We real miss you Mzee Ruksa

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,508
37,404
Huyu baba wa watu siku anaondoka alisema mtanikumbuka na kweli mwaka mmoja tangu atoke madarakani watu walianza kumkumbuka.

Pamoja na iflation wanayoiongelea ila enzi za mzee ruksa tumekula sana bata,mi nakumbuka hizi na wewe utamalizia

1. Majumba ya cinema yote yalikuwa yanajaa weekend hapa namaanisha ,cameo,drive in,new chox,empire,empress,star light,odeon.(theatres nyingi zimebadilishwa matumizi )siku hizi demu akikwambia umpeleke movie mlimani city unaanza kuwa na kigugumizi,masista duu wa siku hizi wanadhani kwenda movie ni kitu kipya.

2. Mwanamuziki CHAKACHAKA toka SouthAfrika alivyokuja kulikuwa na show pale Makondeko nakumbuka kiingilio laki moja na ukumbi ulijaa, nani anaikumbuka hii?

Sasa Diamond kufanya show ya elfu 50,000 Mlimani City mnasema kavunja rekodi jamani jamani.

3. Mishahara ilikuwa inakutana na kupeana mikono siku hizi mshahara unakata tarehe 5,kifuatacho madeni,mshahara mwingine ukija unalipa madeni ya mwezi uliopita.

Endeleeeni kutukumbusha, unakumbuka nini enzi za ruksa
?
 
l29496423672_9691.jpg

jamani kama hukuwa beatiful au handsome ukiwa kijana basi tena
 
Mkuu umesema kweli, nakumbuka kila jmosi na jpili, dingi alikuwa anatupeleka sehemu za bata balaa, cku hzi naziangalia tu kwa macho.
 
Mkuu umesema kweli, nakumbuka kila jmosi na jpili, dingi alikuwa anatupeleka sehemu za bata balaa, cku hzi naziangalia tu kwa macho.
leo hii vijana wa umri ule wengi wanapanga sinza tu hawana hata nyumba zaidi ya vigari
 
aluhudhuria show ya kanda bongo mana uwanja wa taifa...wakati huo manesi muhimbili walikuwa wamegoma..."akatamka"...nasubiri isambe ipigwa....teh teh ilikuwa rahaaa,na bia za stella artois
 
nakumbuka mdingi tulipokuwa tukitoka kwenda mahali tulikuwa tukitumia tax.Sidhan kama familia za sasa hivi zinaweza kumudu gharama hizi zaidi ya bajaji.
 
Dah kipindi kile utoto tulikuwa tunaokota sana hela.
sie tulikuwa tunalilia kufua nguo za mshua unajua hukosi kitu kwenye mifuko siku hizi sijui kama watu wanasahau hela kwenye mifuko
 
nakumbuka niliwahi kuokota sh mia nyekundu hivi kubwa kama gazeti ilikuwa kama sherehe home
Tutamkumbuka sana,huyu ndiye aliyetufanya tukajuwa TV,video,gari recondition toka Dubai na Japan,nguo toka nje,furniture toka nje,vifaa vya ujenzi toka nje,tiles,masinki ya jiko,choo,na vyitu vingi vya kisasa.
 
Na aliyakaribsha makapuni ya nje,kuanzia ya mawasiliano,simu,redio Tv ,spares,machine za aina mbali mbali,vifaa vya umeme na ujenzi,vyombo vya habari.
 
Tutamkumbuka sana,huyu ndiye aliyetufanya tukajuwa TV,video,gari recondition toka Dubai na Japan,nguo toka nje,furniture toka nje,vifaa vya ujenzi toka nje,tiles,masinki ya jiko,choo,na vyitu vingi vya kisasa.
enzi za mwalimu tulikuwa washamba balaa ,kombe la dunia likiisha mnasubiri miezi minne kuja kuangalia mikanda kwa wateule wachache wenye video du
 
enzi za mwalimu tulikuwa washamba balaa ,kombe la dunia likiisha mnasubiri miezi minne kuja kuangalia mikanda kwa wateule wachache wenye video du
Sana,mwinyi katutoa ushamba,ilikuwa tukienda Kenya au Zanzibar ndio twaona TV,na vitu vingine vya kisasa.
 
Kipindi kabla yake Mzee Ruksa, airport ya Dar wamajuu tukifika tunaweka karibu sabuni na dawa ya meno unapitishwa kama mfalme.
 
Back
Top Bottom