Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 356
- 1,605
TUENDELEE NA HISTORIA YA CHAMA CHA (A.A).
Picha namba (1) inaonyesha jengo la ghorofa mbili lenye mistali ya rangi ya kijani na nyeupe, jengo hilo lilikuwa ni la chama cha African Association (A.A) alafu likatumiwa na TAA, alafu baadae TANU. Na pembeni yake kidogo kuna jengo la CCM.
Miaka ilivyozidi kusonga jengo la CCM likaunganishwa na jengo la A.A, baadae TAA, alafu TANU. Jengo hili lipo mtaa wa Lumumba na kariakoo Kama linavyoonekana hivi sasa katika muonekano mpya kwenye picha namba (2).
Kwanza tujiulize! Kleist Sykes haliupata wapi ujasili na moyo wa uzalendo wa kuwaamasisha marafiki zake kuunda chama cha African Association?
Ngoja nikuibie siri kidogo, ilikuwa mwanzoni mwaka miaka ya 1924, DR JAMES KWEGYIR AGGREY mwafrika kutoka GHANA kama anavyoonekana katika picha namba 3, ndiye aliye muamasisha Kleist Sykes kuingia kwenye siasa.
Ilikuaje? Ilikuwa hivi, Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924, kipindi icho alikua katika Phelps_Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya kuchunguza elimu ya waafrika.
Wakati anafika Tanganyika akiwa ndani ya kamisheni yake hiyo, Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Afrika Hotel kwa kuwa alikua mtu mweusi. Ndipo Gavana Cameron ilim'bidi amtafutie chumba Government House ajistiri kwa malazi
Wakati alipokuwa Dar es salaam ndipo Dr Aggrey, akakutana na Kleist Sykes. Baada ya mazungumzo wa muda mrefu baina yake na mgeni wake huyo, Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake vya siasa na akakitia sahihi yake.
Kwa kitendo icho alichofanyiwa na Dr Aggrey, Kleist Sykes alipata hamasa na mwaka 1929 Kleist na marafiki zake wa karibu wakaanzisha African Association (A.A). Kwa mchango aliohutowa Dr Aggrey katika nchi yetu, nasi bila hiyana tukamtunukia mtaa wenye jina lake.
Wahenga wenzangu hii ndio historia ya kweli kabisa ambayo imefichwa na watu wasiopenda Mimi, wewe na vizazi vyetu tuijue historia hii adhimu ya wapigania uhuru wa nchi yetu. Na vilevile historia hii, huwezi kuipata katika vitabu vya kufundishia mashuleni.
ASANTENI: