Kumbukumbu ya kifo cha Hayati Magufuli kwa upande wangu

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
KUMBUKUMBUYA KIFO CHA JPM KWA UPANDE WANGU.

Ilikuwa saa 5 usiku 17 March 2021. Nilikuwa ndani ya kuta za gereza la Ruanda mkoani Mbeya selo namba 16. Nikasikia kelele nyingi selo zingine ukizingatia kelele haziruhusiwi usiku mpaka kuwe na tatizo. Maana kelele ndio alarm ya kuwaita askari kuashiria kuna tatizo ndani ya selo husika. Sasa kwa uzoefu wangu nilijua kelele zile ni mtu kanyatiwa. Maana haiwezi kuisha wiki tukio la mtu kunyatiwa halijatokea.

Kwa waliokaa jela wanaelewa maaana ya kunyatiwa. Lakini kelele zile zilinishtua maana zilikuwa kelele za shangwe kiasi kwamba nikashtuka kuwa huenda kuna jambo la neema limetendeka.

Kipindi hicho nilikuwa na mgogoro mkubwa kati yangu na Bwana jela pamoja na mkuu wa Magereza mkoa RPO. Hii ni baada ya kuwachakaza kwa hoja nikiwawakilisha wafungwa na mahabusu kwenye mkutano uliofanyika gerezani mbele ya Kamishna wa Magereza Tanzania CGP, Naibu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani pamoja na wabunge sijui kamati gani.

Sasa siku hiyo yani tarehe 17 March 2021 Nyapara mkuu msaidizi wa ngome alipewa maagizo na afisa wa zamu mwenye cheo cha Inspector akimuagiza kwamba hakikisha Mdude na wapambe wake Wanahamishwa selo na wapelekwe selo namba 4.

Hii ilikuwa selo ya wagonjwa wa akili. Hivyo ilikuwa ni kawaida ukiwa na bifu na askari Magereza yoyote lazima akuhamishie selo hii kama adhabu. Maana mziki wa hiyo selo sio wa kitoto. Kumbuka wagonjwa wa akili wenyewe kwenye hiyo selo hawalali bila dawa za usingizi na wakati mwingine dawa za usingizi zikikata usiku wa manane kelele zinaanza. Wengine hujisaidia haja zote hapohapo walipolala.

Baada ya maagizo hayo Nyapara mkuu msaidizi akanifuata kabla ya mafungio kunijulisha huku akisikitika kuonesha kutokukubaliana na maagizo hayo ya boss wake. Nikamuambia asijali. Muda wa mafungio ulipofika nikiwa nimebeba Shako au mfuko wangu mkononi ambao ndani yake ulikuwa na chakula, maji, matunda na nguo nilienda moja kwa moja kwa wale maafisa wa zamu. Nikawahoji kuwa; "hivi mnavyoniona mimi nina akili timamu kiasi kwamba litakuwa tatizo mimi kukaa selo namba 4? Selo ya wagonjwa wa akili? Kwamba kuna selo nilitoka nayo nyumbani kuja nayo hapa?

Nilihoji kwa sauti ya juu lengo ni kutaka wafungwa na mahabusu waliokuwa karibu wasikie. Halafu nikaondoka zangu kwa mwendo wa madowido kwenda kupanga foleni selo namba 4. Ikaonekana kuwa aliyekuwa afisa mkuu wa zamu mwenye cheo cha ASP hakufurahishwa mimi kulazwa selo za vichaa hata kama nilikuwa na mgogoro na maboss wake. Akamuagiza Nyapara mkuu msaidizi anihamishie selo namba 16 kutoka selo namba 11 niliyokuwa nakaa awali badala ya kunihamishia namba 4. Lakini wapambe wangu wapatao wanne walipelekwa selo namba 4 huko.

Basi nikaingizwa selo namba 16 na tukawa tumefungiwa watu 82 huku mahabusu tukiwa wawili tu wengine wakiwa wafungwa. Kama ilivyokuwa kawaida yangu baada ya kufungiwa nikaenda kuoga halafu nikarudi sehemu yangu ya kulala nikafanya ibada nikafungua mfuko wangu nikatoa chakula nikala kisha nikakaa kwa kuegamia ukuta huku nikijisomea Biblia.

Sasa kwa mujibu wa taratibu za gerezani ni kwamba inapofika saa tatu kamili usiku ni muda wa kusikiliza taarifa za habari kutoka radio mbalimbali ambazo husoma taarifa za habari muda huo. Baada ya taarifa ya habari amri hutolewa na nyapara wa zamu ndani ya selo redio kuzimwa mpaka asubuhi wakati wa kusikiliza taarifa ya habari ya BBC.

Ni kwamba mpaka radio ya selo inazimwa saa nne kamili usiku kulikuwa hakuna habari mpya zaidi ya habari tunazozisikia kila siku. Basi tukalala zetu. Sasa kuna watu ambao wana radio zao ukiacha ile ya selo. Hivyo amri ya kuzimwa radio ikitolewa wao huendelea kusikiliza radio kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba ni ngumu kuwagundua. Naam hawa ndio waliosikia Rais Samia akitangaza kifo cha Magufuli mida ya saa tano.

Kumbuka katika utawala wa Magufuli alishawahi kuagiza wafungwa wapigwe mateke na wafanye kazi mfululizo. Lakini pia upande wa mahabusu kulikuwa na kilio cha kubambikiwa makesi halafu kesi zenyewe za mchongo na upelelezi haukamiliki miaka na miaka. Sasa wakati nasikiliza kwa umakini kelele zile kutoka selo jirani, nikasikia mmoja wao akisema; "Mungu amesikia kilio chetu huyu alisema tupigwe mateke na tufanyishwe kazi mfululizo".

Hapo ndio nikajua mkubwa JPM katutoka nikawaambia ile selo yetu washeni Radio Rais hatuko naye. Ni kweli wakawasha radio ndio nikamsikia rafiki yangu Samia akitangaza msiba wa taifa. Ndani ya selo sasa ,watu walishangilia wakaninyajua juu mpaka wakaniumiza enka ya mguu lakini hata sikuona ni tatizo kwangu pamoja na kwamba nilikuwa nachechemea.

Kifo kile kilinifundisha kwamba ukiwa na madaraka ni muhimu kuepuka kutesa na kuumiza watu wengine. Kwa sisi wakristo YESU alituagiza kwamba tusiwatendee wengine tusichotaka kutendewa sisi.

Kwa hiyo kama ni mkristo halafu ulitumia madaraka yako kuwatendea wengine usiyotaka kutendewa wewe hata tungeliombea kaburi lako mara elfu ni kazi bure mbele za Mwenyezi Mungu.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

FB_IMG_1625309421685.jpg
 
Aisee kamanda, kwanza nichukue nafasi hii ya kipekee kukukaribisha jamii forums. Lakimi pia nichukue nafasi hii kukupa pole kwa masahibu uliyopitia, lakini pia kukupongeza kwa mapambano uliyo yafanya enzi za JPM, na hata sasa.

NB: Siku moja ikikupendeza, uje pia na story kamili ya lile tukio la kuwekewa madawa ya kulevya na yule mtoto mkali kutoka Arusha! Hivi ilikuwaje kuwaje ukanaswa kirahisi na yule manzi?
 
View attachment 2556226
Pole Sana Mkuu msamehe tu huyo Jamaa
Rip John ur Legacy live on
 
Mbona husemi kuwa malinda yaliondolewa

USSR
 
Kuwa jela kwa sababu za kijinga! Hazimfanyi mtu kuwa shujaa!

Ninauhakika! Hata ungelimtukana M/kiti wa chama chako kwa matusi yale uliyoyaporomosha kwa Rais, usingebaki salama!

Sasa iwe kwa kiongozi wa nchi?

Hata ingelikuwa kwako wewe utukanwe hivyo na mwanao, hicho kibao Chake ambacho angekipata, sipati picha!
 
..wajinga ni wale waliompeleka Mdude magereza bila makosa yoyote.
 
Back
Top Bottom