Kumbukumbu: Rais Magufuli alimpandisha cheo Jaji wa kesi ya Kafulila

Kuuliza sio ujinga, naomba kuuliza utaratibu wa kupandisha vyeo majaji unaanzia kwa raisi au unaanzia wapi? Au inaanzia na jopo fulani la majaji kisha raisi anahidhinisha?
CC: Pascal Mayalla,
Petro E. Mselewa
Mkuu, utaratibu wa kupandisha majaji vyeo (vya uteuzi) unaansia kwenye tume ya utumishi wa mahakama, raisi anapelekewa mapendekezo tu. kazi ya raisi ni kuidhinisha. Tazama kifungu namba 29(1) cha sheria ya uongozi wa mahakama (The Judiciary administration Act, 2011. Act no. 4 of 2011).
 
Aliyempongeza kafulila mungu anamuona

Send by Nokia 3310 from mbalizi-mbeya
 
OKW BOBAN SUNZU,
Umefanya jambo zuri kugutuka kama great thinker kitu ambacho media house zingine za Tanzania hujifanya hazina kumbukumbu kabisa.

JamiiForums ndipo pekee ambapo kila kauli / tukio / hotuba / tamko n.k la kiongozi tujaribu kuona kama ni la Ukweli bila hila yoyote au propaganda za kutafuta Kiki .
 
Si ndiyo Rais huyu huyu alisema kamwe hatamteua mpinzani yeyote kwenye serikali yake, lakini hivi karibuni akamteua yule Profesa kutoka UDSM kutoka chama cha ACT kuwa Katibu Mkuu wizara ya maji na yule mama kutoka chama hiko hiko kuwa RC wa Kilimanjaro?

Unless atwambie kuwa ACT siyo chama cha upinzani bali ni CCM - B
 
Pongezi zile kwa Kafulila (hadi kujipigapiga kifuani kama Msamaria anafanya toba) ni mbinu tu ya kuwateka akili wasikilizaji. Ni namna ya kutaka uungwaji mkono kwa njia haramu. Na kuna wale wasioenda mbele zaidi kufikiria wataingizwa "machinjioni" wazimawazima.

Mtoa pongezi aliwahi kuwa mwalimu. Hivyo basi, anacheza kisaikolojia na hadhira. Na hadhira itasema... "haaa hata yule kasifiwa? Basi tumepata Mwokozi. Yulee alosubiriwa. Mpakwa mafuta..."! Ukiangalia vema utakuta kaficha jambia mgongoni. Kalagabaho!
 
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!
Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo. Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion. Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.
Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
Ww ni msemaji wa mahakama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine huwa nafikiriaga kumpongeza JPM kwa baadhi ya hatua zake lakini huwa najiuliza, sitokuja kuzijutia pongezi zangu?
Mkuu, nakuhakikishia lazima uje ujute katika maisha yako ikiwa utatoa pongezi kwa mfalme huyu. Haki ya Mungu na mitume yake utajuta tu.
 
Mkuu, utaratibu wa kupandisha majaji vyeo (vya uteuzi) unaansia kwenye tume ya utumishi wa mahakama, raisi anapelekewa mapendekezo tu. kazi ya raisi ni kuidhinisha. Tazama kifungu namba 29(1) cha sheria ya uongozi wa mahakama (The Judiciary administration Act, 2011. Act no. 4 of 2011).

Anakuuliza swali la kukuongoza (technical leading question) ili uingie mulemule anamotaka. Nia kuu ni kumuondolea lawama alomkusudia.

La muhimu kujiuliza ni, Je, kabla ya kuidhinisha upandishwaji wa cheyo alijiridhisha kwa sifa, historia na mwenendo wa mpendekezwa kwa kiasi gani? Na hapo ndiyo utapata jibu la zile sifa kwa Kafulila.

Utajua tu ni kuwa nia kuu ni ku - win mioyo ya hadhira iwe upande autakao na si vinginevyo.
 
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!
Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo. Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion. Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.
Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
Kuna baadhi ya mambo hayahitaji ushahidi sana kama hilo la jaji mazingira yanaonesha ukweli,kama ilivyokuwa kwa hakimu aliyemhukumu mbowe, muda mfupi baada ya hukumu akapandishwa cheo na kuhamishwa kituo cha kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usilolijua litakusumbua! Jaji wambali kabla ya kuwa jaji alikuwa msajili wa mahakama ya Rufaa. Kipindi hicho wasajili walikuwa wananguvu sana kimaamuzi katika utawala wa mahakama (hili usiniulize, kama hujui maana). Wambali alikuwa na msimamo dhabiti, hakuwaogopa wala kuwanyenyekea majaji pale alipoona masuala yao au madai yao ni ya kikazi (administration) zaidi. aliwahudumia kama watumishi wengine tu wa mahakama.
Alipopewa ujaji (kipindi cha utawala wa kikwete) Majaji wenzake walimtenga, hata wakati wa chakula ilibidi apelekewe chakula kwenya ofisi (chamber) yake mwenyewe. Alikuwa akijumuika na majaji wenzake kwenye chai au chakula majaji wote walikaa kimya, hakuna story. Akiwa bado jaji wa mahakama kuu Tabora, alitolewa kituoni kwake akapelekwa Lushoto (chuo cha mahakama) kuwa principal. Majaji wengine walifurahia wakisema hii ni demotion.
Hapa juzi kateuliwa kuwa jaji kiongozi, kuna majaji wamefurahia, kuna walionuna wakidhani atalipiza kisasi. Lakini huyu bwana hata hakumbushii kilichokuwa kinaendelea huko nyuma.
una swali zaidi?
Ulitaka kutueleza kitu gani? Kwa kuwa alikuwa akitengwa, basi akaonewa huruma baada ya kuhakikisha 'tumbili' anakosa ubunge?
 
Nakurudisha nyuma kidogo wakati kesi ya Kafulila ikitolewa na Jaji Wambari pale mahakama kuu ya Tabora. Moja kati ya kesi za uchaguzi zilizokuwa na mazonge zonge ni ile ya Kafulila na Hasna Mwilima. Yalisemwa mengi kwamba wazee wa Escrow walisimama kidete kuhakisha Davie hapati kitu

Mwisho mawakili wa Kafulila,msomi Tundu Lissu na Prof.Safari wakanyoosha mikono. Mara ngafla Jaji aliyetoa hukumu ile yenye maswali mengi akapandishwa cheo na Mh.Rais. Jaji Wambari akawa Jaji Kiongozi.......wajuzi tukasema hiyo ni asante au shavu kwa kazi nzuri.

Leo hii Kafulila anapongezwa kwa kazi nzuri ya kuwaumbua majizi ya Escrow....Huu sio unaa wakuu?Kama kweli majizi ya Escrow yanamuuma mbona waliobeba hela kwenye masandarusi kwenda ikulu hajawakamata?
Chadema hamna wema!
 
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!
Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo. Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion. Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.
Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
Tuthibitishie kwanza hayo ya kwako,lakini pia nani hajui figisu zilizofanyika kwa kafulila toka uchaguzi hadi kesi?
 
Back
Top Bottom