Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
- Thread starter
- #861
Kwabahati mbaya mzee wangu haujakisoma kitabu chsngu, ingekuwa busara ukisome kisha uulize maswali... Kwa waliokisoma wameona vema mwishoni mwa kitabu nimeweka nyaraka na rejea zote, swali la chanzo lingejibiwa hivyo...Yericko ninachouliza mimi nini chanzo cha habari za Cecil Matola.
Vitabu? Magazeti au nyaraka binafsi?
Historia nzima ya African Association kuanzia 1929 hadi 1949 mimi
nimeisoma kwenye nyaraka za Kleist Sykes.
Historia ya TAA 1950 hadi 1954 na kuundwa kwa TANU nimepata
kutoka kwa Nyaraka za watoto wake Abdulwahid na Ally Sykes.
Matola mwenyewe nimemsoma katika Nyaraka za Kleist na naamini
wewe ni baada ya kusoma kwangu ndiyo ukamjua.
Habari za Dr. Aggrey pia nimezisoma katika Nyaraka za Kleist naamini
pia wewe baada ya kumsoma kwangu ndipo ukamjua.
Kuwa AA iliasisiwa 1929 ipo katika Nyaraka za Kleist na picha ya ufunguzi
wa ofisi yote haya ni katika Nyaraka za Kleist naamini wewe baada ya
kunisoma mimi ndipo ukaja na mwaka wa 1927 kuwa ndiyo AA ilipoasisiwa
kitu ambacho si sawa.
Hivyo utaona uzito wa nyaraka za Kleist na watoto wake katika historia ya
TANU na uhuru wa Tanganyika na pia katika kumjua Mwalimu Julius
Nyerere.
Ninalouliza ni ''source,'' yako ni nini kwa uliyoandika kuhusu Cecil Matola?
Ikiwa umepata kutoka kwenye nyaraka zake binafsi baada ya miaka 85
hakika hili ni jambo kubwa sana ndiyo nakuomba utupe taarifa hizi tujue.
AA iliasisiwa 1927 na gavana wa kiingereza kama chama cha kushughulika na mambo ya starehe za watu weusi waliokuwa wamezuiwa kwenda kwenye maendeo ya starehe za wazungu huko mjini hasa katika ukumbi wa starehe wa Karijee leo NBC Garden ....
Matola amefariki 1933 wakati AA imeshazawadiwa jengo mtaa wa Stanley, leo Lumumba na leo ni makao ya TANU/ccm... Hoja ya kuwa ukoo wa Sykes ndio uliotoa jengo hilo ni uongo, labda tuseme waliteka umiliki baada ya Matola kufariki...kumbuka tangu afariki matola 1933 hadi achukue Nyerere madaraka 1953 chama hicho kilikuwa kama kikundi cha kahawa tu kisicho na dira... Baadae ndio chama kikaanza kuwa cha Siasa...