Kumbuka; Viumbe hatari hupenda kujificha

Limebarikiwa tumbo lililokuzaa ndugu muandishi.....hakika kazi za mikono yako kupitia kalamu vinakamilisha dhumuni la uwepo wako hapa duniani.....

Uandishi wako
Mpangilio wa uandishi wako na ujumbe uliopo kwenye maandishi vinanifanya nikiri kwa nafsi na kinywa kupitia mikono yangu kuwa wewe ni nguli wa fasihi..... barikiwa sana.....
Unatumia ID nyingine kujipakulia nyama?
 
KUMBUKA; VIUMBE HATARI HUPENDA KUJIFICHA.

Anaandika, Robert Heriel.

Moja ya sifa kuu ya kiumbe hatari ni kupendelea kujificha, kukaa mafichoni, kukaa chobingo.
Hawapendi kujianika Anika hovyo, kujidhihirisha hovyo.
Kwanza weka akilini kuwa Kiumbe hatari hujijua kuwa yeye ni hatari, tena hujijua yeye ni mbaya asiyehitaji mchezo.

Nyoka, Nge, Tandu, buibui wang'atao ni miongoni mwa wadudu hatari kubwa, hawa hupenda kukaa mafichoni.
Na hata akiingia ndani ya nyumba yako hawezi pita sehemu wazi inayoonekana, lazima atembee na laini ya ukuta chini ili akitembea usimuone.

Viumbe hatari na Wabaya hupendelea giza katika harakati zao. Kwao nuru ni adui mkubwa.

Ukienda Mbugani ni ngumu Sana kuwaona Wanyama hatari, kama vile Chui, Simba, chatu, Koboko, Cobra, n.k.

Saikolojia ya viumbe hatari ni kutokuwa na Imani na yeyote. Muda wote wako machomacho, kujihami, n.k. pia viumbe hatari hupendelea Ambush, naam ndio shambulizi la kushtukiza.

Katika Maisha wapo watu hatari, na watu hatari siku zote wanatabia hizohizo.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umeandika kitalaam sana
 
Kiumbe hatari ni binadamu tu ieleweke hivyo na wala hajifichi ndio maana anaogopwa na viumbe vyote
Sio kweli mbona wale dada poa ambao ni binadamu tena warembo wanajificha usiku tena gizani lakini hawaogopwi.Wengi .. wakiwa na magonjwa hatari lakini wanaume vicheche wanakimbilia huduma zao.
 
Dah nachelea kusema hujaelewa na umejibu tu anyway nyoka simba chui kila mmoja hawezi kuogopa jamii yake ila ataogopa jamii nyingine
 
Viumbe hatari kumbe hawajijui kuwa wao ni hatari?
Kwamaana hiyo hata Simba au Black Mamba hawajijui kuwa wao ni miongoni mwa "watu wabad"?
 
KUMBUKA; VIUMBE HATARI HUPENDA KUJIFICHA.

Anaandika, Robert Heriel.

Moja ya sifa kuu ya kiumbe hatari ni kupendelea kujificha, kukaa mafichoni, kukaa chobingo.
Hawapendi kujianika Anika hovyo, kujidhihirisha hovyo.
Kwanza weka akilini kuwa Kiumbe hatari hujijua kuwa yeye ni hatari, tena hujijua yeye ni mbaya asiyehitaji mchezo.

Nyoka, Nge, Tandu, buibui wang'atao ni miongoni mwa wadudu hatari kubwa, hawa hupenda kukaa mafichoni.
Na hata akiingia ndani ya nyumba yako hawezi pita sehemu wazi inayoonekana, lazima atembee na laini ya ukuta chini ili akitembea usimuone.

Viumbe hatari na Wabaya hupendelea giza katika harakati zao. Kwao nuru ni adui mkubwa.

Ukienda Mbugani ni ngumu Sana kuwaona Wanyama hatari, kama vile Chui, Simba, chatu, Koboko, Cobra, n.k.

Saikolojia ya viumbe hatari ni kutokuwa na Imani na yeyote. Muda wote wako machomacho, kujihami, n.k. pia viumbe hatari hupendelea Ambush, naam ndio shambulizi la kushtukiza.

Katika Maisha wapo watu hatari, na watu hatari siku zote wanatabia hizohizo.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mwanadamu ndiyo kitu hatari mwenye mamlaka juu ya viumbe vyote,na viumbe vyote hai humtii mwanadamu
 
Back
Top Bottom