nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,683
- 14,066
Naam ni msoto baada ya kupoteza muelekeo kwa miaka kadhaa.
Kila kitu kilikwama kuharibika na kuchakaa.
Nguo viatu vyote viliisha yaani kuna mashati yalichakaa mpaka yakawa kama neti.
Habari ya kulala njaa ilikuwa jambo la kawaida sana,muhimu watoto wapate japo chai jioni.
Tulichakaa mpaka tukawa simulizi kwa majirani,sometimes gengeni na kwenye mangi shop hatukuaminiwa sababu ya ugumu wa kulipa.
Inapopatikana pesa kidogo mtoto anaugua hivyo pesa yote inakwisha.
Mifumo ya shughuli zangu ikabadilika nikawa napata riziki kwenye jua kali na huku nina njaa.
Sikukataa tamaa......nilikuwa sikosi nyumba ya ibada hata kama sina sadaka.
Ashukuriwe Mungu kuna mtu nilimtendea wema miaka mingi iliyopita na nilikuwa nimekwisha msahau.
Alinikuta nimechoka sana sana.....ingawa wengi kwenye hali hii walinikimbia....yeye hakufanya hivyo.
Nakumbuka maneno yake....mkuu haya si maisha yako.....kwa kifupi hata sura na muonekano kwa ujumla ulikuwa unatisha kwa kupigika na maisha na kuonekana kama mgonjwa....
Kwanza alinipoza na fedha kiasi...akanipa business card kwamba lazima j3 usubuhi niripoti ofisini.
Jumapili jioni naangalia nguo ya kwendea ofisini...sina....viatu sina...daah....
Nakumbuka niliamka alfajiri kupanda basi moja ili kusevu nauli......kipande kilichobaki nilichapa mguu...asubuhi kumepoa lakini nilisweti kimtindo.
Nilipokelewa kwa ukarimu ofisini hawakujali muonekano na mavazi yangu yaliyochoka.
Nilipigwa na A/C roho ikatulia.....nikasema kimoyomoyo Mungu saidia wanangu wasipite kwenye mateso kama haya......na kimsingi mateso waliyapata waziwazi.....dua na maombi yasirudie tena....AMEN amen 🙏