Mimi nilipoona kichwa cha habari nilienda mbali zaidi. Nilikumbuka hadithi kuwa kuna baadhi ya "mashoga / ma anti", katika wiki ya mwisho ya mwezi hula mapapai mengi wakawa "wanaendesha kama ngisi" na kudai wako katika siku zao. (lol)!
Lakini baada ya kusoma nimefahamu umekusudia nini, ila hilo la kuita mihemuko, hisia kubwa, jazba (emotions) kwa wanaume kuwa ni hedhi nahisi umeenda mbali kidogo. Tayari pameshatolewa maana ya hedhi (mensturation), ambapo vile vile hisia kubwa za mhusika huonekana wakati huu, lakini ni matukio mawili tofauti.
Ama kuhusu mwanamume kuwa na siku za mihemuko kunaweza kuwa na sababu nyingi, furaha, huzuni, hasira, kicheko, tafrani...kutokana na matukio au hali zinazomkuta wakati fulani.
Lakini kwa kuungana nawe kidogo kuhusu mihemko ya wanaume, inawezekana pia kusababishwa (bado kuthibitisha kwa upande wangu) na mzunguko wa mwezi ambao una athari nyingi sana kwa binadamu, wanyama na mazingira kwa jumla.
Ningependa kujua Mkuu, ikiwa mwanamke akiwa katika hedhi siku hizi hawezi kupata ujauzito, jee ikitokea kuwa mwanamume yuko katika "hedhi" siku hizi asitumie kondom kwani mbegu zake haziwezi kusababisha ujauzito?