Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,165
- 1,361
Nimeona uzi hapa JF ukisifia Jumba la Senema la Empire la siku hizo, nikaona nikumbushie (na kuwajuza uzao wa dot.com) majumba ya senema yaliyokuwepo Dar enzi hizo.
Miaka ya 70 kulikuwepo na majumba sita ya senema jijini Dar. Bila kufuatilia mpangilio wa umaarufu au kigezo kingine cho chote, nayataja majumba hayo kama ifuatavyo:-
1. Empire: Hili lilikuwa mtaa wa Azikiwe mkabala na Posta Mpya.
2. Empress: Hili lilikuwa Mtaa wa Samora maeneo ya Askari Monument, likiangaliana na tawi la benki la Bank House.
3. Avalon: Hili lilikuwa Mtaa wa Zanaki, jirani na Halmashauri ya Jiji. Jumba hili lilidumu muda mrefu kushinda yote, hadi mwaka 2000.
4. New Chox: Hili lilikuwa Mtaa wa Nkrumah likitazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja, jirani na Chinese Restaurant ambayo ilikuwa ikijulikana sana kwa 'fried rice'.
5. Cameo: Hili lilikuwa Kisutu, Mtaa wa Jamhuri, karibu na Tawi la Posta La Kisutu. Hili lilijikita katika kuonyesha senema za Kihindi. Pamoja na hayo, Waswahili walikuwa wakifurika kuangalia senema hizo.
6. Drive-In: Hili lilikuwa palipo Ubalozi wa Marekani hivi sasa. Halikuwa jumba bali uwanja wa wazi, unaingia na gari lako na unaangalia senema ukiwa kwenye gari.
Majumba hayo yalikuwa yakionyesha senema tofauti mara mbili kwa siku. Senema ya "The Ten Commandments" mwaka 1975 (or was it 1976?) ndiyo ilikuwa ya kwanza na ya mwisho kwa majumba yote sita (pamoja na Cameo) kuonyesha senema hiyo hiyo mara zote mbili kwa wiki nzima na bado watu walikuwa 'wakipigana' kuingia. Huo ni ushahidi tosha wa jinsi senema hiyo ilivyopendwa.