Dar: Polisi wataja namba za dharura kipindi cha Sikuu ya Eid Al Adha

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Dar es Salaam 19, Julai, 2021

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM KUIMARISHA USALAMA SIKUKUU YA EID AL ADHA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limejipanga kikamilifu kuimarisha usalama katika kipindi cha sikukuu ya Eid Al Adha inayaotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21/07/2021.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawaasa wananchi kusherehekea sikukuu ya Eid Al Adha kwa amani na utulivu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kuimarisha doria maeneo yote muhimu zikiwemo nyumba za ibada, fukwe za bahari na kumbi za starehe na maeneo mengine yote yatakayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu ili kuhakikisha Wananchi wote wanasherekea sikukuu hii kwa amani na utulivu.

Pia wazazi wahakikishe watoto wao hawatembei peke yao bila ya kuwa na ungalizi wakaribu na kutowaruhusu kuogelea peke yao ili wasizame na kupoteza maisha.

Wamiliki wa kumbi za starehe wanatakiwa kufuata sheria ,kanuni na taratibu za uendeshaji wa kumbi hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limepiga marufuku Disko toto katika kumbi zote za starehe za hapa Jijini Dar es Salaam.

Vilevile, Madereva wa vyombo vya moto waendelee kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha magari au pikipiki wakiwa wametumia pombe/vilezi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawaomba wakaazi wote wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa namba zifuatazo 0735009983-ZPC, 0658111100-ZCO, 0715009976-RPC KINONDONI, 0735009980-RPC ILALA na 0736009979-RPC TEMEKE.
MULIRO J.MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM
 
Back
Top Bottom