Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,707
- 1,729
Mpaka miaka ya kama themanini hivi nchi hii palikuwa na majumba ya kuonesha sinema kama Avalon, New Chox, Empire, Empress, Drive In n.k. kwa Dar es Salaam na mikoani pia palikuwapo majumba hayo kwa majina tofauti kama Diamond Talkies la Tabora n.k. Kilivokuja kimbunga cha CD na DVD basi utaratibu mzuri wa kuangalia sinema hasa ukiwa na familia ukaisha. Wenzetu Ulaya nasikia bado yapo. Majumba hayo (nasikia) yalikuwa yanamilikiwa na Tanzania Film Company (TFM), sijui kama ipo hivi sasa na palikuwa na burudani kwelikwli hasa mwisho wa juma. Jamani si wote wanapenda kuangalia sinema za CD na DVD nyumbani, wito wangu kampuni hii iturejeshee burudani hiyo kwenye majumba hayo kwani mengi bado yangalipo.