Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

No way. I'm not buying into this. Mnataka watu wakishaamini huu utumbo wenu, muwaambie ndo maana hawapaswi kuukataa ushoga..!! Mshindwe na mkome... Waone kwanza
 
Huu ni upuuzi. Kama ni kweli basi mke na mume kuzaa lazima wote wakutane wakiwa katika hedhi na ingekuwa hivyo famile chache zingepata kuzaa. Ongea na daktari wako kwa ufafanuzi zaidi. Huyu ana hiden agenda ambayo ni mbaya.
 
Kama ni hivyo basi kuna wananume wengine tuna hedhi kila siku. Manaake kwa siku kuna saa unakuwa na hasira na unatamani kumpiga mtu, unasikitika, unafurahi na na wakati mwingine unapenda kufanya ule mchezo wa kikubwa hasa akipita jirani na wewe kiumbe wa jinsia tofauti mwenye mvuto na yale mambo mengine tunayopenda kuyatathmini kwa macho.
 
Aaaah! Mi nimenusurika bhana, hasira ninakuwa nazo pale tu ninapokuwa empty mfukoni au kazi zinapokuwa nyingi sana (Over working) Labda wewe umeshindwa kugundua kuwa kuna siku tatu nne unakosa mshiko kila mwezi. Mwisho napinga kuwa wanaume wanaingia kwenye hedhi na kama wanaingia SIO MIMI, Hao hao!

Mimi huu mgao wa umeme siku chache zilizopita ulikuwa unanipa hasira na masikitiko kila siku kwani siku ilikuwa haiishi bila umeme kukatika. Sasa hiyo nayo sijui inaingia katika "definition" ya hedhi kama alivyoitoa mwanzishaji wa mada hapo juu?
 
Sasa wanawake wana uwezo wa kuamua kupata hedhi au la, baada ugunduzi wa vidonge ambavyo humfanya mwanamke asizione siku zake kabisa.

Vidonge hivyo ambavyo vimefanyiwa majaribio kwa muda mrefu vimebainika kuwa na uwezo katika suala hilo. Kati ya wanawake waliotumia vidonge hivyo, asilimia 60 hawakuona kabisa damu kwenye siku zao, wakati asilimia 20 waliona vidoa tu.

Hii ina maana kwamba, kati ya kila wanawake kumi wanaotumia vidonge hivi, wanawake wanane wanafanikiwa kutoziona siku zao.

Vidonge hivyo vinavyofahamika kwa jina la Lybrel, ni vya kwanza duniani, ambavyo vimemudu kuondoa kabisa damu ya hedhi kwa mwanamke. Kampuni ya Wyeth Pharmaceuticals, ambayo ndiyo iliyofadhili utafiti huo, inasema vidonge hivyo ambavyo vitauzwa kwa bei rahisi na ambavyo hutumiwa kwa dozi ndogo havina madhara kwa watumiaji.

Lakini hata hivyo naomba ieleweke kwamba kauli hiyo ni ya kutarajiwa sana kutoka kwa mtengenezaji wa bidhaa yoyote, iliyo au isiyo na madhara.

Lakini, wataaalamu wa masuala ya wanawake, wanasema mwanamke kuziona siku zake siyo lazima, yaani anaweza kuacha kuziona na hilo lisimletee madhara yoyote, labda tu kama ameacha kwa kuuugua.

Mpaka sasa haijafahamika kama vidonge hivi vimeshaingia nchini, lakini naamini taarifa hii itapokelewa kwa furaha na si kwa wanawake tu, bali pia na wanaume ambao swala la hedhi kwa wake au wapenzi wao limekuwa kero.

Mnaweza Kubofya hapa kwa habari zaidi: http://contraception.about.com/od/prescriptionoptions/a/Lybrel.htm
 
Wewe unataka kutuharibia sasa! Wameshasema hazina MADHARA bana!

sijaelewa nani kasema? Au hao waliofanya reseach? Lakini mtambuzi ukubali ukatae vitakuwa na long term effects mungu akiumbacho hakosei bhana....upande mwingine wanaume watakuwa na furaha kweli
 
Hivyo vitakuwa na madhara asee, hiyo hedhi itakuwa inapotelea wapi? Yaan atakaetumia atajuta manake kuna siku atapata hedhi ya miezi yote aliyoizuia isitoke..
 
hamtaishia hapa...................mwisho mtakuja na je mbegu za uzazi zitoke na nguvu ya kumimbisha au la? Mungu hakuwa mjinga kutuwekea hiyo kitu nyie!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
mmh! hii ni njia ya kutongezea kansa ya vizazi kwa sisi wanawake, hizi dawa lazima zinamadhara makubwa sana sikatai hedhi huwa inakera ila kwa hili siliafiki kabisa labda waseme hizi ni dawa kwa wanawake ambao hawazai tena maana kwa mwanamke anayataka kuzaa atajuaje kuwa huu ni muda wa yeye kuweza kubeba mimba???
 
Hivyo vitakuwa na madhara asee, hiyo hedhi itakuwa inapotelea wapi? Yaan atakaetumia atajuta manake kuna siku atapata hedhi ya miezi yote aliyoizuia isitoke..

Wewe sema tu unataka kutuharibia............... hebu soma hiyo link utaelewa wlichosema wataalamu
 
Back
Top Bottom