Kumbukumbu: Rais Magufuli alimpandisha cheo Jaji wa kesi ya Kafulila

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,191
103,716
Nakurudisha nyuma kidogo wakati kesi ya Kafulila ikitolewa na Jaji Wambari pale mahakama kuu ya Tabora. Moja kati ya kesi za uchaguzi zilizokuwa na mazonge zonge ni ile ya Kafulila na Hasna Mwilima. Yalisemwa mengi kwamba wazee wa Escrow walisimama kidete kuhakisha Davie hapati kitu

Mwisho mawakili wa Kafulila,msomi Tundu Lissu na Prof.Safari wakanyoosha mikono. Mara ngafla Jaji aliyetoa hukumu ile yenye maswali mengi akapandishwa cheo na Mh.Rais. Jaji Wambari akawa Jaji Kiongozi.......wajuzi tukasema hiyo ni asante au shavu kwa kazi nzuri.

Leo hii Kafulila anapongezwa kwa kazi nzuri ya kuwaumbua majizi ya Escrow....Huu sio unaa wakuu?Kama kweli majizi ya Escrow yanamuuma mbona waliobeba hela kwenye masandarusi kwenda ikulu hajawakamata?
 
Nakurudisha nyuma kidogo wakati kesi ya Tumbiri David Kafulila ikitolewa na Jaji Wambari pale mahakama kuu ya Tabora. Moja kati ya kesi za uchaguzi zilizokuwa na mazonge zonge ni ile ya Kafulila na Hasna Mwilima. Yalisemwa mengi kwamba wazee wa Escrow walisimama kidete kuhakisha Davie hapati kitu

Mwisho Tundu Lissu na Prof.Safari wakanyoosha mikono. Mara ngafla Jaji aliyetoa hukumu ile yenye maswali mengi akapandishwa cheo na Mh.Rais. Jaji Wambari akawa Jaji Kiongozi.......wajuzi tukasema hiyo ni asante au shavu kwa kazi nzuri.

Leo hii tumbiri anapongezwa kwa kazi nzuri....Huu sio unaa wakuu?
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!

Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo.

Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion.

Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.

Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
 
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!
Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo. Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion. Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.
Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
Mkuu usitufanye mafala , watu waishang'amua mapema , jaji anakuwaje adui wa majaji wenzake ?
 
Information-retaining capacity ya Mkulu imeporomoka kwa kasi ya ajabu sana OR level yake ya unafiki na uongo-uongo imekua kwa kiwango cha juu sana. Leo hiii JPM anampongeza Kafulila!?
 
.
Jaji wambari ana historia yake katika mahakama!
Kuwa jaji kiongozi ilikuwa ni mpango wa toka awali, tena usiyoyajua yatakusumbua. Jaji wambali hakupanda cheo kwa sababu ya kesi hiyo. Jaji wambali alikuwa na maadui wengi sana ndani ya mahakama kwa sababu ya upeo wake na nafasi aliyoistahili, ikafikia kipindi (tena baada ya kesi uliyoitaja) akapelekwa 'sehemu' ambayo kwa macho ya harakaharaka ilikuwa inaonekana ni demotion. Punde baada ya mahakama kuanza kupangika tena akaonekana anaestahili nafasi hiyo ya ujaji kiongozi.
Mleta mada tafadhali sana acha kuingiza siasa kwenye vyeo vya mahakama na watawala wake, vinginevyo uje na tafiti na vigezo vya kudhibitisha.
unasema Apache kuingiza siasa kwenye mahakama Wakati mahakama zina wabunge has a wale wanaofukuzwa vyama , mwanasiasa anaweza agiza kesi ivutwe toka mahakama hii kwenda ile, anaweza agiza hukumu zitolewe fedha ya itokanayo na ushindi kuipangia kabisa itafanya nini. Wanasiasa wanakatalia mahakamani wasikamatwe we usema Je?
 
Mkuu usitufanye mafala , watu waishang'amua mapema , jaji anakuwaje adui wa majaji wenzake ?

Usilolijua litakusumbua! Jaji wambali kabla ya kuwa jaji alikuwa msajili wa mahakama ya Rufaa. Kipindi hicho wasajili walikuwa wananguvu sana kimaamuzi katika utawala wa mahakama (hili usiniulize, kama hujui maana).

Wambali alikuwa na msimamo dhabiti, hakuwaogopa wala kuwanyenyekea majaji pale alipoona masuala yao au madai yao ni ya kikazi (administration) zaidi. aliwahudumia kama watumishi wengine tu wa mahakama.

Alipopewa ujaji (kipindi cha utawala wa kikwete) Majaji wenzake walimtenga, hata wakati wa chakula ilibidi apelekewe chakula kwenya ofisi (chamber) yake mwenyewe.

Alikuwa akijumuika na majaji wenzake kwenye chai au chakula majaji wote walikaa kimya, hakuna story. Akiwa bado jaji wa mahakama kuu Tabora, alitolewa kituoni kwake akapelekwa Lushoto (chuo cha mahakama) kuwa principal. Majaji wengine walifurahia wakisema hii ni demotion.

Hapa juzi kateuliwa kuwa jaji kiongozi, kuna majaji wamefurahia, kuna walionuna wakidhani atalipiza kisasi. Lakini huyu bwana hata hakumbushii kilichokuwa kinaendelea huko nyuma.

Una swali zaidi?
 
unasema Apache kuingiza siasa kwenye mahakama Wakati mahakama zina wabunge has a wale wanaofukuzwa vyama , mwanasiasa anaweza agiza kesi ivutwe toka mahakama hii kwenda ile, anaweza agiza hukumu zitolewe fedha ya itokanayo na ushindi kuipangia kabisa itafanya nini. Wanasiasa wanakatalia mahakamani wasikamatwe we usema Je?

Mahakama kuwa na mbunge haipo kwa sasa, acha uongo. Kama yupo ujue huyo anafanya kazi ya mahakama, sio ubunge.

Hakuna mwanasiasa anaeagiza kuhamishwa kwa kesi. Kesi inahamishwa toka mahakama moja kwenda nyingine kwa mpango na utaratibu maalum, wanasheria wanajua hii -ni mambo ya jurisdiction.

Kuipangia mahakama matumizi ya pesa ni kitu sahii kwa wahisani na viongozi. Mahakama ina bajeti yake na mhisani au mdau anaehusika kupanga bajeti na matumizi ya fedha za mahakama atakuwa sahihi kutoa mwongozo wa matumizi ya fedha.

Mwanasiasa kukatalia mahakamani haimaanishi kwamba mahakama ina siasa. Mtu akikatalia mahakamani kakatalia kwenye majengo ya mahakama tu, sio kwamba kakatalia mahakamani. Mahakamani au mahakama ikiwa kazini inadeal na masuala ya mahakama pekee, sio siasa.
 
Nakurudisha nyuma kidogo wakati kesi ya Tumbiri David Kafulila ikitolewa na Jaji Wambari pale mahakama kuu ya Tabora. Moja kati ya kesi za uchaguzi zilizokuwa na mazonge zonge ni ile ya Kafulila na Hasna Mwilima. Yalisemwa mengi kwamba wazee wa Escrow walisimama kidete kuhakisha Davie hapati kitu

Mwisho Tundu Lissu na Prof.Safari wakanyoosha mikono. Mara ngafla Jaji aliyetoa hukumu ile yenye maswali mengi akapandishwa cheo na Mh.Rais. Jaji Wambari akawa Jaji Kiongozi.......wajuzi tukasema hiyo ni asante au shavu kwa kazi nzuri.

Leo hii tumbiri anapongezwa kwa kazi nzuri....Huu sio unaa wakuu?

mkuu kafulila alionewa? na je kesi wanazoshinda chadema inakuwaje??

kafulila angeshinda ubunge....angeathiri nini CCM??

je kukamatwa kwa singh na rugemalira kuna maana gani?

kafulila alikiri kuwa alipata support ya IPTL kutoka kwa magufuli...unasemaje hili?

je huyo jaji alipandishwa cheo kwani kazi yake ilikuwa ni hiyo tu?
 
Back
Top Bottom