Kumbuka; Viumbe hatari hupenda kujificha

Limebarikiwa tumbo lililokuzaa ndugu muandishi.....hakika kazi za mikono yako kupitia kalamu vinakamilisha dhumuni la uwepo wako hapa duniani.....

Uandishi wako
Mpangilio wa uandishi wako na ujumbe uliopo kwenye maandishi vinanifanya nikiri kwa nafsi na kinywa kupitia mikono yangu kuwa wewe ni nguli wa fasihi..... barikiwa sana.....

Nashukuru Sana Mkuu.
Nafarijika kusikia haya.
Barikiwa zaidi Mkuu
 
Watu hatari hawajifichi wanakifivha ni wasumbufu tu elewa hili

Sawa Mkuu. Wala tusibishane kuhusu hili.

Ila siku ukianza kuwa mtu hatari na mbaya utaelewa falsafa ya watu Hatari.

Au Anza hata kuchepuka Kwa Mkeo utaelewa ni kwanini watu hatari na Wabaya hujificha.
Au Mkeo akianza kuwa mtu hatari Dalili ya Kwanza ni kutaka kuficha au kujificha
 
KUMBUKA; VIUMBE HATARI HUPENDA KUJIFICHA.

Anaandika, Robert Heriel.

Moja ya sifa kuu ya kiumbe hatari ni kupendelea kujificha, kukaa mafichoni, kukaa chobingo.
Hawapendi kujianika Anika hovyo, kujidhihirisha hovyo.
Kwanza weka akilini kuwa Kiumbe hatari hujijua kuwa yeye ni hatari, tena hujijua yeye ni mbaya asiyehitaji mchezo.

Nyoka, Nge, Tandu, buibui wang'atao ni miongoni mwa wadudu hatari kubwa, hawa hupenda kukaa mafichoni.
Na hata akiingia ndani ya nyumba yako hawezi pita sehemu wazi inayoonekana, lazima atembee na laini ya ukuta chini ili akitembea usimuone.

Viumbe hatari na Wabaya hupendelea giza katika harakati zao. Kwao nuru ni adui mkubwa.

Ukienda Mbugani ni ngumu Sana kuwaona Wanyama hatari, kama vile Chui, Simba, chatu, Koboko, Cobra, n.k.

Saikolojia ya viumbe hatari ni kutokuwa na Imani na yeyote. Muda wote wako machomacho, kujihami, n.k. pia viumbe hatari hupendelea Ambush, naam ndio shambulizi la kushtukiza.

Katika Maisha wapo watu hatari, na watu hatari siku zote wanatabia hizohizo.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Fact mkuu
 
vp wale wa sehem za kuungama,anakuona ila wewe haumuon,je! nawao ni hatar
 
Back
Top Bottom