Kumbuka; Viumbe hatari hupenda kujificha

Robert Heriel

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
11,671
25,945
KUMBUKA; VIUMBE HATARI HUPENDA KUJIFICHA.

Anaandika, Robert Heriel.

Moja ya sifa kuu ya kiumbe hatari ni kupendelea kujificha, kukaa mafichoni, kukaa chobingo.
Hawapendi kujianika Anika hovyo, kujidhihirisha hovyo.
Kwanza weka akilini kuwa Kiumbe hatari hujijua kuwa yeye ni hatari, tena hujijua yeye ni mbaya asiyehitaji mchezo.

Nyoka, Nge, Tandu, buibui wang'atao ni miongoni mwa wadudu hatari kubwa, hawa hupenda kukaa mafichoni.
Na hata akiingia ndani ya nyumba yako hawezi pita sehemu wazi inayoonekana, lazima atembee na laini ya ukuta chini ili akitembea usimuone.

Viumbe hatari na Wabaya hupendelea giza katika harakati zao. Kwao nuru ni adui mkubwa.

Ukienda Mbugani ni ngumu Sana kuwaona Wanyama hatari, kama vile Chui, Simba, chatu, Koboko, Cobra, n.k.

Saikolojia ya viumbe hatari ni kutokuwa na Imani na yeyote. Muda wote wako machomacho, kujihami, n.k. pia viumbe hatari hupendelea Ambush, naam ndio shambulizi la kushtukiza.

Katika Maisha wapo watu hatari, na watu hatari siku zote wanatabia hizohizo.

Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,180
3,506
Kiumbe hatari ni binadamu tu ieleweke hivyo na wala hajifichi ndio maana anaogopwa na viumbe vyote
binadamu kajificha ndio maana kajitenga na wanyama wengine,kaacha pori kaja mjini..tena kajenga na nyumba anajificha humo wakati wa kulala na kuishi,anajificha ndani ya gari safarini na anajihami sana kwa kuwa mbunifu.
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
23,791
25,235
Ni kweli hata wale watu tusio wajua ni hatari sana hata kazi wanafanya usiku
 

pilato93

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
6,022
5,910
Aliyekuambia Mwanadamu hajifichi ni Nani?😂😂

Siku ukianza kuwa mtu hatari na kufanya mambo ya hatari utaelewa mada hii inazungumzia kitu gani.
Hivihivi huwezi elewa.
Watu hatari hawajifichi wanakifivha ni wasumbufu tu elewa hili
 

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
5,280
11,691
Kiumbe hatari ni binadamu tu ieleweke hivyo na wala hajifichi ndio maana anaogopwa na viumbe vyote

Muuza magendo, jambazi, muuza madawa ya kulevya, muuza silaha hatari, mbakaji wote hao hujificha kamwe hawajianiki na huezi kukuta kajianika sahau,
 

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
17,269
29,176
Limebarikiwa tumbo lililokuzaa ndugu muandishi.....hakika kazi za mikono yako kupitia kalamu vinakamilisha dhumuni la uwepo wako hapa duniani.....

Uandishi wako
Mpangilio wa uandishi wako na ujumbe uliopo kwenye maandishi vinanifanya nikiri kwa nafsi na kinywa kupitia mikono yangu kuwa wewe ni nguli wa fasihi..... barikiwa sana.....
 

Similar Discussions

27 Reactions
Reply
Top Bottom