Kumbukumbu ya kuundwa kwa chama cha AA mwaka 1927 chini ya Sesilia Matola

Wanajamvi kwa mujibu wa Mohamed, maswali yamejaa lugha ya kughadhabika na shari. Maswali ni hayo hapo juu, kama kuna mahali lipo tatizo naomba mtu anionyeshe kughadhabika au shari, nitaomba radhi.

Kama hakuna Mohamed maswali yapo wazi ndani ya mada na maudhui, jamvi linakusikiliza

Hakuna jipya.

Maswali ni hayo kwa hayo, miaka nenda miaka rudi.

Kama mna jipya nje ya kitabu cha Alama Mohamed Said si mkilete?

Wewe hukubali kuwa katika hiyo kura wengi walikuwa ni Waislam? Leta list yako ya walio hudhuria.
 
Mimi nimezaliwa wakati ule harakati za uhuru zinaanza na wazee wangu walikuwa pale Gerezani walipokuwa wanaishi hawa watu akina Aziz Ally, Kleist Sykes, Omari Londo kuwataja wachache na walishiriki katika TANU.
Kwa mara ya kwanza kabisa, labda katika maisha yako yote, ni leo tu umepata ujasiri wa kuukiri ukweli...kwamba wakati unazaliwa ndio harakati za uhuru zinaanza. Zile hadithi za babu zako kuanza harakati za uhuru ni porojo tu ulizozitunga kwa malengo unayoyajua wewe tu. Ni uongo uliopitiliza kudai kwamba AA iliyoanzaishwa mwaka 1929 na Gavana wa wakati huo Cameroun kama klabu ya starehe kwa wasomi weusi ilikuwa na malengo ya kudai uhuru.

Hilo la kwanza na pili ni ukweli kuwa wakati Nyerere anahudhuria mkutano mkuu wa AA akiwakilisha jimbo la Tabora wewe ulikuwa hujazaliwa. Na kwamba viongozi wa AA walikuwa hawamjui Mwalimu Nyerere kabla ya mwaka 1953 alipohamia Dar es Salaam pia ni uongo. Mtu ambaye yawezekana hakumjua Mwalimu Nyerere labda ni Abdul Sykes peke yake kwa sababu nyakati hizo hakuwepo...tunaanza kumsikia tu pale alipoongoza uvamizi wa ofisi za AA kuwatoa wazee wake!

Tatizo kubwa alilo nalo Mohamed Said ni kwamba tunapompinga kwa kukosoa hadithi zake, utetezi wake ni kuturejesha kwenye hadithi zile zile na porojo zile zile. Je mtuhumiwa kujitetea kwa ushahidi wa yale yale anayotuhumiwa nayo inaingia akilini kama si sawa tu na kuzidi kujitia kitanzi. Anapoweka picha zake ama za wazee wake kama ushahidi maana yake ni nini? Anapotumia ukurasa mzima kunukuu yale yale aliyoyaandika na tunayoyakosoa, anataka kufikisha ujumbe gani?
 
Mag3,
Mimi sina tatizo kabisa na yote niandikayo.

Ikiwa wewe unaona ni porojo na unaamini historia rasmi ya Chuo Cha Kivukoni,
mimi sina tatizo.

Wala sijakulazimisha kunisoma.
Ukiona bandiko langu lipite tu kwa mbali ujisalimishe na porojo.

Atakae atasoma wewe usiotaka utakuwa umesalimika.
 
Hapa wanavyokusoma wa naona raha na wanaipata picha ya mambo yalivyokuwa, ila yao ni maradhi tu yaliyo mioyoni mwao "aah kwanini wazee wetu hawakuwemo".

Hebu Mag3, Nguruvi3, Yericko Nyerere na wale mnaofanana nao, tupeni historia za wazee wenu na mitaa yenu japo "kiduchu", nyie kufyonza tu ya Kariakoo? Makwenu vipi, hakukuwa na harakati za Uhuru?
 
"Mag3, post: 22924929, member: 10873"]
...Kuwa wakati Nyerere anahudhuria mkutano mkuu wa AA akiwakilisha jimbo la Tabora wewe ulikuwa hujazaliwa. Na kwamba viongozi wa AA walikuwa hawamjui Mwalimu Nyerere kabla ya mwaka 1953 alipohamia Dar es Salaam pia ni uongo.

Mtu ambaye yawezekana hakumjua Mwalimu Nyerere labda ni Abdul Sykes peke yake kwa sababu nyakati hizo hakuwepo...tunaanza kumsikia tu pale alipoongoza uvamizi wa ofisi za AA kuwatoa wazee wake!
Hili ni 'debunked' kwa kila kiwango.
Vipi HQ hawakujua wanawasiliana na nani katika tawi, wakati huo wasomi wakihesabika kwa kiganja

Hoja ya Mohamed kuwa aliyemwingiza Nyerere katika siasa ni Abdul ni uongo.
Nyerere akiwa Makerere tayari alikuwa na mwamko wa siasa, achilia mbali kwenda masomoni Ulaya
Tatizo kubwa alilo nalo Mohamed Said ni kwamba tunapompinga kwa kukosoa hadithi zake, utetezi wake ni kuturejesha kwenye hadithi zile zile na porojo zile zile.
Historia ya Abdul ipo miaka ya 1940 hadi 1953 kisha giza linatanda hadi 1968 wakati wa kifo chake

Miaka husika anairuka kwasababu ina mambo yanayopingana na ngano kwa ujumla wake
Utaelezaje miaka 7 bila kutaja AMNUT na Abdul Sykes ukihusisha na umaarufu na failure ya kuijenga AMNUT kwa kutumia watu wale wale aliokuwa nao?

Ni wazi, kwavile tangu 1953 hadi 1968 takribani miaka 15 Abdul haijulikani alifanya nini katika siasa.
Kuna sababu za kulaumu coverage ya msiba wake?
Anapoweka picha zake ama za wazee wake kama ushahidi maana yake ni nini? Anapotumia ukurasa mzima kunukuu yale yale aliyoyaandika na tunayoyakosoa, anataka kufikisha ujumbe gani?
Amenimaliza jana wakati analeta ushahidi wa wajukuu wa wazee kama ndiyo facts. Kwamba, Wanzagi mjukuu wa Nyerere anakuwa shahidi wa Nyerere!

Nilimuuliza kama Abdul alianzisha TANU ushahidi upo wapi?

Ukisoma kitabu na JF kuna sehemu anasema 'it's said that...' kwamba inasemekana ndiye mwasisi.
Mbele ya safari anashadidia akijua watu hawakuona maneno hayo na mantiki yake.
it's said ni presumption siyo fact

Kuna video aliweka ukimsikiliza anawaambia wasikilizaji, kabla ya mkutano wa Tabora Nyerere alimchukua ''X'' na kumwacha 'Z' kwenda kwa Sheikh Sembe Tanga.

Halafu anasema sababu za kumwacha 'Z' wasikilizaji watafute wenyewe.
Alichokwepa ni kutosema sababu za udini kwasababu hana ushahidi wa hilo

Anawaachia wasikilizaji waje na majibu akiwa ametengeneza mazingira ya majibu

Ninapumzika na uzi nisiwakoseshe watu fursa ya kufyonza
 
Hebu Mag3, Nguruvi3, Yericko Nyerere na wale mnaofanana nao, tupeni historia za wazee wenu na mitaa yenu japo "kiduchu", nyie kufyonza tu ya Kariakoo? Makwenu vipi, hakukuwa na harakati za Uhuru?
Ulimi uliponza kichwa wanasema
''Tunaambiwa hii ni historia ya kweli ya harakati za kupigania Uhuru Tanganyika''
Wewe unatuambia ni Historia ya Kariakoo, ulimi bwana!
 
Labda nimeuliza swali nje ya mada kwa kutaka mada ihamie baada ya uhuru, unabisha?
Ahaa nimekuelewa. Kabla ya uhuru kuna kiporo cha 1953-1961 kukihusisha AMNUT na Abdul.
Hapa panatakiwa hoja maana panarukwa sijui wanaofyonza wakati huo wanapata juisi au! Inaweza kuwa ni time out

Historia ni mtiririko wa matukio kama yalivyotokea.
Ukiondoa sehemu tu inakuwa tamthilia kama si ngano
 
Mag3, Mimi sina tatizo kabisa na yote niandikayo.
Mimi, kwa upande wangu nina matatizo sana na unayoyaandika...acha kupotosha jamii na maandishi ya kichochezi yaliyojaa simulizi zinazoweza kutumika kutugawa kwa namna yoyote ile. Wazee wetu wote walijitolea nafsi zao katika harakati za kudai uhuru bila kubaguana Kikabila, Kidini wala Kiutamaduni. Mbegu ambayo umeweza kuipandikiza na unayoendelea kuipandikiza lazima ipigwe vita na wote wanaoitakia mema nchi yetu.

Katika harakati zozote zile lazima wawepo viongozi lakini lazima awepo kiongozi moja anayewaunganisha na sisi kama Watanganyika aliyeweza kutuunganisha pamoja katika harakati za kudai uhuru alikuwa ni moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na katika hilo hana mpinzani. Ingawa ni kweli na hao wengine nao walitoa michango yao naomba tusiwaangalie kwa dini zao bali kwa utaifa wao.

Kama binadamu utawapata wengi sana watakaoamini hizo ngano zako na kuzimeza mazima mazima lakini pia wapo wengi ambao watatusoma na sisi wengine na kusikiliza upande wa pili na kujiuliza maswali kama haya tunayoyauliza. Kwa kejeli zako kwa wazee wetu Watanganyika kwa ujumla wao lazima watauliza lengo lako hasa ni nini? Ujumbe gani uliotaka kuufikisha kwa Watanzania wa leo.
 
Ulimi uliponza kichwa wanasema
''Tunaambiwa hii ni historia ya kweli ya harakati za kupigania Uhuru Tanganyika''
Wewe unatuambia ni Historia ya Kariakoo, ulimi bwana!
Naam ni ya Kariakoo, ndipo kitovu cha harakati za Uhuru.

Si tupe basi ya kwenu? Vipi, kama hakuna, sema tu hakuna.

Wewe ulisikia wapi Nyerere akifanya harakati za kudai uhuru butiama au na wazee wa butiama?

Hao wazee wanaotajwa kwenye harakati za uhuru karibia wote ni wa Dar, 90% wazee wetu wa Kariakoo. Nyerere mwenyewe alipokelewa na kuwekwa Kariakoo kwa kina Abdul Wahid Sykes.

Leta raha za kudai Uhuru kutokea kwenu.
 
Aaa kwetu nitaanzia Kiwanda, KM7 , Magila Muheza, Mkanyageni , Lusanga, Pongwe hadi 'Ndanga' au Tanga kwa Sheikh Sembe.
Historia itakuchoma moyo, ngoja tumalize hii ya ''Tanganyika'' unayotuthibitishia ni ya Kariakoo
 
Siyo Nansio?

Tanga baba'ko alihamia tu, sema kweli.

Usisahau na Kipumbwi.

Hilo la harakati kuanzia Kariakoo lisikipe shida, huo ndiyo ukweli.

Kasome wapi ilizaliwa TANU.
 
Mimi, kwa upande wangu nina matatizo sana na unayoyaandika...acha kupotosha jamii na maandishi ya kichochezi yaliyojaa simulizi zinazoweza kutumika kutugawa kwa namna yoyote ile. Wazee wetu wote walijitolea nafsi zao katika harakati za kudai uhuru bila kubaguana Kikabila, Kidini wala Kiutamaduni. Mbegu ambayo umeweza kuipandikiza na unayoendelea kuipandikiza lazima ipigwe vita na wote wanaoitakia mema nchi yetu.

Katika harakati zozote zile lazima wawepo viongozi lakini lazima awepo kiongozi moja anayewaunganisha na sisi kama Watanganyika aliyeweza kutuunganisha pamoja katika harakati za kudai uhuru alikuwa ni moja tu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na katika hilo hana mpinzani. Ingawa ni kweli na hao wengine nao walitoa michango yao naomba tusiwaangalie kwa dini zao bali kwa utaifa wao.

Kama binadamu utawapata wengi sana watakaoamini hizo ngano zako na kuzimeza mazima mazima lakini pia wapo wengi ambao watatusoma na sisi wengine na kusikiliza upande wa pili na kujiuliza maswali kama haya tunayoyauliza. Kwa kejeli zako kwa wazee wetu Watanganyika kwa ujumla wao lazima watauliza lengo lako hasa ni nini? Ujumbe gani uliotaka kuufikisha kwa Watanzania wa leo.

Mag3,
Narudia kusema kuwa sina tatizo na mawazo yako kuhusu historia hii.

Lengo langu ni kuihifadhi historia ya wazee wangu isipotee na nikiondoka
niache kumbukumbu ambayo itawasaidia waliokuwapo kujua nchi hii wapi
ilikotoka.

Ingekuwa sikufanya utafiti na kuandika mengi ya haya ambayo wewe hii leo
huyakubali yangekuwa yamepotea.

Kitabu kipo sasa miaka 20 na tunakwenda toleo la nne na ibra moja ambayo
hakika hata mimi hucheka ni kuwa kila mjadala unapopamba moto hapa na
kitabu ndivyo kinavyonunuliwa kwa wingi.
 
Hata tupe ya Kariakoo...usidandie ya wahamiaji wa Gerezani (Wazulu na Wamanyema) tupe ya Kariakoo ya Watanganyika.

Hata Nyerere alikuwa wakuja tu Kariakoo. Kumbuka hilo.

Na huko atokako huelewi kuwa ni wahamiaji tu?

Andrew Nyerere njoo utueleze asili ya ulipotokea ukoo wenu.
 
Mag3,
Narudia kusema kuwa sina tatizo na mawazo yako kuhusu historia hii.

Lengo langu ni kuihifadhi historia ya wazee wangu isipotee na nikiondoka
niache kumbukumbu ambayo itawasaidia waliokuwapo kujua nchi hii wapi
ilikotoka.
Ungekiri hivyo kutoka mwanzo wala hatungekuwa na ugomvi wowote...ni historia ya wazee wako, period. Ugomvi unakuja pale unapoanza kudai ni historia ya Tanganyika!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom