Kumbe Uchina si chochote katika maswala ya Computer, ukubwa wa Bure!

Kumbe Uchina si chochote katika maswala ya Computer, ukubwa wa Bure!

Hata mkeo/mumeo pamoja na uzuri na sifa utakazompa lakini hakosi kasoro
 
Wachina kwenye teknolojia za sasa ni wazuri kwa kuchukua kitu kilichopo, kuki reverse engineer na kutoa chao.

Mwaka huu, hata hiyo Reverse Engineering yao "imechemka" kwa DRM iliyotumiwa na EA Sports kwenye FIFA 15.
 
Mleta mada inabidi ujifunze kwanza kuelewa kwamba hakuna nchi inayozalisha kila kitu
 
Mleta mada inabidi ujifunze kwanza kuelewa kwamba hakuna nchi inayozalisha kila kitu

Yes Bulldog, Hata kampuni ya Apple Inc. iliyopo Marekani inapotengeneza bidhaa zake zikiwemo Iphone inatumia baadhi ya components za kutoka nchi nyingine kama South Korea...na hii haimaanishi kwamba wako nyuma ki technology bali kuna factors nyingi zinazingatiwa kwa kufanya hivyo.." kwa nini ununue ng'ombe wakati jirani anauza maziwa bei chee ?"
 
Una hoja lakini ulinganifu wako si yakinifu. Uhusiano wa idadi ya watu na ujuzi wa kitelnolojia? ! Teknolojia ni zao la kuwekeza kwenye elimu na tafiti. Lakini pia China kuwa nyuma kiteknolojia haiifanyi kutokuwa na maendeleo. Labda jaribu kupita kwenye majarida ya uchumi utagundua hilo.
 
Unashangaa UCHINA baada ya kushangaa TANZANIA yenye watu zaidi ya milioni 48 inaagiza hadi chupi nje ya nchi......
 
Sijaongelea ukubwa wa Eneo kumbuka bali Idadi ya Watu, Uchina ina watu zaidi bilioni 1.3 wakati Urusi ina watu Milioni 140 tu, hivyo kutokujitosheleza kwa Urusi ktk nyanja fulani kunaweza kueleweka halafu isitoshe sio kwamba Urusi hawawezi kutengeza Meli za kivita!

Ila uchina kama wanashindwa mpaka leo pmj na kuwa na watu wote hao yaani bilioni moja 1.3 wanashindwa kutengeneza tu hata transistor hapo kuna tatizo!
Kumbuka Uchina Mainjinia milioni kumi humaliza Chuo kila mwaka karibu nusu ya Wakazi wote wa Taiwani lkn Taiwani wana Makampuni yao wenyewe kweye hizo key industries zote!
Tanganyika pekee ina watu zaidi ya milioni 40 hatuwezi kutengeneza hata cassete ya redio au CD, achilia mbali memory card au flush disc,
idadi ya watu sio hoja, hoja ni shule mkuu, hata huko wanakotengeneza hizo chip hawatengenezi kwa vile ni wengi, bali kwa vile wamewekeza kwenye shule zaidi.
 
mfano kuna baadhi ya smart phone zinakuwa designed Ujerumani , zinatengenezwa marekani na zinakuwa assembled china, manake wewe mnunuzi wa cm ujue pesa yako imegawanyika kwenda nchi 3
 
Ni vizuri kufikiria jinsi unavyoweza kutoa changamoto kwa waafrica kujinasua kwenye utegemezi wa vitu vingi ambavyo viko kwenye uwezo wetu kuliko kushabikia mwenzio ambaye tayari kakuacha mile nyingi mno katika kila nyanja.
 
Mwanzisha uzi una chuki binafsi na wachina la sivyo huna taarifa za kutosha. Uliyoyasema hayana usahihi kikamilifu.
Huawei kwa mfano imewekeza teknolojia yao marekani tena majuzi waliletewa shida baada ya Obama kuingilia kati uwekezaji wao maeneo jirani na kambi kubwa ya jeshi lao.

Kikubwa China si wavumbuzi sana. Hata hao Taiwan, Korea na nchi nyingi za Asia wananakili tu teknolojia za kimagharibi hasahasa Marekani. Samsung vs Apple, n.k. Falsafa yao ni kuwa huna haja "to re-invent the wheel". Na ndo walichofanya Asian Tigers ili watoke haraka.

Ulinganisho wako wa idadi ya watu na teknolojia hauna mantiki.
 
Tanzania kwa zaidi ya miaka 40 tunaongoza kwa tecknolojia ya wizi na ufisadi na kila kitu tunacho.
 
Kwanza mimi nashindwa kuitenganisha China na Taiwan, Hivi Taiwan wana permanent seat umoja wa mataifa?
 
Back
Top Bottom