Kumbukizi: Miaka 6 sasa hatupo na Muammar Gaddafi!

Kumbukizi: Miaka 6 sasa hatupo na Muammar Gaddafi!

Hakuna binadamu asiekuwa na mapungufu!!!

So Namsifia kutokana na mazuri aliyowaletea wana-Libya.hata kama alikuwa na mapungufu yake lakini wananchi wake walinufaika! Maji bure,,umeme bure,,matibabu bure,,watoto wanasomeshwa bure,,mama mjamzito anapewa dola 5000 N.K___huyu mtu bado utamchukia jamani!!!! Kwanini binadamu hatutosheki/ridhiki tunachopewa!!___

So Libya ipi bora Mkuu?? alipokuwa akiiongoza yeye au libya ya sasa maelfu na maelfu wanauawa??? na wengine kufia baharini!!!

Binafsi hawa ndio maraisi nnao wakubali na watakumbukwa.

  1. Gaddafi
  2. Kagame
  3. Mulatu Teshome
  4. Ali Hassan Mwinyi.
  5. J.Kikwete
  6. Mkapa kwa mbali..
Tatizo lako standards zako ndogo.
 
Ndiyo maana hatuwezi kuelewana.

We mtu kasema atakwenda mlango hadi mlango kuwatafuta wapinzani wake awaue, unamsifia kwamba ni kiongozi mzuri huyo?

Kila mmoja na maono yake Mkuu___kwako ni mtu mbaya na kwangu mimi namuona kiongozi mzuri tu japo alikuwa na mapungufu yake. hivyo ni vyema tuishie hapo bwana Al-watan kama nimekuudhi tusameheane Asante!!
 
Kila mmoja na maono yake Mkuu___kwako ni mtu mbaya na kwangu mimi namuona kiongozi mzuri tu japo alikuwa na mapungufu yake. hivyo ni vyema tuishie hapo bwana Al-watan Ahsante!!
Kuna maoni, kila mtu anaruhusiwa kuwa na yake.

Lakini facts hazipindi.

Mtu anayeua ma jenerali wake yeye mwenyewe, kwa sababu za kijinga kama kutaka kuwapora wake zao, mpaka wakati wa vita anashindwa, mtu anayepindua ufalme kwa kusema mtawala mmoja hatakiwi kutawalakipindikirefu, halafu yeye anakuja kutawala miaka 42, mtu anayesema atawawinda wapinzani wake mlango kwa mlango mpaka awamalize, huyo siwezi kumuita kiongozi mzuri.

Hizo ni facts, si maoni.

Tafuta kitabu kinaitwa "Gaddafi's Harem: The Story of a Young Woman and the Abuses of Power in Libya"
by Annick Cojean.

Kasome ushenzi wa Gaddfi humo.

The terrible truth about Gaddafi's harem | Daily Mail Online
 
Tatizo lako standards zako ndogo.
Mtu mzuri hawezi kuzikwa na familia yake tu,dunia nzima ilisusa msiba wake.Mali asili ya Libya ( mafuta ) ndiyo yaliowaletea mafanikio Walibya.Gaddafi hakuwa na mali yake binafsi mfukoni kuwasaidia Walibya.Machafuko ya sasa huko Libya yamezalishwa na Gaddafi mwenyewe kwa kung'ang' ania madaraka kama vile Walibya wengine wote ni wajinga hawawezi kutawala.Wapinzani wanataka kutawala na wafuasi wake pia wanataka, hapo vita haitakwisha hadi mwisho wa dunia.Hii ni laana ya udikteta wa Gaddafi na ndio maana hata yeye alifia kwenye mtaro wa maji taka.Aliwazika watu wakiwa hai kwenye makaburi ya halaiki, na kafa akinywa maji machafu ya mtaro.
 
Napata mashaka na wewe yawezekana hata nyerere huwa unamtolea maneno ya kejeli
How could he rest in peace! Alikuwa anadondosha watu kwa siku moja kama mia sita hivi kwa bunduki baada ya kuanza kupingwa! Huyu ni moja ya majambazi yaliyopata kuongoza nchi! Usiamini maneno yake ya umoja na kwamba nitawapa helaa!
 
Mtu mzuri hawezi kuzikwa na familia yake tu,dunia nzima ilisusa msiba wake.Mali asili ya Libya ( mafuta ) ndiyo yaliowaletea mafanikio Walibya.Gaddafi hakuwa na mali yake binafsi mfukoni kuwasaidia Walibya.Machafuko ya sasa huko Libya yamezalishwa na Gaddafi mwenyewe kwa kung'ang' ania madaraka kama vile Walibya wengine wote ni wajinga hawawezi kutawala.Wapinzani wanataka kutawala na wafuasi wake pia wanataka, hapo vita haitakwisha hadi mwisho wa dunia.Hii ni laana ya udikteta wa Gaddafi na ndio maana hata yeye alifia kwenye mtaro wa maji taka.Aliwazika watu wakiwa hai kwenye makaburi ya halaiki, na kafa akinywa maji machafu ya mtaro.
Asante.

Kwa nini watu wengi wanakuwa hawaoni udikteta wa Gaddafi na ulivyoleta halihii ya sasa? Wanamfanya Gaddafi kuwa ni bonge la hero fulani hivi!
 
Ukiona watu wameanza kukupinga na wameanza Andamana ili uishi vizuri kimbia mapema
 
Sijui Nani mbaya, waliomuua na kuifanya Libya kuwa jehanamu, adui mkubwa wa afrika na dunia nzima ni mmarekani na mwingereza, ghadafi alitetea demokrasia ya kizazi kibishi cha sasa
 
Kwahili waafrika tujilaumu mpaka kufa,ujinga wakukubali Jambo bila kupima impact yake kwasabb za kibinafsi uishe sasa ,nauhakika huu upumbavu bado unawauma kichwa viongozi wa Africa
 
Huo UHURU NA HAKI wanautumia sasa huko libya ni akil finyu za waafrica wachache

..Gaddafi angesimika utawala wenye haki na uhuru hayo unayoyaona Libya leo hii yasingetokea.

..kuna nchi ni masikini kuliko Libya, lakini viongozi wake wamedumisha amani kwa kutawala kidemokrasia na kuzingatia utu na uhuru wa wananchi.
 
hakuna cha mzimu wala nini. He's dead and gone na Libya inasonga mbele. by the way, he was the worst dictator this world has ever seen.
Tumeona Libya sasa imekua na maendeleo kuliko kipindi cha Gaddaffi,amani imetamalaki na maisha yamekuwa mazuri sana
 
Sijui Nani mbaya, waliomuua na kuifanya Libya kuwa jehanamu, adui mkubwa wa afrika na dunia nzima ni mmarekani na mwingereza, ghadafi alitetea demokrasia ya kizazi kibishi cha sasa
Wa Marekani na Waingereza ndo waliomweka Gaddafi madarakani ili ang'ang'anie halafu tena ndo hao hao wàlisaidia kumwondoa kwa nguvu?
 
Wa Marekani na Waingereza ndo waliomweka Gaddafi madarakani ili ang'ang'anie halafu tena ndo hao hao wàlisaidia kumwondoa kwa nguvu?
51f0f2656cc23541282fd2d9e6ad0122.jpg
 
Back
Top Bottom