Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtambuzi, Aug 1, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni machache sana ukilinganisha na yale tusioyafahamu.

  Kiasi cha miezi kadhaa iliyopita nilisoma utafiti fulani kuhusu hedhi. Awali nilipousoma niliona ni hadithi tupu. Lakini nilipoona ni vyema kuujaribu kwa kutenda miezi minne baadae nilishangaa. Hata wewe najua utashangaa utakaposoma makala haya. Lakini ombi langu kwako ni kukutaka ujaribu kufanya mazoezi ili uthibitishe ukweli huo.

  Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

  Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.

  Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.

  Ni jambo ambalo lipo na limeshafanyiwa tafiti mbalimbali, hata mimi binafsi nimefanya zoezi hilo kwa miezi minne na limetoa majibu kama hayo. Kwa kawaida mwanaume hana dalili za kimwili za kutoka damu kama mwanamke – ndio maana, karne na karne hakuna mtu aliyejali – lakini ni jambo la uhakika kwamba wanaume wanapata hedhi.

  Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.

  Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi. Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.

  Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa ‘matofali’ yaleyale, kwa maumbile yaleyale na baiolojia ileile. Tofauti yao ni kwamba mwanaume ni chanya na mwanamke ni hasi kama tungekuwa tunazungumzia umeme. Huwezi kupata umeme kwa kuwa na chanya mbili; wala ukitumia hasi mbili bali ukichanganya chanya na hisi. Hivyo, kama mwanamke anapata hedhi kama hatua muhimu kuelekea mwito wa kimaumbile, haiwezekani mwanaume asipitie hatua hiyo, ingawa kwa uchanya wake.

  Kupata hedhi kwa mwanamke inaeleweka kwamba, ni kutokana na wito wa kimwili. Maana yake ni kwamba, alikuwa amefikia hatua ambapo kimaumbile alitakiwa kujamiiana ili apate ujauzito. Je, kama hakuna mabadiliko kwa mwanaume, itawezekana vipi mwanaume kujamiiana na mkewe ambaye yuko kwenye hitaji hili la kimaumbile?

  Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi. Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Duh,hebu ngoja ntaanza kuji-monior kuanzia mwezi huu maana mimi nilikua nadhani iko-affiliated na kuishiwa au matatizo madogo madogo ya kifamilia....hii kali bhana, lakini afadhali hatununui mataulo maana nilivyomgumu wa kutoa pesa, ningemwibia Shemeji yenu tu..........
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Elli nimesoma nikaishiwa cha kusema maana duh ngoja nikajifanyie research maana ahhh ngumu kumesa
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Duh..........umenigusa mno

  wiki iliyopita kuna siku kama nne mfululizo nilikuwa so down
  na nilikuwa sitaki hata kupokea simu ya mtu for no good reason..

  Yaani nilikuwa sina interest na chochote
  ni kula kulala,tv na internet

  hata kuzungumza niliona uvivu

  kwa kuwa nilikuwa nina matibabu ya malaria nili connect na tiba hiyo
  but nilikuwa najiuliza mbona huwa hainitokei hivyo mara zote ninapougua malaria???

  Could it be..............?????????????????
   
 5. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tafuta neno jingine.
  Lakini usiite hedhi.
  Hedhi ni yenu kutoka damu, lakini kama damu hakuna, huwezi kuita hiyo ni hedhi.
   
 6. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Aaaah! Mi nimenusurika bhana, hasira ninakuwa nazo pale tu ninapokuwa empty mfukoni au kazi zinapokuwa nyingi sana (Over working) Labda wewe umeshindwa kugundua kuwa kuna siku tatu nne unakosa mshiko kila mwezi. Mwisho napinga kuwa wanaume wanaingia kwenye hedhi na kama wanaingia SIO MIMI, Hao hao!
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hata ulikataa kutoka na mimi wikiend kumbeeeeeeeeee
   
 8. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Malaria yalipanda kichwani bana sio hedhi EBO! tena kuwa mwangalifu malaria za namna hiyo zikija unaweza kuvunja hata hiyo kompyuta yako!
   
 9. JS

  JS JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />

  .......yes Boss you were going through some some last week..hehehehehe lmao!!!
   
 10. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  kweli mimi huwa na hizo dalili kila baada ya tarehe 28 katika mwezi, hii inakwenda mpaka tarehe 30, nakuwa na hasira siku za mwazo siku ya pili huwa na fura na mchangamfu, nikafanya utafiti na kugudua inatokea kila mshahara unapochelewa na kuwa na hasira na ukishatoka huwa na furaha. kwahiyo inawezekana nakuwa na hedhi ya mshahara ee?
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ungetuwekea huo utafiti tukasoma wenyewe. Hata hivyo mwanume hawezi kuwa na hedhi, kwa sababu hedhi inahusiana na masuala ya uzazi (reproductive system), na ndiyo maana inaitwa "menstrual cycle" kwa mwanamke; na inahusiana na yai "ovary" kutokurutubishwa kwa ajili ya kutunga mimba, ndo maana baada ya muda wake hutoka kwa njia hiyo ya hedhi.

  Kwa kuwa mwanaume hana utaratibu huo hedhi, iyo hali unayoisema hata kama kweli inatokea kwa wanaume bado huwezi na haiwezi kuitwa "hedhi". Labda itaitwa kwa jina lingine. Zaidi sana itakuwa ni Psychological, labda kwa kuwa hasa walio kwenye ndoa hawezi kushiriki na mkewe katika siku ambazo mke yuko katika hedhi.

  Ni maoni yangu tu, ila ukituwekea hapa bandiko la huo utafiti kutoka kwenye journal husika itakuwa bora zaidi ili tujue hasa kisayansi ni kitu gani kinatokea.
   
 12. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,175
  Likes Received: 8,201
  Trophy Points: 280
  :):):):heh:
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Dah....nilivyosoma heading tu, swali la kwanza lilikuwa 'damu itatokea wapi'?......kumbe ni emotions zaidi.
   
 14. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  TB nafikiri ni malaria tuu ilisumbua na hakuna uhusiano wowote na hiyo kitu
  Hiyo kitu kwa wanaume hakuna bana
   
 15. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  ulikuwa kwenye hedhi.
   
 16. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Male menstruation inahistoria ndefu tangu enzi. Watu kwa haraka haraka waweza sema kuwa: Ni ugonjwa utokeao hasahasa ktk nchi za kitropic na huletwa na vijidudu -parasites waitwao (Schistosoma haematobium) na huathiri njia ya mkojo (urinary tract) au matumbo (intestines) na husababisha ugonjwa uitwao kitaalam (schistosomiasis) ambapo siku za nyuma ulikuwa ukiitwa (bilharziasis). Kwa hiyo siyo wanaume wote huwa katika hali hiyo (see also » The mystery of the menstruating men - Blogger News Network). Hili ni sawa na ndivyo ilivyo. Lakini kwa utamu zaidi waweza fuatilia historia ya male menstruation ilivyo kuwa tangu enzi za nyuma hata kama mtu hana ugonjwa wa (schistosomiasis).

  kwa kubofya hapa:
  Project MUSE - Bulletin of the History of Medicine - Jewish Male Menstruation in Seventeenth-Century Spain.

  Natumai wana jf mtafurahia historia hiyo ya kujuwa male menstruation huko nyuma ilikuwa namna gani.
   
 17. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Ok sasa tufafanulie, yai la uzazi la mwanamke linapokuwa limepevuka, baada ya siku kadhaa lisiporutubishwa pamoja na kuta za mji wa mimba ambazo zilikuwa teyari kwaajili ya kubeba mtoto, zinaporomoka kisha wanamke hutoka damu ndo tunaita hedhi, huu ni mfumo uliopo kwa mwanamke kwa ajili ya uzazi, sasa je kwa mwanaume, sasa hilo yai linabomokea kichwani ndo maana tunakuwa na hasira?

  utafiti wako unaweza ukawa na ukweli lakini huwezi kuita kuwa hiyo ni hedhi, kisha si kweli kuwa inatokea kila mwezi ukawa na aina ya matatizo inayofanana katika kipindi kinachofanana, labda itokee coincidence na sikila wakati.
  Sababu ya kuwa we are made from the some stones that can not be the reason tukafana kila kitu, if that is true kwanini wanaume hawabebi mimba?

  Sio kila mtazamo wa kisayansi ukawa 100% true, unless proven true
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri anachosema hapa ni kuwa hata wanaume tuna mzunguko
  fulani wa ndani ya siku 28 ambazo kati yake hizo siku
  kuna siku unapa mchoko fulani hivi usiokuwa na sababu maalumu
  isipokuwa unafanana na ule wa wanawake wanapopata hedhi.......
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Bora umesema!!

  Kweli

  Kweli aiseee....
  Trigger ni kukosa uchache mfukoni..ikimaanisha 'imbalance" ya mfuko huathiri balance ya akilini mwako lol

   
 20. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Nimegoogle na hii ni mojawapo ya majibu:

  "It seems that men may have cycles, as do most living things. However, men's cycles are more subtle and less disruptive. I found no
  substantial research that proves men have cycles,especially for 4 days, but I found quite a bit of theoretical and anecdotal information that some men do indeed have 'cycles'. The jury is still out!"

  unaweza kuendelea kusoma hapa:Google Answers: Male Period?
   
Loading...