kutoka mwanzo wala hatungekuwa na ugomvi wowote...ni historia ya wazee wako, period. Ugomvi unakuja pale unapoanza kudai ni historia ya Tanganyika!
Mag3,
Mimi hulka yangu toka udogoni sikuwa mtu wa shari na ugomvi.

Nilikuwa nikiona shari haraka naikwepa.

Sasa mimi sina sababu ya kugombana na wewe kwa ajili ya ''wazee
wangu,'' au ''Tanganyika.''

Hiyo ndiyo historia kama nilivyoiandika wewe una haki ya kuchagua ni
jina gani unaona linakufurahisha na itapunguza joto katika kifua chako.

Hiki kitabu wakati mwingine kinanisikitisha jinsi kilivyochoma nyoyo za
watu wengi.

Kuna kitu kama hiki kilitokea mwaka wa 1988 wakati wa kuadhimisha
miaka 20 ya kifo cha Abdul Sykes.

Ally Sykes alinunua nafasi katika Daily News na akaniomba niandike
kumbukumbu ya kaka yake.

Mhariri wa Daily News alisema hatoweza kuchapa kumbukumbu ile hadi
amepewa ruhusa na serikali kwa sababu kumbukumbu ile ya maisha ya
Abdul Sykes yamegusa historia ya Tanzania kwa ujumla wake.

image+%252811%2529.jpg
 
Ntamaholo,
Ikiwa unayo historia ya AICT katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa
Tanganyika iweke hapa Majlis tuisome.

Hapo chini nakuwekea namna wazee wangu walivyoliendea jambo hili la
kupigania uhuru.

Kila palipokuwa na ugumu walikaa kitako na kuomba dua:
''Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.''

Katika majiia hayo hapo juu nilifanya mahojiano na Sheikh Rashid Sembe na Mmaka Omari na hayo ndiyo waliyonieleza walipopanga mkakati wa Kura Tatu.

Ikiwa wewe una historia nyingine ya TANU na uhuru usisite kutuletea hapa ili sote tunufaike.
Soma historia ya Sheikh Rashid Sembe hapo chini:
Mohamed Said: SHEIKH ABDALLAH RASHID SEMBE: SHUJAA WA KURA TATU NA UAMUZI WA BUSARA WA TABORA
Kwahiyo mkuu DUA za wazee wako ndo zilisababisha tupate Uhuru sio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu FaizaFoxy!
Uhuru wa Tanganyika kiini chake kikubwa ni Tanga,Dar es Salaam pamoja na Tabora!( Huko ndiko cheche za mapambano ziliruka sana) lakini huwezi puuza mchango wa watanganyika wote bila kujali Imani zao,kabila zao na unasibu mwingine.
Swali la kujiuliza kwa nini Harakati za Uhuru wa Tanganyika Ziliungwa mkono kwa nguvu kuu sana na Hasa Pale Mwalimu Nyerere alipoongoza TANU?
Unwritten History from Lake zone! UNCLE PASCAL MAYALLA atakuwa alishawahi kusikia au anaijua hii.
Alitokea Mtabiri (Mganga wa Jadi) Kutoka Sukuma Land kwa jina la Chalya( If not mistaken) Aliamka asubuhi moja kabla ya mwaka 1950,akawaaambia jamaa zake! Nalotaga elelo Nabhonaga Nzagamba ya pii elifumela Shashi,ele na Ng'wenda gupozu Eyeneyu Igwenha Butemi bhu Si Eyi Tafsiri( Leo nimeota nimeona Ng'ombe dume mweusi akitokea upande wa Ushashi ( eneo hilo leo ni toka Bunda mpaka Butiama) akiwa na Nguo ya kijani huyo Dume ndiyo atakayeleta utawala huru wa Nchi hii.
Hiyo ndiyo Hsitoria ambayo na sie tulisimuliwa na wazee wetu!( Oral History)
Naomba kuwasilisha.
Mnabuduhe, achana na hao malimbukeni, hawakuijua Tanganyika, hawaijui Tanganyika na hata siku moja hawatakuja kuijua Tanganyika wanayojaribu kuiongelea. Moto wa uhuru aliouwasha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Tanganyika iliyokuwa na watu karibu milioni nane (achana na Dar es Salaam iliyokuwa na watu hata kiganjani hawajai) jina la Nyerere liliwapa Watanganyika mori usio na mfanowe. Nani alimjua Abdul Sykes? Heri hata ya Zuberi Mtemvu aliyejaribu kupambana na Nyerere kwa kuanzisha chama pinzani, ANC.

Miongoni mwa baadhi ya Waislaam walioamua kujipima nguvu na Nyerere na kuanzisha chama cha kidini AMNUT walikuwemo hao wazee wa Mohamed Said lakini tsunami ya TANU haikuwaacha salama. Huu uchochezi wa huyu bwana anayedai kuandika eti historia ya kweli atawapata tu masalia ya AMNUT lakini akae akijua historia hawezi kufutika kwa hizi hadithi zake za kufinyangwafinyangwa.
 
Mnabuduhe,
TANU ilipoundwa hali ya siasa Tanganyika nzima ilikuwa imewiva.

TAA ilikuwa imafanya mambo makubwa ya kuhamasisha wananchi kuona madhila
ya ukoloni khasa baada ya Japhet Kirilo kurejea UNO mikono mitupu 1952 kufuatia
''petition,'' ya Meru Land Case na TAA ikaunda kamati iliyokuwa na wajumbe hawa:
Saadan Abdul Kandoro, Abbas Sykes na Japhet Kirilo iliyotembea nchi nzima
kuwaeleza wananchi dhulma za ukoloni.

Kuna kisa kizuri sana nimekieleza katika kitabu jinsi TAA Tabora walivyoshughulikia
tatizo la hali hii iliyokuwapo kabla ya kuundwa kwa TANU.

Ally Sykes alikuwa na mashine ya kudurufu aliyokuwa akiitumia kusambaza makaratasi
ya, ''uchochezi,'' dhidi ya serikali akiwaambia wananchi kuwa wajiunge na TAA kwa
kuwa kuna jambo kubwa linakuja.

Sasa Mwalimu Nyerere alipokuja kuchukua uongozi wa TANU katika hali ya hewa ya
siasa kama hii wananchi walikuwa tayari wanasuburi kuni wauwashe moto.

Lakini kubwa ni kuwa TANU ilikuwa na mabingwa wa kuzungumza, Sheikh Suleiman
Takadir, Bi. Titi Mohamed
na Julius Nyerere.

Hawa walikuwa wakipanda katika jukwaa wananchi walikuwa wanachemka.

Wale watu waliokuwa nyuma ya Nyerere walikuwa watu wenye sauti katika jamii kote
ambako TANU ilikokuwa.

Hii ndiyo siri kubwa ya Mwalimu Nyerere kufanikiwa katika kupambana na Waingereza.

2016%2B-%2B1
 
Tunaweza tukafanya mjadala mzuri wenye faida na tukaweka rekodi nzuri
ya rejea hapa JF wakawa watu wanatusoma na wananufaika.

Jiepushe na lugha kali.

Wewe unajua wazi kuwa mimi si limbukeni kwa hali yoyote utakayonifikiria
si mimi, si baba yangu wala si babu yangu.

Hakika Abdul Sykes hakuwa anafahamika na kila mtu nje ya Dar es Salaam.
Abdul akifahamika kwa viongozi wenzake wa TAA na hili si kwake yeye tu.

Lakini ukitaka kujua nguvu ya Abdul Sykes katika siasa za Tanganyika kwa
wakati ule soma Tanganyika Political Intelligence Summary za majasusi wa
Special Branch.

In Shaa Allah nitaweka, ''link,'' mwisho ili wasomaji wasome.
Wote hata Nyerere hakupata umaarufu kabla ya TANU.

TAA haikuwa na nafasi ya kufanya siasa ambazo viongozi wake wangekuwa
midomoni mwa wananchi.

Nyerere na viongozi wote wa TANU kama Bi. Titi Mohamed na wengineo
akina Oscar Kambona walifahamika baada ya kupanda jukwaa la TANU
mwaka wa 1954.

Mag3,
Unayosema kuhusu AMNUT huyajui unajisemea tu.

AMNUT ilipingwa na Waislam, ikajifia na haikupata nguvu yoyote.

Hakuna hata mmoja katika Baraza la Wazee wa TANU walioiunga mkono AMNUT.

Mmoja wa viongozi wake ni jamaa yangu bahati mbaya hapendi kuzungumza
kuhusu historia hii vinginevyo ningemhoji nikaweka hapa mazungumzo yetu.

Unazungumza mimi kuifuta historia rasmi?
Niifute mara ngapi?

Wewe uko na mimi hapa miaka nenda miaka rudi unajadili historia gani?
Historia ya Chuo Cha Kivukoni au historia ya Mohamed Said?

Msome Abdul Sykes katika taarifa za kijasusi za Waingereza.

Nyaraka hizi nimeletewa kutoka Rhodes House Oxford University:
Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952
 
Nimeamua kwa hiari yangu kuachana na huu mnakasha, nawatakia washiriki wote mtakaoendelea kila la kheri. Narudi kwenye mambo muhimu zaidi kitaifa yanayojiri katika uwanja wa siasa...

Mag3,
Hapana neno ndugu yangu uniwie radhi ikiwa kuna sehemu ulimi
umeniponyoka na lugha ikawa si ya kukupendeza.

Mjadala huu umenifurahisha kwa kiasi chake.
 
Salamu FaizaFoxy!
Uhuru wa Tanganyika kiini chake kikubwa ni Tanga,Dar es Salaam pamoja na Tabora!( Huko ndiko cheche za mapambano ziliruka sana) lakini huwezi puuza mchango wa watanganyika wote bila kujali Imani zao,kabila zao na unasibu mwingine.
Swali la kujiuliza kwa nini Harakati za Uhuru wa Tanganyika Ziliungwa mkono kwa nguvu kuu sana na Hasa Pale Mwalimu Nyerere alipoongoza TANU?
Unwritten History from Lake zone! UNCLE PASCAL MAYALLA atakuwa alishawahi kusikia au anaijua hii.
Alitokea Mtabiri (Mganga wa Jadi) Kutoka Sukuma Land kwa jina la Chalya( If not mistaken) Aliamka asubuhi moja kabla ya mwaka 1950,akawaaambia jamaa zake! Nalotaga elelo Nabhonaga Nzagamba ya pii elifumela Shashi,ele na Ng'wenda gupozu Eyeneyu Igwenha Butemi bhu Si Eyi Tafsiri( Leo nimeota nimeona Ng'ombe dume mweusi akitokea upande wa Ushashi ( eneo hilo leo ni toka Bunda mpaka Butiama) akiwa na Nguo ya kijani huyo Dume ndiyo atakayeleta utawala huru wa Nchi hii.
Hiyo ndiyo Hsitoria ambayo na sie tulisimuliwa na wazee wetu!( Oral History)
Naomba kuwasilisha.
Hehee nimecheka sana teheetehe
 
Nimeamua kwa hiari yangu kuachana na huu mnakasha, nawatakia washiriki wote mtakaoendelea kila la kheri. Narudi kwenye mambo muhimu zaidi kitaifa yanayojiri katika uwanja wa siasa...
Shukrani sana mzee wangu, umeitetea kweli na kweli imesimama wima na kuwa huru....
 
Mnabuduhe,
TANU ilipoundwa hali ya siasa Tanganyika nzima ilikuwa imewiva.

TAA ilikuwa imafanya mambo makubwa ya kuhamasisha wananchi kuona madhila
ya ukoloni khasa baada ya Japhet Kirilo kurejea UNO mikono mitupu 1952 kufuatia
''petition,'' ya Meru Land Case na TAA ikaunda kamati iliyokuwa na wajumbe hawa:
Saadan Abdul Kandoro, Abbas Sykes na Japhet Kirilo iliyotembea nchi nzima
kuwaeleza wananchi dhulma za ukoloni.

Kuna kisa kizuri sana nimekieleza katika kitabu jinsi TAA Tabora walivyoshughulikia
tatizo la hali hii iliyokuwapo kabla ya kuundwa kwa TANU.

Ally Sykes alikuwa na mashine ya kudurufu aliyokuwa akiitumia kusambaza makaratasi
ya, ''uchochezi,'' dhidi ya serikali akiwaambia wananchi kuwa wajiunge na TAA kwa
kuwa kuna jambo kubwa linakuja.

Sasa Mwalimu Nyerere alipokuja kuchukua uongozi wa TANU katika hali ya hewa ya
siasa kama hii wananchi walikuwa tayari wanasuburi kuni wauwashe moto.

Lakini kubwa ni kuwa TANU ilikuwa na mabingwa wa kuzungumza, Sheikh Suleiman
Takadir, Bi. Titi Mohamed
na Julius Nyerere.

Hawa walikuwa wakipanda katika jukwaa wananchi walikuwa wanachemka.

Wale watu waliokuwa nyuma ya Nyerere walikuwa watu wenye sauti katika jamii kote
ambako TANU ilikokuwa.

Hii ndiyo siri kubwa ya Mwalimu Nyerere kufanikiwa katika kupambana na Waingereza.

2016%2B-%2B1
Mzee Said Mohamed! Unarejea nzuri za kuunga mkono hoja zako! Hongera!
Lakini fahamu kuwa Julius Kambarage Nyerere Alitabiriwa! Ushawishi wake ulikuwa wa kipekee!mbele ya wazee wako Julius alipaa! Alitengwa kwa muhula wake! kwa Nyakati zake awe Musa wa Tanganyika.
Mwalimu ,Chief Erasto Andrew Mbwana Mang'enya Alipomuona Mwalimu mara ya kwanza Kipalapala Tabora walipokuwa wameenda kufanya kikao kisicho rasmi kwa kuwahofia Wakoloni hakumjua Nyerere ni nani! alimtazama kizembe kama ka kijana flani hivi wa kawaida sana! lakini siku chache baadae alikubali kuwa Huyu Mzanaki si wa kawaida kabisa! Ushawishi wake ulikuwa wa kipekee!( walipokutana kipalapala kanisani walikuwa Watanganyika bila kujali imani zao! ndio maana Desturi hii mpaka leo itadumu).
Nyerere was a Man of destiny! His influence was beyond normal.His life also teaches us that! He was the one! only among many to lead others to Independence.
Kwa heshima na Taadhima nakubaliana na wewe katika Hoja ya Unsung Heroes from all over Tanganyika!but I agree to disagree with you on one thing Your "Faith Chauvinism"! Inaweza kuchochea Ufa mkubwa utakao athiri Umoja wa Kitaifa.
Wasaalam.
 
Nimeamua kwa hiari yangu kuachana na huu mnakasha, nawatakia washiriki wote mtakaoendelea kila la kheri. Narudi kwenye mambo muhimu zaidi kitaifa yanayojiri katika uwanja wa siasa...
Tafadhali Mkuu! baki nasi! Ingawa pia naona kama unavyoona.
 
Mnabudehe,

Mimi nakuunga mkono kuhusu uwezo wa Mwalimu Nyerere.

Usisahau mimi nimefanya utafiti wa maisha yake kuanzia siku alipokutana na Abdul Sykes 1952 hadi uhuru unapatikana 1961 hadi siku anahudhuria maziko yake makaburi ya Kisutu 1968.

Katika utafiti wangu alipotia mguu Mwalimu nami nimepita kuanzia madras ya Sheikh Hassan bin Amir Mtaa wa Amani, Dar es Salaam hadi Parish Hall ya Kanisa Katoliki Tabora katika mkutano wa Kura Tatu.

Nimemsoma Mwalimu hadi alipoachana na wazee wangu wakaasimiana kimya kimya hakuna anaemuuliza mwenzake baada ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Mzee Idd Tulio kuvunjwa na wao kupigwa marufuku kufika ofisi ya TANU.

Kwa kiasi changu namfahamu Baba wa Taifa. Ninayo mengi.

Ama kuhusu umoja wazee wangu ndiyo walioujenga umoja huu.

Angalia picha za kupigania uhuru wa Tanganyika ni nani waliokuwa nyuma ya Baba wa Taifa?

Tujiulize nani aliyekuja kuuvunja udugu huu?

Jiulize kimepitika nini historia hii ya mashujaa wa uhuru ikafutwa?

Nani alaumiwe kwa dhulma hii?

Iweje leo watokee watu wachukizwe na historia hii na majina ya wazalendo hawa kila yakitajwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko serious? kama kiingereza hamkimudu tumieni kiswahili. Pia hii ungepeleka Jukwaa la biashara au historia.
Yeah Yericko Nyerere yuko serious ni kweli kama unataka hard copy unaweza kununua www.amazon.com wanakufanyia shipping popote pale ulipo !nini shida yako ?au unadhani katika mitandao kila kitu ni virtual?
Kebehi zisizo maarifa na akili ndicho mnachokijua tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good history to start with, lakini Yericko wewe si nasikia huwa unaandika vitabu? Kama ndivyo, mbona una punctuation mbovu kiasi hiki?

In addition, for your own benefit, hukutakiwa kuweka link kavu ya Amazon bali link ya hicho kitabu! Na hicho kitabu chenyewe binafsi nimeshindwa kukiona kupitia hiyo Amazon main link!
Unaingia amazon then unakisearch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom