Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Kaka hivyo vitu vichache vya maana uliyoyaandika kuhusu AA, TA, TAA na TANU ni kama punje moja ya mchanga wa Baharini, kila mtu akiandika anachokitaka itakuwa ni fujo tu, na ndio maana uandishi wa Historia unakuwa na Historia rasmi na hii inapatikana baada ya kufanyika research ya kuangalia mambo gani ya msingi yanayopaswa kuwemo ndani ya hiyo historia inayoandikwa, Kama Nyerere kusaidiwa kitoweo na Mzee Kiyate ina uzito kweli wa kuwekwa kwenye historia? Nyerere kasaidiwa vingapi kila alipokuwa anapita?
hahhaahaha et mpaka kitoweo kwake historia,alinunuliwa kikombe cha kahawa nk
huyu ndo mwandish mamboleo
 
Mnabudehe,

Mimi nakuunga mkono kuhusu uwezo wa Mwalimu Nyerere.

Usisahau mimi nimefanya utafiti wa maisha yake kuanzia siku alipokutana na Abdul Sykes 1952 hadi uhuru unapatikana 1961 hadi siku anahudhuria maziko yake makaburi ya Kisutu 1968.

Katika utafiti wangu alipotia mguu Mwalimu nami nimepita kuanzia madras ya Sheikh Hassan bin Amir Mtaa wa Amani, Dar es Salaam hadi Parish Hall ya Kanisa Katoliki Tabora katika mkutano wa Kura Tatu.

Nimemsoma Mwalimu hadi alipoachana na wazee wangu wakaasimiana kimya kimya hakuna anaemuuliza mwenzake baada ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Mzee Idd Tulio kuvunjwa na wao kupigwa marufuku kufika ofisi ya TANU.

Kwa kiasi changu namfahamu Baba wa Taifa. Ninayo mengi.

Ama kuhusu umoja wazee wangu ndiyo walioujenga umoja huu.

Angalia picha za kupigania uhuru wa Tanganyika ni nani waliokuwa nyuma ya Baba wa Taifa?

Tujiulize nani aliyekuja kuuvunja udugu huu?

Jiulize kimepitika nini historia hii ya mashujaa wa uhuru ikafutwa?

Nani alaumiwe kwa dhulma hii?

Iweje leo watokee watu wachukizwe na historia hii na majina ya wazalendo hawa kila yakitajwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee Said Hebu tupe kisa cha Mleba huyu John Hatch alivyohutubia mnazi mmoja 1958!na alivyojaza watu wakati Julius akiwa mikoani!
 
Huyu ndie Mohamed Said wetu
Yericko,
Hakika ndimi Mohamed Said Salum Abdallah.

Mimi ndiye katika wakati mgumu watu wakiwa wamehofishwa
kuieleza historia ya TANU mimi nilikuwa na ujasiri si tu ule wa
kuwasahihisha waalimu wangu wa historia Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam kuwa historia wasomeshayo ina kasoro bali
kuieleza historia hiyo kwa ufasaha darasani na katika semina
zetu za masomo pale ilipobidi.

Sikuishia hapo nikaandika na kitabu.
Sikuishia katika kitabu.

Nimetoa mihadhara ndani na nje ya nchi kuieleza.

Nilipojiunga JF historia hii imevutia wasomaji wengi kiasi cha
kuweka rekodi ya mhadhara tuliojadili kwa miezi sita.

JF ilininyanyua sana kufanya nitambulike na watu wengi na hii
ikasaidia sana si tu katika kuisomesha historia ya wazee wangu
katika juhudi yao ya kuunda TANU na kupigania uhuru wa bali
na katika mauzo ya kitabu.

Historia ya wazee wangu imewafurahisha wengi na imewaudhi
wengi pia lakini hii ndiyo hali ya dunia.

Mwaka 2011 Abdulwahid Kleist Sykes na mdogo wake Ally
katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika 1961
wakatunukiwa medali ya, ''Mwenge wa Uhuru.''

Picha hiyo hapo nikiwa na watoto wa Abdul Sykes nimeibeba hiyo
medali ambayo nilikuwa bado sijaiona kwa kuwa nilikuwa nje
ya Dar es Salaam:

20170429_185254.jpg

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mohamed Said
Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes ni meshikilia Medali ya
''Mwenge wa Uhuru.'' aliyotunukiwa
Abdul Sykes katika kuadhimisha miaka 50 ya
uhuru wa Tanganyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Said Hebu tupe kisa cha Mleba huyu John Hatch alivyohutubia mnazi mmoja 1958!na alivyojaza watu wakati Julius akiwa mikoani!
Mnabuduhe,
Nakunyambulia kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

''Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa Kamati Kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia na Kambona walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee. Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu kazi ya ualimu. Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi. Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu. Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley. Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma. John Hatch alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Tutaona hapo baadae kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider Abdillah Plantan kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Ilikuwa wakati Nyerere yuko Musoma ndipo John Hatch kutoka Chama cha Labour cha Uingereza alipokuja Tanganyika kama mgeni wa TANU. TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja na Hatch akawahutubia wananchi. Inakisiwa takriban wanachama wa TANU na mashabiki wake jumla yao kiasi watu elfu ishirini walijitokeza kwenye mkutano huo. Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia. Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma. Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu.''

vanKMRu6CL-wyOJ8Hf9aR2l_oqFDte0uPqv_yHlw6wrWQ-beBmV7zAbq25-rnTUEx_dP8E2baZ8tij0i-B9ShSxodl1tpo0HzBjGcKMhJGTYPcezTT6dSF0FQnQnq_Hm2GMLePZ7rWenqTYdp0Xc9oTGFgjv7tJ07TaWIKE6dnPlTFN0zbBorBXWCinfSEE068oF4HNkuiyzfzYS9GtAn1szbAryXJqgkwuQQ7SeexCw6L0m9yn2WFNc4jHxzOoeVIoQCJ2ZK2v-eocoGu_wzymdJx34GJkd1W0B_AfMQvC7oVzBNxA0lK--R12CmWatKveO68v5z9pFplIc0tKoXjLns00IiKWCx8RnyuCqGmNLNGPgb3CfsIIDngtOtImyNKfs5jNhuI4z7OUndILBCebiKX7TEHyaOHU3ydrMmKV7sm7OMbEjA0_vUmzyvUifgnAMywfkbgwGzeE7qHwxDXHWRcCX5ICaZZyt9TKMlxdgDfC_J_JCQSvWY6pd63ggcO-ONjYtEE-2_e9E39iBCLcym9bji4d2kcjhD77bCqnOPqbJv2vgGrQufYUDLdoS2-Z9r1af6VDJBX5IndO3YYfQ1LlOFPdmmmvH_LPZPr69r5q5OQpIqF2jCBYhWAI8hIlvz1SgDSnq7r_4PGhLHmnRAZbX5kcrGZxSY7ClFx7V5Co=w880-h545-no

Kushoto: Bi Tatu bint Mzee, wa tatu Julius Nyerere, wa tano Bi. Titi Mohamed wakimsindikiza Nyerere safari
ya kwanza UNO 1955.

hNnzige34q-EadQqjYxSespSUXHUjLY3a_uF-LdJ44I2h22Z-bhXaDUbEUd1smw3v7kVBy-6Jk42jbVFjlgH4nsRbI_918egEZXeqlJ3ppTy5LiuVoY_Voxr1bGXrhLVPQZcUlbiIefTWGvxCTgyBDM0LS2QWI3OWrqNGDQsR6t6xOHbZY6BnKgI4TxuOiaIpHBVFUyqCeOuP89V73aiVF9M3XD1hrATvulJSmYiWeAQbSBd0lmaXHajyF8KKqokleOn8F3ShC9EsZubZrvn1X1drkdPCJRgBIn8lR_7YoMu-r6T1bKuk8PqQ3UmaW6Z3nMTPSz_-tJOMSNYU6YiuSyCFVmjZoMqe9ZKBSpEqFlacNSYAUoLCMWqKTxZxju_Elb6wHjlQNvs-dx_wJdBZTS8HQt_mMte8BdUJhsRgr-Alj5gvBhX_ENBKdiFE4pGGkxmhuHLMjTnzTZO7D4K3OowOlWcRqKbwbrEQqD4yqv_LYgPxZPjAxugGrpFIwxesS3Kzh-gzDV2sEHa-ENeHwuLFaUnA6DFAF06efOmu_QqP78ysKbplFAyC-ulumwxXVcSvB_DWAJ7QBAu3f5emAbHY54Gx7ZTMoUQm03pv1T3C2XkERgNFg=w850-h629-no

Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere.
 
yaan huyo 'dais' na hao nduguze soga zao kwako ndo reference ukiamin kwamb hawajatia chumvi chochote!
*huu msiba wa mudi
 
Mzee Mohamed

Wewe ni muongo sana, Nyerere ndie alikuwa rais wa TANU akiwa na uzoefu wa kimataifa akifahamiana na waingereza wengi na akiwemo John,

Nyerere ndie aliyeratibu na kuuleta ugeni huo Tanganyika, leo unasema alikuwa kijijini Mwitongo???

Aisee wewe ni muongo sijawahi kuona mzee wangu....

Hebu tujikumbushe hapa yaliyomo kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

_________________________________________________

Mwl. Julius Kambarage Nyerere, alipendwa na kuheshimika sana ndani na nje ya nchi. Mwaka 1985, aliamua kwa hiari yake mwenyewe, kuacha uongozi wa Taifa ili apumzike. Alizunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania. Kwa mapenzi makubwa, wakampa zawadi za kila aina. Wananchi walionesha wazi huzuni waliyokuwanayo kwa uamuzi aliouchukua. Walimuaga wakilia machozi!
Kumbukumbu muhimu ni hutuba yake, ya kuwaaga Watanzania, ya ter. 5 Novemba, mwaka 1985, kabla hajastaafu Urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam:
Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam, na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana, mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza, Oktoba 1952, miaka thelathini na mitatu (33) nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi (ushee). Niliporudi, nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini, nikiwa shuleni Chuo Kikuu nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo. Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.
Niliporejea nchini, hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari, nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi, anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Alishaniambia habari hizo, tangu nikiwa Makerere, Chuo Kikuu, nikiwa mwanafunzi.
Pale (Makerere), mimi na wanafunzi wenzangu tulianzisha chama kinachoitwa, Tanganyika African Welfare Association (TAWA), cha wanafunzi wa Tanganyika, mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.
Tukaona kwa nini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na si Tanganyika nzima? Kwa hiyo, nikawaandikia baadhi ya watu, Tanganyika. Nikasema, jamani eeh, tumeanzisha chama, kwa nini msianzishe huko matawi ya chama hicho?
Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia (nikiwa Makerere), akasema: “Wewe, kwa nini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).”
Kwa hiyo, la maana si kuanzisha matawi, maana Chama kipo na matawi yameenea. La maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo, mimi nikawa katibu wa katawi la TAA, hapo Makerere. Niliporudi Tabora, na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora. Kwa hiyo, nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo. Nilipelekwa na Kasela Bantu, ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.
Wakati huo, mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo, Anautouglou. Kwenye mkutano huu, wakanichagua kuwa Rais wao, wa TAA. Ninasema yote haya, kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo, Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana―cha matatizo.
Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana―katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.
Baada ya miezi kumi na mitatu (13), hapo mwaka 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani (Vita Kuu ya Pili ya Dunia) huko Burma. Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu, nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa miguu, kila Jumamosi. Baadaye, wazee wakanipa baiskeli, nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu, kufanya mikutano.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz, (na wengine wengi) waliokuwa ni wazee.
Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: “Wazee na Ndugu zangu!” Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa. Hawakuyumba hata kidogo. Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza. Nalo jambo lenyewe ni la hatari, la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi, na wapo waliopoteza kazi. Wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.
Nilikwenda Songea mwaka 1955, mara baada ya kujiuzulu. Huko, wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu, niliufanya na wazee kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.
Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya Vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa. Wakaona, mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza? Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya. Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa, uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tujitawale. Waingereza wanafanya ujanja, hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine, mpya (United Nations Organisation UNO), umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.
Kwa hiyo, nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao, wamesahau kabisa!
Wazee wakauliza: “Eeh, inawezekana?” Nikasema, inawezekana. Kazi yetu ya kwanza, ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi. Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo, kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi, hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.
Mzee John Rupia (marehemu), alikuwa mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: “Potelea mbali!”. Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.
Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: “Leo wazee wanakutaka.” Wapi? “Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku.” Nikasema, haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo(u), wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza. Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilizomalizika, zilikuwa za Kurani. Sasa, zikaja dua za wazee, za jadi. Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku naambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: “Tambuka!” Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: “Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!”
Sasa mimi Mkristo(u), hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini, tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo, nilitambuka pale na kuambiwa: “Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!” Wazee wangu wengine, wanakumbuka. Tulikuwa tunakwenda Bagamoyo (kwenye makaburi). Kwenye makaburi kule, tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.
Baadhi yetu mtakumbuka safari moja, jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu), walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga, tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 (za) jioni.
Baada ya mkutano, tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: “Sheikh, una Aspro?” Akajibu: “Kwa nini unataka Aspro?” Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kweli kweli. Akasema, S”ubiri.” Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia, akaniuliza: “Bado unataka Aspro?” Nikajibu, “Kichwa sasa hakiumi!” Kumbe ilikuwa njaa. Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.

Nyuma ya pazia, Mwl. Nyerere amebeba alama muhimu na rekodi za kipekee duniani. Alama hizo zinamfanya kuwa binadamu wa kipekee kabisa Afrika katika Karne ya Ishirini na Moja ( 21), alama hizo ni:
Alizaliwa tar. 13 Aprili, mwaka 1922, Butiama na kufariki tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, London, Uingereza. Ni Rais wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
Ni Rais wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo yake akiwa bado Rais.
Ni kati ya Marais aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani, na pengine kati ya rais aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma Chuo Kikuu nchini Uingereza, akiwa Mwafrika wa pili kupata Shahada nje ya Afrika: akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hutuba yake maarufu akisema kwamba,”Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia, bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana. Kwa hiyo, kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia.”
Ndiye mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini (Anti Apartheid Movement), mwaka 1959, pamoja na Trevor Huddleston, nchini Uingereza.
Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.
Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yeyote katika historia ya ukoloni. Nchi hizo ni: Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975, (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990 (Namibia) na 1994 (South Africa).
Mwaka 2009, alitajwa na rais wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama, Shujaa wa Waulimwengu Kuhusu Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice).
Amepokea shahada mbalimbali kutoka Vyuo mbalimbali ambavyo ni: University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa), Sokoine University of Agriculture (Tanzania) na Lincoln University (PA, USA).
Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba (1975), Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico (1975), Order of Amílcar Cabral, Guinea Bissau (1976), the Nehru Award for International Understanding (1976), the Third World Prize (1982), Order of Eduardo Mondlane Mozambique (1983), the Nansen Medal for outstanding services to Refugees (1983), Order of Agostinho Neto, Angola (1985), Sir Seretse Khama SADC Medal (1986), Joliot-Curie Medal of Peace (1988), the Lenin Peace Prize (1987), the International Simón Bolívar Prize (1992), the Gandhi Peace Prize (1995), Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi (2000), Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold), South Africa (2004), Royal Order of Munhumutapa, Zimbabwe (2005), Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master), Uganda (2005), Order of Katonga, Uganda (2005), National Liberation Medal, Rwanda (2009), National Liberation Medal, Rwanda (2009), Campaign Against Genocide Medal, Rwanda (2009), Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis, Namibia (2010), Tanzania Professional Network Award (2011), Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania (2011), National Order of the Republic (Grand Cordon), Burundi (2012) na Order of Jamaica, Jamaica.
Mwaka 2007, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo ambayo ni Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda, kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.
Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni, Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive, Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km) na Nyerere Road, Kisumu (2 km) nchini Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) nchini Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) nchini South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) nchini Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) nchini Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday (14/10), Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School, Mwanga District na J.K. Nyerere Secondary School, Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School, Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School, Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli Iringa Region, Nyerere Secondary School, Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre na Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.

Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha Declaration, Education for self-reliance, The Varied Paths to Socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, Uongozi na Hatima ya Tanzania, na Tujisahihishe.
Pamoja na kujulikana kama Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama Baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.
Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha, pia alifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.
Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopidia kama mtu pekee duniani katika historia ya Karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.
Binadamu pekee aliyeasisi Muungano wa aina yake duniani wa Tanganyika na Zanzibar (wa serikali mbili) na kisha kuikalia kijasusi Zanzibar kwa Nusu Karne.

Yote aliyoyaanza tangu utoto wake, makuzi yake, harakati zake, utuuzima wake, uzee wake, yalifikia kikomo tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, alipoaga dunia kwenye kitanda cha Hospitali ya Mtakatifu Thomas, mjini London, alikokwenda kwa matibabu. Kabla hajafariki dunia, aliwakumbuka Watanzania wake akisema: “Najua nitakufa, sitapona ugonjwa huu. Ninasikitika kuwaacha Watanzania wangu, najua watalia sana. Lakini nami nitawaombea kwa Mungu.” Naam, Watanzania wake walilia sana, walipopata taarifu za kifo chake. Mwili wake ulipoletwa nchini, waliomboleza kwa uchungu mno. Mwl. Julius Kambarage Nyerere alizikwa kijijini kwake, Mwitongo Butiama, kwa heshima zote na wananchi wa Tanzania na wmataifa mbalimbali wakiwemo viongozi mashuhuri, waliokuja kwa ajili ya mazishi.
Ni dhahiri, msingi wa yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia, utaendelea kudumu ndani ya mioyo ya kizazi chake, kizazi hiki na vizazi vijavyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa muasisi na Baba wa Taifa katika kujenga taifa la Tanzania. Huyo ndiye mtoto aliyezaliwa siku ya mvua, na kupewa jina la mzimu wa mvua, KAMBARAGE; mwana wa Chifu, Nyerere Burito na Mgaya wa Nyang’ombe. Ni dhahiri, tar. aliyozaliwa 13 Aprili, mwaka 1922, Mgaya hakujua kwamba ajifungua mtoto ambaye angekuja kuwa kiongozi mashuhuri sana Afrika na duniani, aliyewapenda binadamu wote na kuwatumikia Watanzania kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake zote.
 
Sijasema uongo.
Katika mkutano wa John Hatch, Nyerere hakuwapo alikuwa Butiama.

Huenda wewe hujui lakini nasomwa na watu wengi sana.

Siku hizo Nyerere akikaa nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya kuacha
kazi.

Siwezi kunyanyua kalamu nikaandika uongo kwani kufanya hivyo ni mie
kuishusha heshima yangu.

Nitakuongeza kiti kingine katika kipindi hiki ambacho Nyerere hakuweko
Dar es Salaam ndipo Bi. Titi kwa mara ya kwanza anakwea jukwaa la TANU
kuhutubia na mtu aliyemleta alikuwa Schneider Plantan.

Umemtaja Sheikh Mohamed Ramiyya.

Huyu alikuwa Khalifa wa Tariqa Quadiriyya na alikuwa na sauti kubwa katika
umma wa Waislam.

Bi. Titi kaingia TANU na kahutubia mkutano wa TANU wala hajakutana na
Nyerere.

Nataka nikufahamishe Nyerere alifikaje kujuana na Sheikh Ramiyya:

''Mwaka wa 1954 wakati TANU inaasisiwa Iddi Tosiri na ndugu yake Iddi Faiz Mafongo walikuwa na umri wa miaka 40 na zaidi kidogo na tayari walikuwa katika siasa za TAA na Al Jamiatul Islamiyya. Ndugu hawa wawili ni kati ya wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na TANU. Iddi Tosiri kadi yake ya TANU ni no. 24 na Iddi Faizi kadi yake ni no. 25. Iddi Tosiri alikuwa akiishi Mtaa wa Livingstone na Amani mwendo wa kama dakika 10 hivi kufika ofisi ya TANU New Street. Ndugu hawa wawili walikuwa na kaka yao mkubwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo, Khalifa wa Tariqa Qadiriyya. Katika kuipa nguvu TANU na kumtambulisha Nyerere kwa watu maarufu, Iddi Tosiri na Iddi Faizi walimchukua Julius Nyerere hadi Bagamoyo kwenda kumtambulisha kwa kaka yao Sheikh Mohamed Ramia. Sheikh Mohamed Ramia alikujakuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika. Nimebahatika kuonyeshwa na mtoto wa Iddi Tosiri, Maulid ‘’Chubby’’ Tosiri picha alizoacha marehemu baba yake Mzee Tosiri zikumuonyesha yeye mwenyewe na Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika. Nami kwa hisani ya familia hii naziweka hapa kama kumbukumbu ya mashujaa wa uhuru wa Tanganyika picha hizi tatu zilizofuatana.''

iQr8dxwBqbNywZNplVZwZ9uMaEoJn6FH7U9Vz82RFfUyDwBPmS79YGFUj3BtX7L5BSbq1mgLDKaW29M4S0oLOlsYKEKnzGd5ryDgu770NlL3RksESrq3DWwyjc5rwiELmNoxei-WbuMmlA_GNo9Lyp7DIIcy0ezP_Ji6UVXM8qbR0QpZ6zPOoKMV3QGNK7dJ6Lpg1TZB9mKKuV_be_Dp6fUXwouWkXllpvH2pfqlVeeJWbt0y9mY6pSSCRBH0R1Yxygt7p9_D1VCXzRj6axIVhHw6CHOs3ZOScIRK8nXUPJhD6TFFPwgNyGnvoK1nFHwtZO4h4avGoidHs5Q2Vj8NrPe74vskaycYEPyestd308LxxD9QFzn9pZiMFSP-hBtIn2qnB-Qf1nEkNxd6KiUQA5xBgvX51uLzFb3vB4SQFH4TStsCwB5F19tdLKN_P4cG4GW_HVtLtFkUrMK_Kc3-o6u4cNSYAz3Rus7NK2rQ6NnV4GnQ2MsKxcqjRTPzg3yhj1nGdhhC5lVcBq8wX4OjH-eJVkjEyRs141ROH0eJMqLQnfdolOwW2mpV-4hpcTBViAmJ8yTpwpuXqm0jzQgmoDSKaSOy6FYChwegvQl3XejpXxgfXJqOA=w839-h629-no

Aliyevaa koti jeusi ni Idd Tosiri na huyu mbele waliosimama wa pili kushoto ni Maulid ''Chubby'' Tosiri rafiki
yangu toka utoto.

4sm4-aiH2datxvGzUFX4Onlxv0KRZ2dTYkehir6Vg40ORv4KA5hmmLHPHcR5VevUa_TYTxr8JpILSIUGvE3PGaZr_P26AMTz8-EN6iPKrfb0Zi4QUwbQKrmWxgHQE3J8LpgFs_zxQ-bPTyNdm8mtQjHkXr11D-LX0oVazN6bmcQjxg4QyzcPXF-x0lxiq18YEx-0CCAbOQPolBtukOcGOfnqKT7_139_AOcitY74lRQyVPmSbGpke8h4HJqk2wfyElltw-AuOSlef9tQ6idPXRTwyS5SnFzQ4P1Gn71G8aJBe2uVmhP1rmcksXevaNT0Fp9loGoqlIY9giwp7vIYxOVvw2k8V0DteECRwdehUVoCh3PExI6B0uPQOb8dbT9-FIL1id8HboATpc3NKxbN44uI5Z3ruDRg6ybYbYy7Va0Di0OWvi1PY0B60Eq5_qY5IIhFiwjRM-OSeGOenEQtZUg1oF5D46BL4nTAZeZWhiNSBEEpgPgBUdegzBo2p_Ij7fiPZb8AJa4VbYDEQ1CIs-B7mEnvq7QcmMtfRzYUFqyZhP6fQfOMZjjo9LxaBYQZaZKthHBLJkvgzB2HZ1vtcHqP924LzIF3FEm-4WDS7YkOdNaOlAiM=w839-h629-no

Kushoto: Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu
Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma 1956.

3v9Fu_zLNVkRIkookbzuD2TQdFaIHNSYklchhMeRMZ0Z-pTO3OwjYxzQNNmTZFL_fQnY9je6gEsh0MvO6nwKtF7kjRtTjProPBUR1v-zT5yCTdUu-3XQJti-4Q2bwYIr2kwiPx0fWfD9HWht3MJD8sEHLV_KWumttYxjuPMMExx8c0dehgT-8J681vX1pXSjQmi-iES86s_9fR1Orhtdv0ScNcsRDFJDHa7Y-85HSuIqgYC0A2LNx0Y1AYkLIJaw-JMK-we83HORHMpfOqCVBK_imzPnwwasaUbipGE2LSS0u_LiVTbB8qA70f9XUyb-WmW28SroR8_y2OsuTno0wa5IRymdnw4ykjXRBL6hlxwRBOKN1VZ4F-1KYbJu0s_frf1zYS1OkX7XllNPGFTYkMlLwsDpZAnB3MIHUmZOk6-kRiHcME-ONM7M_CjcdSACvf4_51cc1vf_IwA_Fdq03_QSqZCuWwj0jztYDcQHw0Nun5o2biJ8QCHtsLGaUHS02M-a3_GvblrDKJTQ_pDJgzbAmqv8Fpv6N_ypBHQQp0i8kMjhmgkOoisXY6kjFhEe8ixyOCoBrCmhDXG3yzL_TXwiMTxdgQO4cmHld1i-Fq6wbhZAL3mQQA=w473-h629-no

Julius Kambarage Nyerere
Picha kwa kwa hisani ya Maulid ''Chubby'' Tosiri

Yericko,
Umeweka safari ya Nyerere Songea 1955.
Ngoja nikufahamishe ilikuwaje hadi Nyerere akafunga safari ile.

Ukweli ni kuwa safari ya kwanza ya Nyerere akiwa rais wa TANU
Morogoro na alifuatana na Zuberi Mtemvu.

Safari hii haikuwa na mafanikio:
''Mmoja wa wanachama wa mwanzo shupavu na msomi kabisa kujiunga na TANU alikuwa Zuberi Mtemvu. Mtemvu alikuwa akiishi mtaa wa Somali jirani na akina Sykes. Baba yake , Mzee Mwinshehe Manga Mtemvu, alikuwa amejenga nyumba yake nyuma ya nyumba ya Kleist. Kwa hiyo Mtemvu alimfahamu Nyerere mwaka 1952, Nyerere alipokuja kufahamiana na akina Sykes. Mtemvu alikuwa na kipaji cha kuzungumza kama alichokuwanacho Nyerere. Mtemvu alikuwa na kipaji cha kuweza kushawishi na kuwashirikisha watu katika harakati. Takriban mwezi mmoja baada ya kuundwa kwa TANU Nyerere na Mtemvu walikwenda kukifanyia kampeni TANU huko Morogoro ambako ndiko ilipokuwa asili ya ukoo wa Mtemvu.

Baba yake Mtemvu, Mzee Mwinshehe, alikuwa ameongea na baadhi ya wezee wenzake kuhusu TANU mjini Morogoro. Ijapokuwa Nyerere alijaribu kwa uwezo wake wote kuwafikishia watu ujumbe wa TANU matokeo hayakuwa mazuri. Katika barua ambayo Mtemvu alimwandikia Ally Sykes mnamo Agosti, 1954 aliwaelezea watu wa kabila lake kama, ‘’wagumu.’’ Katika barua hiyo Mtemvu alimjulisha Ally kuhusu mwanachama mpya wa TANU, msomi, Ally Mwinyi Tambwe. Mtemvu alimjulisha Ally kuwa Tambwe kukubali kujiunga na TANU lilikuwa ‘’jambo zuri sana.’’ Tambwe, Mngazija wakati huo alikuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika. Tambwe alimwahidi Mtemvu kuwaingiza TANU wanachama wengine ‘’wanaounga mkono,’’ harakati zile. Baadaye kidogo, mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya, Iddi Faiz Mafongo, akawa mweka hazina wa TANU.''
Angalia:
(Barua ya Zuberi M.M. Mtemvu kwa Ally Sykes, 15 th August, 1954. Nyaraka za Sykes).

Sasa hii safari ya Songea ilianzia Lindi na nakuwekea kisa chake hapo chini:

''Baada ya muda mfupi tu toka kufunguliwa kwa TANU Mkutano Mkuu wa Kwanza wa TANU wa mwaka 1955 ulifuatia. Tawi la Lindi lilikuwa tayari lina uhusiano na makao makuu ya TANU mjini Dar es Salaam, na lilikuwa likitarajia kuhudhuria mkutano huo na kukutana na Julius Nyerere na uongozi mzima wa TANU pale makao makuu Dar es Salaam. Salum Mpunga, mwanachama muasisi wa TANU, na Ali Ibrahim Mnjawale waliteuliwa kuhudhuria mkutano huo kama wajumbe kutoka Jimbo la Kusini. Halmashauri ya TANU ya Lindi iliwaelekeza wajumbe hawa wafikishe ombi rasmi kwa makao makuu ili Julius Nyerere aje kufanya ziara kusini kwanza, kukutana na wananchi na kufanya kampeni kwa ajili ya TANU na pili aje kupambana na propaganda dhidi ya TANU zilizokuwa zikitawanywa na Yustino Mponda. Mponda akitumia uhusiano wake na serikali ya kikoloni na nafasi yake kama mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria kutoka Newala; na vilevile akitumia ushirikiano wake wa muda mrefu na kanisa ambao bila shaka yoyote lilikuwa serikali ndani ya serikali kule kusini, alikuwa ameanza kampeni yake ya kuipinga TANU. Hili lilikuwa likiathiri msukumo wa uanachama. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbe waliotumwa na Gavana Twining kwenda Umoja wa Mataifa Februari, 1955 kwa niaba ya serikali ya kikoloni kwenda kuipinga. Uongozi wa TANU huko Lindi ulitaka Nyerere aende kupambana na Mponda akiwa katika uwanja wake mwenyewe, ndani kabisa ya ngome ya Ukristo wa Kikatoliki katika Tanganyika.''

Yericko,
Nina mengi lakini nachelea kuwachosha watazamaji wetu.
Tusimame hapa kwa sasa.
 
Mnabuduhe,
Nakunyambulia kutoka kitabu cha Abdul Sykes:

''Nyerere alilipeleka tatizo hili kwa Clement Mtamila, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mtamila aliitisha mkutano wa Kamati Kuu nyumbani kwake mtaa wa Kipata na TANU ilijadili tatizo hilo. Miongoni mwa wajumbe wa kamati ile mbali na Rupia na Kambona walikuwa Bibi Titi Mohamed na Bibi Tatu bint Mzee. Kamati Kuu ya TANU ilimshauri Nyerere ajiuzulu kazi ya ualimu. Tafarani hii ilitokea wiki chache tu baada ya kurudi kutoka Umoja wa Mataifa katika wiki za mwisho za mwezi Machi. Tarehe 23 Machi, 1955 Nyerere alijiuzulu ualimu. Ilikuwa adhuhuri Nyerere alipokuja Dar es Salaam kutoka Pugu, akiwa si mwalimu wa shule tena. Inasemekana aliposhuka tu kwenye basi alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Abdulwahid katika soko la Kariakoo kumpasha habari rafiki yake. Nyerere alikaa na Abdulwahid katika nyumba yake namba 78 Mtaa wa Stanley. Baadaye kidogo Nyerere alirudi kijijini kwake huko Musoma. John Hatch alipokuja Dar es Salaam kwa mwaliko wa TANU Nyerere alikuwa kwao kijijini. Tutaona hapo baadae kidogo jinsi mgeni huyu Mwingereza alivyomgutusha Schneider Abdillah Plantan kuhusu TANU kuwashirikisha wanawake katika harakati za kudai uhuru.

Ilikuwa wakati Nyerere yuko Musoma ndipo John Hatch kutoka Chama cha Labour cha Uingereza alipokuja Tanganyika kama mgeni wa TANU. TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja na Hatch akawahutubia wananchi. Inakisiwa takriban wanachama wa TANU na mashabiki wake jumla yao kiasi watu elfu ishirini walijitokeza kwenye mkutano huo. Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia. Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma. Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu.''

vanKMRu6CL-wyOJ8Hf9aR2l_oqFDte0uPqv_yHlw6wrWQ-beBmV7zAbq25-rnTUEx_dP8E2baZ8tij0i-B9ShSxodl1tpo0HzBjGcKMhJGTYPcezTT6dSF0FQnQnq_Hm2GMLePZ7rWenqTYdp0Xc9oTGFgjv7tJ07TaWIKE6dnPlTFN0zbBorBXWCinfSEE068oF4HNkuiyzfzYS9GtAn1szbAryXJqgkwuQQ7SeexCw6L0m9yn2WFNc4jHxzOoeVIoQCJ2ZK2v-eocoGu_wzymdJx34GJkd1W0B_AfMQvC7oVzBNxA0lK--R12CmWatKveO68v5z9pFplIc0tKoXjLns00IiKWCx8RnyuCqGmNLNGPgb3CfsIIDngtOtImyNKfs5jNhuI4z7OUndILBCebiKX7TEHyaOHU3ydrMmKV7sm7OMbEjA0_vUmzyvUifgnAMywfkbgwGzeE7qHwxDXHWRcCX5ICaZZyt9TKMlxdgDfC_J_JCQSvWY6pd63ggcO-ONjYtEE-2_e9E39iBCLcym9bji4d2kcjhD77bCqnOPqbJv2vgGrQufYUDLdoS2-Z9r1af6VDJBX5IndO3YYfQ1LlOFPdmmmvH_LPZPr69r5q5OQpIqF2jCBYhWAI8hIlvz1SgDSnq7r_4PGhLHmnRAZbX5kcrGZxSY7ClFx7V5Co=w880-h545-no

Kushoto: Bi Tatu bint Mzee, wa tatu Julius Nyerere, wa tano Bi. Titi Mohamed wakimsindikiza Nyerere safari
ya kwanza UNO 1955.

hNnzige34q-EadQqjYxSespSUXHUjLY3a_uF-LdJ44I2h22Z-bhXaDUbEUd1smw3v7kVBy-6Jk42jbVFjlgH4nsRbI_918egEZXeqlJ3ppTy5LiuVoY_Voxr1bGXrhLVPQZcUlbiIefTWGvxCTgyBDM0LS2QWI3OWrqNGDQsR6t6xOHbZY6BnKgI4TxuOiaIpHBVFUyqCeOuP89V73aiVF9M3XD1hrATvulJSmYiWeAQbSBd0lmaXHajyF8KKqokleOn8F3ShC9EsZubZrvn1X1drkdPCJRgBIn8lR_7YoMu-r6T1bKuk8PqQ3UmaW6Z3nMTPSz_-tJOMSNYU6YiuSyCFVmjZoMqe9ZKBSpEqFlacNSYAUoLCMWqKTxZxju_Elb6wHjlQNvs-dx_wJdBZTS8HQt_mMte8BdUJhsRgr-Alj5gvBhX_ENBKdiFE4pGGkxmhuHLMjTnzTZO7D4K3OowOlWcRqKbwbrEQqD4yqv_LYgPxZPjAxugGrpFIwxesS3Kzh-gzDV2sEHa-ENeHwuLFaUnA6DFAF06efOmu_QqP78ysKbplFAyC-ulumwxXVcSvB_DWAJ7QBAu3f5emAbHY54Gx7ZTMoUQm03pv1T3C2XkERgNFg=w850-h629-no

Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir na Julius Nyerere.
Nashukuru Mzee Said!Lakini Mbona rejea yako ni moja tuuuu!? Huna rejea za maandiko ya wasomi wengine ! Haya yote ulisimuliwa na Wazee wako? Kama rejea yako ni historia iliyohifadhiwa kichwani kwa mtu!(GRIOTS)Historia ya namna hiyo huwa na dosari nyingi!
Nilitarajia utamrejea John Hatch mwenyewe;
Two African statesmen: Kaunda of Zambia and Nyerere of Tanzania.
Au kitabu cha Kilichotafsiriwa na Mzee Paul Sozigwa- Mwalimu Nyerere. na vinginevyo.
Usiache kutumia rejea za wasomi wengine,Unawapa credit wazee wako tu! Huitendei haki historia.
Yericko Nyerere ameonesha rejea zake vema amejaribu kujenga hoja juu ya weledi na Kipawa cha julius Nyerere katika duru za siasa za Ukombozi wa bara la Afrika.
Mzee Said Kwanini unaamua kufanya hivo! Historia Unaifahamu vema! Kwanini kuipindisha ili Kuwapa credit kundi hilo ulilolikusudia?
Asante.
 
Ninazo rejea nyingi, ''primary source,'' na ''secondary source.''

Hapo nimekuwekea hiyo barua ya Mtemvu kwa Ally Sykes kwa kuwa ndipo
pake.

Lakini kama ungekuwa unanisoma katika kitabu ungekuta, ''source,'' nyingine.
Angalia hapo chini:

[209] Ulotu A. Ulotu, Historia ya TANU, (1971) p. 11.

[210] Julius Nyerere, Freedom and Unity, Dar es Salaam, 1966, p. 38.
[211] Kirilo Japhet and Earle Seaton, The Meru Land Case, Nairobi, 1966, p.16.

[212] John Hatch, Two African Statesmen, London 1976, p.17.

[213] M.H.Y. Kaniki, TANU, ‘The Party of Independence and National Consolidation’ in G. Ruhumbika (ed) Towards Ujamaa, Twenty Years of TANU Leadership, Nairobi, 1974, pp.1-2.

[214] Julius K. Nyerere, Tanganyika African Association, to Governor Edward Twining, 10 th August, 1953. Sykes' Papers.

Mnabudehe,
Usisite kuja na maswali mengine.

Lakini ningependa kukusikia kuhusu hayo niliokuwekea mwanzo kabla
Yericko hajaghadhibika na kunifedhehesha kwa kuniita muongo.
 
Sikutaka kuachanganya mambo ndiyo maana haya nisemayo hapa sikuyasema
hapo juu.

Nasema hivi kwa kuwa unasema kuwa Yericko ametumia rejea kujenga hoja
zake katika sifa za Mwalimu Nyerere.

Napenda kukufahamisha kuwa kitabu cha Abdul Sykes hakikuwa kabisa na nia ya
kushusha hadhi ya Mwalimu Nyerere.

Kitabu hiki kimeeleza namna TANU ilivyoundwa na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ningependa ujue kuwa mimi sijapatapo kuhoji sifa za Mwalimu Nyerere hata siku
moja kwani naamini hizo sifa zote ambazo Yericko kazieleza kwa hakika anastahili.

Ningependa pia uzingatie kuwa kitabu changu mimi kipindi chake ni kati ya 1900
- 1970 na miaka michache baada ya uhuru na sifa za Mwalimu Nyerere kazipata
baada ya uhuru wa Tanganyika.
 
Mnabudehe,
Sikutaka kuachanganya mambo ndiyo maana haya nisemayo hapa sikuyasema
hapo juu.

Nasema hivi kwa kuwa unasema kuwa Yericko ametumia rejea kujenga hoja
zake katika sifa za Mwalimu Nyerere.

Napenda kukufahamisha kuwa kitabu cha Abdul Sykes hakikuwa kabisa na nia ya
kushusha hadhi ya Mwalimu Nyerere.

Kitabu hiki kimeeleza namna TANU ilivyoundwa na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ningependa ujue kuwa mimi sijapatapo kuhoji sifa za Mwalimu Nyerere hata siku
moja kwnai naamini hizo sifa zote ambazo Yericko kazieleza kwa hakika anastahili.

Ningependa pia uzingatie kuwa kitabu changu mimi kipindi chake ni kati ya 1900
- 1970 na miaka michache baada ya uhuru na sifa za Mwalimu Nyerere kazipata
baada ya uhuru wa Tanganyika.

Mnabudehe,
Nadhani hii hapo chini utaipenda:

TAAZIA: RAFIKI YA PAUL SOZIGWA ANAMZUNGUMZA MZEE SOZIGWA RAFIKI YAKE WA ZAMANI
Mohamed Said May 12, 2017 0

DcyYzhP2SOjbvl27G-ztlUaJNhdts58kCo6fTXSQwjsvAvVn9sG-e5O7oDY0Dq9s6izBiiibhik=w328-h257-no

Paul Sozigwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Leo asubuhi mapema kabisa rafiki yangu mmoja wa Kariakoo kanifikishia taarifa katika ‘’whatsapp,’’ kuhusu msiba uliotufika wa Mzee Paul Sozigwa. Nami nikasita kusamabaza kwa kuhofu isije habari si za kweli maana umezuka mtindo wa maskhara ya kijinga. Si kama simwamini mpashaji wangu la hasha, ila wakati mwingine inapendeza kwa mtu kuchukua tahadhari.

Mzee Sozigwa ni jirani yangu nyumba kwa nyumba na wanangu wanamwita babu na mkewe bibi. Kwa ajili hii basi nikifahamu ugonjwa wa Mzee Sozigwa na kulazwa kwake hospitali. Lakini kubwa zaidi ni kuwa mke wangu na binti ya Mzee Sozigwa, Salome walikuwa mashoga wakati wanasoma pamoja shule ya Kisutu Girls kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kisha Korogwe Girls kidato cha tano hadi cha sita na baadae Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa ushoga huu wao basi mkewe Mzee Sozigwa kwetu sisi ni mama yetu.

Haraka sana baada ya kuthibitisha msiba nikampelekea taarifa ya msiba huu rafiki yangu ambae sitamtaja jina kwa kuwa sijamuomba ruhusa ya kutumia aliyoandikia kuhusu Mzee Sozigwa kwa hofu ya kunikatalia na hivyo kupoteza historia muhimu katika nchi yetu kwani hatoandika tena haya aliyoaniandikia.

Yeye Mzee Sozigwa alikuwa rafiki yake wa karibu sana katika miaka ya mwishoni 1970 wakikutana katika mapenzi ya club ya mpira ya Pan Africa ya Dar es Salaam. Siku zile tukikaa akinihadithia mengi katika ‘’massive intellect,’’ ya Mzee Sozigwa.

Lakini raha yenyewe iko hapa. Huyu sahib yangu Mashaallah ana kichwa si cha kawaida. Nitaweka hapa aliyoniandikia kuhusu Mzee Sozigwa nanyi mpate kufaidi. Sahib yangu anasema hayo hapo chini kuhusu Mzee Sozigwa:

‘’Nilipata kuwakaribu sana na Mzee Sozigwa na tukaelewana na kupatana sana zile enzi za mpira Pan African. Mimi tukaelewana sana katika siasa za mitaani zilizoingia katika vilabu vya Yanga na Simba. Tukijadili sana tukiwa na marehemu Sam Mdee. Nikagundua huyu ni mkali sana kichwani! Jumapili moja tuliangusha mjadala juu ya makala ikitoka katika Sunday News kila wiki katika miaka ya 1970. Ilikuwa ikiandikwa kutoka Uingereza. Ikiwa na, ‘’heading.’’ "What they Say about Us." Mdee alikwama katika ‘’analysis,’’ ya nini kilichojificha, ‘’between the lines,’’ ya ile makala ambayo siku ile ilikuwa ikionesha kumsifu Mwalimu. Nyerere. Mdee aliona sifa. Mzee Sozigwa hakuona hivyo. Mie nikawa mtu wa kuduwaa, tu. Wakati huo Mdee Mwandishi na Msaidizi wa Mwalimu Nyerere Ikulu.’’

Naomba tusimame hapa nieleze machache ya makala haya kwani rafiki yangu hakueleza muktadha yake lakini mimi na yeye tulipata mara kadhaa kuijadili na akanipa michapo ya Mzee Sozigwa jinsi alivyotembea katikati ya mistari ya huyu mwandishi Muingereza.

Kilichotokea ni kuwa huyu Mwingereza alikwenda kufanya mahojiano na Mwalimu Nyerere nyumbani kwa Mwalimu Msasani. Sasa aliporudi kwao akaandika makala na katika makala hayo kwanza, akaanza kwa kumsifia Nyerere na ‘’simplicity,’’ yake akasema watumishi waliokuja kuwaletea vinywaji walikuwa hawakuvaa nguo nadhifu hivyo na ukiangalia kama vile hazikupigwa hata pasi. Akaendela na kusema na ‘’juice,’’ aliyopewa ilikuwa ya moto haikuwa baridi akigongea labda nyumbani kwa Mwalimu hakuna jokofu kiasi inabidi wageni wake wanywe vinywaji vya moto.

Lakini jinsi alivyokuwa akieleza anakupa picha kuwa anamsifia Mwalimu kwa kutopenda makuu tofauti na viongozi wenzake wa Afrika mfano wa Mobutu waliokuwa wakiishi katika maksri.’’ Makala yale yalikuwa yanapita katika hali kama hii. Ni miaka mingi sana imepita siwezi kukumbuka kila kitu. Makala hii na mfano wa hizi zikawa zinachapwa na Daily News chini ya ‘’What They Say About Us,’’ wakati ule mhariri alikuwa Frene Ginwalla mama aliyekuwa akiwajua vyema Waingereza na vitimbi vyao na kejeli zao.

Sasa Mzee Sozigwa akawa anamwambia Sam Mdee, ‘’Huyu Mzungu hasifii huyu, huyu anaponda. Msomeni vizuri mtaona.’’ Lakini kama alivyoeleza sahib yangu, Sam Mdee yeye aliona Mwalimu kasifiwa kwa kutopenda makuu. Enzi zile zilikuwa enzi za siasa ya Ujamaa. Mzee Sozigwa yeye kaona Mzungu alikuwa anamdhihaki Mwalimu Nyerere na alikuwa na sababu nzito za kukubalika.

Huyu ndiye Mzee Sozigwa. Bingwa wa vijembe na kucheza na maneno, pia mtu wa kusikia yale ambayo hayakutamkwa, mpita katikati ya mistari ya waandishi. Hakuishia hapo tu. Paul Sozigwa akikaa nyuma ya ‘’microphone,’’ katika studio anasoma alichokiandika mwenyewe utasema yuko kakaa katika jamvi anazungumza na wewe na wala haitakujia fikra kuwa anasoma utadhani anasema.

‘’Topic,’’ yoyote atakayoizungumza katika radio wewe utamsikiliza hata kama hutaki. Huwezi kubadilisha stesheni wakati Mzee Sozigwa yuko hewani. Huo ni muhali mkubwa.

Sasa hebu turudi tena kwa rafiki yangu tumsikilize anavyosema kuhusu rafiki yake Mzee Sozigwa:

‘’Sozigwa Mkurugenzi TBC. Sozigwa akipenda kunibishia kila nilipokuwa na hoja ya kutoa ‘’Public Statement,’’ redioni kuhusu, ‘’controversies,’’ baina ya club na, ‘’other authorities.’’ Kumbe sababu yake kubwa ilikuwa kuni "shape" katika, ‘’thinking approaches,’’ zangu na hoja zake. Alifika mahali akawa na, ‘’great confidence,’’ kwangu na akizipenda hoja nilizozijenga; kiasi kwamba siku moja nilikuwa na, ‘’statement,’’ nzito na nyeti.

Tulianza kubishana ofisini kwake TBC. Aliporidhika akatoa amri nii ‘’record,’’ yote na itolewe hivyo katika kipindi cha michezo. Na ili kuhakikisha inatoka vizuri, aliamrisha mtu wa zamu aende kunirekodi katika, studio za ‘’External Services,’’ kulikokuwa na vifaa vya kisasa. Akaniweka jikoni studio, na ‘’recorder,’’ akawa, ‘’next room,’’ tunaenda kwa, ‘’signal lights.’’

Mimi binafsi namkumbuka Mzee Sozigwa katika mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Madola Singapore na TBC wakawa wanamrusha Paul Sozigwa mubashara kutoka Singapore mara baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Utafurahi na nafsi yako. Paul Sozigwa mwenyewe hatajitambulisha kama ‘’Paul,’’ bali, ‘’Paulo,’’na ‘’Singapore,’' ataitaja kama, ‘’Singapura,’’ na si bure anafanya hivi, hicho ni moja ya vijembe vyake kwa Waingereza kulibadili jina lake likae Kiswahili. Paul Sozigwa ataeleza yaliyopitika katika mkutano kisha atachomeka kijembe kidogo. Wakiwa Singapore iko siku ilikuwa ya mapumziko hakuna kikao. Ungetegemea siku hiyo pasiwe na kipindi mubashara cha Paul Sozigwa kutoka, ‘’Singapura,’’ hata kidogo, Paul Sozigwa akaingia katika kueleza viongozi waliojimwaga kucheza, ‘’golf,’’ ile siku ya mapumziko na viongozi wenzao katika viwanja.

Ukweli ilikuwa Paul Sozigwa alikuwa anawananga viongozi wa nchi za Kiafrika kuwa wao na ‘’golf,’’ wapi na wapi hasa wakati Afrika ya Kusini imekaliwa na Makaburu na nchi nyingine za Afrika bado ziko mikononi mwa wakoloni. Sasa njoo hapo anapoaga, ‘’signing off,’’ kutoka Singapore yeye ataaga kwa kusema, ‘’Huyu ni Paulo Sozigwa kutoka Singapura.’’
Iko siku Mzee Sozigwa alikuja nyumbani kwetu baada ya kutembelewa na Prof. Emmanuel Bavu kisha akamleta Prof. Bavu kwetu. Prof. Bavu alikuwa mwalimu wetu mimi na mke wangu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Siku zote Mzee Sozigwa tukisalimiana kijuujuu tu ninapomwona nje ya nyumba yake lakini siku ile nilikuwa karibu na yeye, kwangu mimi hii ilikuwa heshma kubwa na jambo la kihistoria. Nilimwomba tupige picha na alinikubalia.

Waandishi wa leo hasa watangazaji wana mengi ya kujifunza kwa Mzee Sozigwa.

Picha aliyoniachia Mzee Sozigwa ni kumuona kila Jumapili asubuhi bila kukosa akifuatana na mkewe kwenda kusali kwenye kanisa lao Kigamboni.

Naamini wanaomjua vizuri zaidi Mzee Sozigwa watamwandikia taazia stahili yake.

ua72xCDFYLJsD-h1uH5WhNO4dcHj8oH7ZFNXLenK9SlHt1Xq-yGOGPRGR9ur1TYgGz3nxLmGgwlqn9OXTn14aRX6a1xd3IS2m2b3NtU-VLAPxy1-ezGEF-xw1WoR7j6SiUw8UU-sYut1xQqBbp4bpXgcPQXKSadRTcsujpLTGlfJBaP6a4hduzy3hsSS3e_PQB9hgaVJ-B5iPDIDf9wb0yqlNhvQm8AW_5Fi6wZ_R2MF0zpqTg-Ov0kW8d4oU48Xl1-krfvlg9yVj-F9tPthdyfNwUkZMgLgsnIgDSljWHiCTWKGCou-JDP7jfUcMEM-iYUHrCIulzUMM9tV1ihahDuZ0uSExi2Es-QNAFBd7QDATGMSiHg0jLge-_OySEoh-xE_MLPF2fRfcU_TNalmisbg851CL2YMc7-zfnf-iG4Z4xpKihQgGDWV_A8c6kmmeVfLW6WoQPR1ZDtpTvA3xh2VrhSWsxCuX3FryMiOEJu02Cns08K1hxdr0pAihXQRzTq8-2YcOhUr_oZce1BkBygf2U8HyerQmc5wApY6PR3s3dSY8H6KH3qCZx1IrkVhijP0HmopQXsvZKh2QnEDeq56hNmnk-O_OF96uzh7SR2dAAsZ=w1038-h692-no

Kulia: Paul Sozigwa, Mwandishi na Prof. Emmanuel Bavu

Taazia
 
Mzee Mohamed

Wewe ni muongo sana, Nyerere ndie alikuwa rais wa TANU akiwa na uzoefu wa kimataifa akifahamiana na waingereza wengi na akiwemo John,

Nyerere ndie aliyeratibu na kuuleta ugeni huo Tanganyika, leo unasema alikuwa kijijini Mwitongo???

Aisee wewe ni muongo sijawahi kuona mzee wangu....

Hebu tujikumbushe hapa yaliyomo kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.

_________________________________________________

Mwl. Julius Kambarage Nyerere, alipendwa na kuheshimika sana ndani na nje ya nchi. Mwaka 1985, aliamua kwa hiari yake mwenyewe, kuacha uongozi wa Taifa ili apumzike. Alizunguka nchi nzima kuwaaga Watanzania. Kwa mapenzi makubwa, wakampa zawadi za kila aina. Wananchi walionesha wazi huzuni waliyokuwanayo kwa uamuzi aliouchukua. Walimuaga wakilia machozi!
Kumbukumbu muhimu ni hutuba yake, ya kuwaaga Watanzania, ya ter. 5 Novemba, mwaka 1985, kabla hajastaafu Urais aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam:
Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam, na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana, mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza, Oktoba 1952, miaka thelathini na mitatu (33) nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi (ushee). Niliporudi, nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini, nikiwa shuleni Chuo Kikuu nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo. Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.
Niliporejea nchini, hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari, nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi, anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Alishaniambia habari hizo, tangu nikiwa Makerere, Chuo Kikuu, nikiwa mwanafunzi.
Pale (Makerere), mimi na wanafunzi wenzangu tulianzisha chama kinachoitwa, Tanganyika African Welfare Association (TAWA), cha wanafunzi wa Tanganyika, mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.
Tukaona kwa nini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na si Tanganyika nzima? Kwa hiyo, nikawaandikia baadhi ya watu, Tanganyika. Nikasema, jamani eeh, tumeanzisha chama, kwa nini msianzishe huko matawi ya chama hicho?
Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia (nikiwa Makerere), akasema: “Wewe, kwa nini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo chama cha TAA (Tanganyika African Association).”
Kwa hiyo, la maana si kuanzisha matawi, maana Chama kipo na matawi yameenea. La maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo, mimi nikawa katibu wa katawi la TAA, hapo Makerere. Niliporudi Tabora, na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora. Kwa hiyo, nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo. Nilipelekwa na Kasela Bantu, ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.
Wakati huo, mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo, Anautouglou. Kwenye mkutano huu, wakanichagua kuwa Rais wao, wa TAA. Ninasema yote haya, kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo, Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana―cha matatizo.
Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana―katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.
Baada ya miezi kumi na mitatu (13), hapo mwaka 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani (Vita Kuu ya Pili ya Dunia) huko Burma. Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu, nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa miguu, kila Jumamosi. Baadaye, wazee wakanipa baiskeli, nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu, kufanya mikutano.
Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz, (na wengine wengi) waliokuwa ni wazee.
Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: “Wazee na Ndugu zangu!” Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa. Hawakuyumba hata kidogo. Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza. Nalo jambo lenyewe ni la hatari, la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi, na wapo waliopoteza kazi. Wengine wakaacha kazi. Akina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.
Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.
Nilikwenda Songea mwaka 1955, mara baada ya kujiuzulu. Huko, wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu, niliufanya na wazee kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.
Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya Vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa. Wakaona, mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza? Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya. Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa, uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tujitawale. Waingereza wanafanya ujanja, hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine, mpya (United Nations Organisation UNO), umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.
Kwa hiyo, nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao, wamesahau kabisa!
Wazee wakauliza: “Eeh, inawezekana?” Nikasema, inawezekana. Kazi yetu ya kwanza, ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi. Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo, kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi, hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.
Mzee John Rupia (marehemu), alikuwa mfanyabiashara na kaidi kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang’anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang’anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: “Potelea mbali!”. Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.
Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.
Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: “Leo wazee wanakutaka.” Wapi? “Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku.” Nikasema, haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo(u), wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza. Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilizomalizika, zilikuwa za Kurani. Sasa, zikaja dua za wazee, za jadi. Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku naambiwa, “Twining (Twainingi) umekwisha!” (Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: “Tambuka!” Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: “Basi nenda zako; tangu leo Twainingi amekwisha!”
Sasa mimi Mkristo(u), hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini, tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo, nilitambuka pale na kuambiwa: “Nenda nyumbani salama. Twaining hawezi tena!” Wazee wangu wengine, wanakumbuka. Tulikuwa tunakwenda Bagamoyo (kwenye makaburi). Kwenye makaburi kule, tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.
Baadhi yetu mtakumbuka safari moja, jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu), walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga, tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 (za) jioni.
Baada ya mkutano, tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: “Sheikh, una Aspro?” Akajibu: “Kwa nini unataka Aspro?” Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kweli kweli. Akasema, S”ubiri.” Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia, akaniuliza: “Bado unataka Aspro?” Nikajibu, “Kichwa sasa hakiumi!” Kumbe ilikuwa njaa. Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.

Nyuma ya pazia, Mwl. Nyerere amebeba alama muhimu na rekodi za kipekee duniani. Alama hizo zinamfanya kuwa binadamu wa kipekee kabisa Afrika katika Karne ya Ishirini na Moja ( 21), alama hizo ni:
Alizaliwa tar. 13 Aprili, mwaka 1922, Butiama na kufariki tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, London, Uingereza. Ni Rais wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
Ni Rais wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo yake akiwa bado Rais.
Ni kati ya Marais aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani, na pengine kati ya rais aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma Chuo Kikuu nchini Uingereza, akiwa Mwafrika wa pili kupata Shahada nje ya Afrika: akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hutuba yake maarufu akisema kwamba,”Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia, bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana. Kwa hiyo, kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia.”
Ndiye mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini (Anti Apartheid Movement), mwaka 1959, pamoja na Trevor Huddleston, nchini Uingereza.
Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.
Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yeyote katika historia ya ukoloni. Nchi hizo ni: Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975, (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990 (Namibia) na 1994 (South Africa).
Mwaka 2009, alitajwa na rais wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama, Shujaa wa Waulimwengu Kuhusu Haki za Kijamii (World Hero of Social Justice).
Amepokea shahada mbalimbali kutoka Vyuo mbalimbali ambavyo ni: University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa), Sokoine University of Agriculture (Tanzania) na Lincoln University (PA, USA).
Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba (1975), Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico (1975), Order of Amílcar Cabral, Guinea Bissau (1976), the Nehru Award for International Understanding (1976), the Third World Prize (1982), Order of Eduardo Mondlane Mozambique (1983), the Nansen Medal for outstanding services to Refugees (1983), Order of Agostinho Neto, Angola (1985), Sir Seretse Khama SADC Medal (1986), Joliot-Curie Medal of Peace (1988), the Lenin Peace Prize (1987), the International Simón Bolívar Prize (1992), the Gandhi Peace Prize (1995), Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi (2000), Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold), South Africa (2004), Royal Order of Munhumutapa, Zimbabwe (2005), Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master), Uganda (2005), Order of Katonga, Uganda (2005), National Liberation Medal, Rwanda (2009), National Liberation Medal, Rwanda (2009), Campaign Against Genocide Medal, Rwanda (2009), Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis, Namibia (2010), Tanzania Professional Network Award (2011), Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania (2011), National Order of the Republic (Grand Cordon), Burundi (2012) na Order of Jamaica, Jamaica.
Mwaka 2007, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo ambayo ni Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda, kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.
Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni, Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive, Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km) na Nyerere Road, Kisumu (2 km) nchini Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) nchini Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) nchini South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) nchini Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) nchini Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday (14/10), Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School, Mwanga District na J.K. Nyerere Secondary School, Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School, Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School, Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli Iringa Region, Nyerere Secondary School, Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre na Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.

Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha Declaration, Education for self-reliance, The Varied Paths to Socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, Uongozi na Hatima ya Tanzania, na Tujisahihishe.
Pamoja na kujulikana kama Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama Baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.
Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha, pia alifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.
Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopidia kama mtu pekee duniani katika historia ya Karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.
Binadamu pekee aliyeasisi Muungano wa aina yake duniani wa Tanganyika na Zanzibar (wa serikali mbili) na kisha kuikalia kijasusi Zanzibar kwa Nusu Karne.

Yote aliyoyaanza tangu utoto wake, makuzi yake, harakati zake, utuuzima wake, uzee wake, yalifikia kikomo tar. 14 Oktoba, mwaka 1999, alipoaga dunia kwenye kitanda cha Hospitali ya Mtakatifu Thomas, mjini London, alikokwenda kwa matibabu. Kabla hajafariki dunia, aliwakumbuka Watanzania wake akisema: “Najua nitakufa, sitapona ugonjwa huu. Ninasikitika kuwaacha Watanzania wangu, najua watalia sana. Lakini nami nitawaombea kwa Mungu.” Naam, Watanzania wake walilia sana, walipopata taarifu za kifo chake. Mwili wake ulipoletwa nchini, waliomboleza kwa uchungu mno. Mwl. Julius Kambarage Nyerere alizikwa kijijini kwake, Mwitongo Butiama, kwa heshima zote na wananchi wa Tanzania na wmataifa mbalimbali wakiwemo viongozi mashuhuri, waliokuja kwa ajili ya mazishi.
Ni dhahiri, msingi wa yale yote aliyoyaamini na kuyasimamia, utaendelea kudumu ndani ya mioyo ya kizazi chake, kizazi hiki na vizazi vijavyo kutokana na mchango mkubwa alioutoa akiwa muasisi na Baba wa Taifa katika kujenga taifa la Tanzania. Huyo ndiye mtoto aliyezaliwa siku ya mvua, na kupewa jina la mzimu wa mvua, KAMBARAGE; mwana wa Chifu, Nyerere Burito na Mgaya wa Nyang’ombe. Ni dhahiri, tar. aliyozaliwa 13 Aprili, mwaka 1922, Mgaya hakujua kwamba ajifungua mtoto ambaye angekuja kuwa kiongozi mashuhuri sana Afrika na duniani, aliyewapenda binadamu wote na kuwatumikia Watanzania kwa moyo wake wote, akili na nguvu zake zote.
Yericko Nyerere

Umenifanya nicheke peke yangu kwa upuuzi ulioleta hapa. Kwanza kwa maelezo yako yote hakuna kitu kipya tusichokijua ulicholeta ! Zaidi ya kunakili kila kitu kutoka kwenye sources mbali mbali bila ya hata kutoa credits kwa mtu or kazi ulikotoa hizi habari.

Lakini pia nilitegemea wewe Yericko Nyerere kuleta hapa habari yote kuhusu jinsi mkutano ulivyokuwa umeratibiwa na bwana Nyerere kama ulivyosema kuwa mzee Mohamed Said amepotosha and so wewe umekuja kurekebisha! Badala yake umezunguka zunguka hapa bila ya kuelezea vitu hivi muhimu! Kama unataka kujadiliana kihoja lete historia kama unavyoijua wewe ukiwa na vyanzo kama mzee Mohamed Said anavyoleta, sio unapinga then huelezi kilichojiri..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salamu FaizaFoxy!
Uhuru wa Tanganyika kiini chake kikubwa ni Tanga,Dar es Salaam pamoja na Tabora!( Huko ndiko cheche za mapambano ziliruka sana) lakini huwezi puuza mchango wa watanganyika wote bila kujali Imani zao,kabila zao na unasibu mwingine.
Swali la kujiuliza kwa nini Harakati za Uhuru wa Tanganyika Ziliungwa mkono kwa nguvu kuu sana na Hasa Pale Mwalimu Nyerere alipoongoza TANU?
Unwritten History from Lake zone! UNCLE PASCAL MAYALLA atakuwa alishawahi kusikia au anaijua hii.
Alitokea Mtabiri (Mganga wa Jadi) Kutoka Sukuma Land kwa jina la Chalya( If not mistaken) Aliamka asubuhi moja kabla ya mwaka 1950,akawaaambia jamaa zake! Nalotaga elelo Nabhonaga Nzagamba ya pii elifumela Shashi,ele na Ng'wenda gupozu Eyeneyu Igwenha Butemi bhu Si Eyi Tafsiri( Leo nimeota nimeona Ng'ombe dume mweusi akitokea upande wa Ushashi ( eneo hilo leo ni toka Bunda mpaka Butiama) akiwa na Nguo ya kijani huyo Dume ndiyo atakayeleta utawala huru wa Nchi hii.
Hiyo ndiyo Hsitoria ambayo na sie tulisimuliwa na wazee wetu!( Oral History)
Naomba kuwasilisha.
Ni vyema sana japo wewe umekuja na mistari ya kusadikika uijuayo kuhusu mtabiri wa kwenu.

Cha kushangaza ni pale Mohamed Said anapokuja na historia ikiambatana na mapicha kuhusu wazee wetu lakini watu inawauma badala ya wao kuchukuwa kalamu (key board) na kutuletea historia ya wazee wao au ya yeyote yule waijuwayo, badala yake wanapinga na hata wanachokipinga hawakielewi.

Wakiambiwa hata jina la TANU Nyerere alikuta limeshabuniwa miaka kabla hajakaribishwa Dar na wazee wetu, bado tu haiwaingii akilini.
 
Ni vyema sana japo wewe umekuja na mistari ya kusadikika uijuayo kuhusu mtabiri wa kwenu.

Cha kushangaza ni pale Mohamed Said anapokuja na historia ikiambatana na mapicha kuhusu wazee wetu lakini watu inawauma badala ya wao kuchukuwa kalamu (key board) na kutuletea historia ya wazee wao au yeyote ile wa ijayo, badala yake wanapinga na hata wanachokipinga hawakielewi.

Wakiambiwa hata jina la TANU Nyerere alikuta limeshabuniwa miaka kabla hajakaribishwa Dar na wazee wetu, bado tu hawaingii akilini.
Wazee wako usitake kuwapa umaarufu nyerere ndyo mkombozi wa Taifa hili
 
Sergio5,
Hakika Nyerere ndiye kiongozi wa harakati za TANU kudai uhuru wa Tanganyika.

Hili hakuna apingae ila TANU ina historia yake na halikadhalika Nyerere ana historia yake katika kudai uhuru wa Tanganyika.

Katika historia hizi mbili ndipo nikaandika kitabu cha Abdul Sykes.

Katika kitabu hiki ndipo yalipo mengi ambayo hayakujulikana na wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko Nyerere

Umenifanya nicheke peke yangu kwa upuuzi ulioleta hapa. Kwanza kwa maelezo yako yote hakuna kitu kipya tusichokijua ulicholeta ! Zaidi ya kunakili kila kitu kutoka kwenye sources mbali mbali bila ya hata kutoa credits kwa mtu or kazi ulikotoa hizi habari.

Lakini pia nilitegemea wewe Yericko Nyerere kuleta hapa habari yote kuhusu jinsi mkutano ulivyokuwa umeratibiwa na bwana Nyerere kama ulivyosema kuwa mzee Mohamed Said amepotosha and so wewe umekuja kurekebisha! Badala yake umezunguka zunguka hapa bila ya kuelezea vitu hivi muhimu! Kama unataka kujadiliana kihoja lete historia kama unavyoijua wewe ukiwa na vyanzo kama mzee Mohamed Said anavyoleta, sio unapinga then huelezi kilichojiri..!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ubavu,
Yericko
bado ni mwanafunzi katika uandishi.
Bado hajajua thamani ya mwandishi kuja na kitu kipya.

Anadhani unaweza ukakaa kitako na kunakili hapa na kunakili kule ikawa
ushaandika kitabu.

Nimejaribu kumfahamisha lakini ni mbishi hasikii la muazini, mnadi sala
wala la mteka maji.

Ubavu,
Ninalokusudia ni kutokana na maneno haya aliyosema Mwalimu Nyerere
siku alipozungumza na Wazee wa Dar es Salaaam Ukumbi wa Diamond:

''Wakati huo, mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo, Anautouglou. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo, Anautouglou. Kwenye mkutano huu, wakanichagua kuwa Rais wao, wa TAA.''

Inakuwa tabu sana kwa wasomaji kusoma yale ambayo yanakinzana na
historia rasmi na khasa inapomgusa Baba wa Taifa.

Mwalimu Nyerere anasema yeye kaikuta TAA chini ya uongozi wa Abdul
Sykes
''inasinzia,'' lakini ukienda katika historia na kuangalia hali ilikuwaje,
ukweli unapingana na kauli hiyo.

Tanganyika nzima hali ya siasa ilikuwa ikiwatisha Waingereza.
Angalia hali ilivyokuwa:

''Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha fedha za kupeleka msafara mwingine kwenda Umoja wa Mataifa kuueleza umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao. Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha Kandoro, Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo. Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa ampelekee Kirilo hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu. Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua. Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile kamati ilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na Shinyanga. Rais wa chama cha TAA, kanda ya ziwa, Paul Bomani aliipokea ile kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika jimbo lote. Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.''

''The TAA leadership at the headquarters organised a nationwide campaign to inform the people about the outcome of the Meru Land Case at the United Nations and to seek financial support to enable TAA to send another delegation to the United Nations to present and establish Tanganyika’s case as Mandate Territory seeking independence. A TAA committee composed of Kandoro, Kirilo and Abbas Sykes was formed for that purpose. Ally Sykes as the assistant treasurer was requested to send a money order to Usa River in favour of Japhet Kirilo to enable him travel to Dodoma to join the three-man TAA delegation. There was no money order facility at Usa River in those days and the money was held up at the post office for some time, but eventually Kirilo collected it from Arusha. [1] From 26 th September, 1953, for almost a month, the committee toured and addressed public meetings, collecting funds in Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma and Shinyanga. The president of TAA, Lake Province, Paul Bomani received the three-man TAA committee and addressed meetings with them in the province. Bomani told TAA members and all Africans in Mwanza of the importance of contributing generously to the cause.'' [2]

[1] Money order receipt to Usa River from TAA, details not legible and Ally Sykes handwritten notes. Sykes' Papers.

[2] Report ya Lake Province Kwa Kifupi Iliyotolewa na Bwana Abbas K. Sykes, Sykes’ Papers. Also see Japhet, op. cit. p.62.

Hali hii si hali ya kuwa TAA ilikuwa imesinzia na Nyerere akaja kuiamsha.

Ninayo mengi ambayo ningeweza kuyaweka hapa kudhihirisha kuwa hali
ya siasa Tanganyika kwa wakati ule ilikuwa ya kutia moyo sana.

(Nimeweka hiyo nukuu ya Kiingereza kwa sababu ya rejea kwani katika
Kiswahili rejea zinasumbua kidogo).
 
Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.

Si tupe basi ya kwenu? Vipi, kama hakuna, sema tu hakuna.

Wewe ulisikia wapi Nyerere akifanya harakati za kudai uhuru butiama au na wazee wa butiama?

Hao wazee wanaotajwa kwenye harakati za uhuru karibia wote ni wa Dar, 90% wazee wetu wa Kariakoo. Nyerere mwenyewe alipokelewa na kuwekwa Kariakoo kwa kina Abdul Wahid Sykes.

Leta raha za kudai Uhuru kutokea kwenu.

Haya mambo haya, ni balaa, Huyo Mohamed Said naye ni wakuja tu, wametoka Congo wakaishia Musoma, kisha wakaja Mzizima, naye ni wakuja tu, so hiyo history anayoandika ni story ya wazee wake wahamiaji sio wana Mzizima
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom