Kumbe 'wazungu' wanakithamini kiswahili kiasi hiki..

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,284
1,195
Wakati watanzania na serikali yake tukiidharau na kuchukulia poa lugha yetu adhimu ya kiswahili, wenzetu wa mataifa ya nje wanaithamini sana na kujifunza kwa kasi.

Leo kupitia habari kwenye TV nimemsikia mkurugenzi wa benki ya maendeleo ya Ujerumani akisoma na kuzungumza kiswahili vizuri kabisa..

My take: Ndugu zangu tuache kiswa-kinge, tuipende lugha yetu!
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
9,309
2,000
Mzungu hatakuja penda kitu cha kibantu toka moyoni, isipokuwa kama ana maslahi nacho tena si maslahi ya kitoto!
 

mpendwa789

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
226
250
Kumbe, Twilumba, mimi napenda lugha ya Kiswahili sana tena sana! Binafsi nafikiri kwamba ni lugha bora! Ni nani anayeweza kudharau lugha ya Kiswahili? Hamna mmoja! Au kusema ni lugha duni? Hamna hata mmoja! Hayupo – isipokuwa anakosa sana. Miaka kadhaa iliyopita nilinunua vitabu vya shule ‘Tujifunze Lugha Yetu'. Vilinisaidia saaana kujifunza Kiswahili. Nilisoma kama mtoto. Nilijifunza kama mtoto – nilifurahia sana kufanya hivyo. Sasa je, naweza kukuvuta ukubali nami ya kwamba ……..inawezekana…….. labda …… yupo mzungu mmoja duniani anayependa lugha ya Kiswahili toka moyoni mwake bila kutafuta faida yake yenyewe??? Unafikirije?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom