Kumbe Uchina si chochote katika maswala ya Computer, ukubwa wa Bure!

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
10,777
Reaction score
18,686
Kumbe Nchi ya Uchina pamoja na kelele zoote kupigwa hapa Duniani sijui kwamba Ina uchumi Mkubwa, sijui ni World Power kumbe si lolote katika maswala ya computer, yaani kitu kikubwa lakini kisichokuwa na kitu ndani yake!

Nasema hivi kwa maana sasa hivi Uchina ndiyo inayoongoza kwa kujenga SuperComputer yaani ni computer ambayo ina uwezo mkubwa wa kukokotoa mahesabu kwa haraka kuliko nyingine yoyote ile Duniani, lakini kumbe mpaka sasa hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya bilioni 1.3 haiwezi kutengeza computer chips zake yenyewe, yaani processors zote ambazo imetumia kwenye SuperComputer yake wameagiza kutoka nje, wanashindwa na Nchi ndogo kama Taiwani (watu kama milioni 20 hivi) ama Korea Kusini ambao wanatengeza computer chips zao wenyewe!

Inasemekana itawachukua miaka mingi ili tu waweze kuwa na processors zao wenyewe kama nchi ndogo ya Taiwani ama Korea!

Onyo: Sijalingalisha Tanzania na Uchina!

​
 
Mkuu hakuna nchi inayojitosheleza kwa kila kitu ndio maana kuna biashara za kimataifa,Russia ananunua manuari kwa Mfaransa wakati Russia ni nchi kubwa kuliko zote duniani.
 
teh tehjishangae tz manakufa na njaa wakat rutuba imejaa tele Taiwan inawapa chakula wakati kanchi chenyewe kama kigamboni tu.
 
Mkuu hakuna nchi inayojitosheleza kwa kila kitu ndio maana kuna biashara za kimataifa,Russia ananunua manuari kwa Mfaransa wakati Russia ni nchi kubwa kuliko zote duniani.

Sijaongelea ukubwa wa Eneo kumbuka bali Idadi ya Watu, Uchina ina watu zaidi bilioni 1.3 wakati Urusi ina watu Milioni 140 tu, hivyo kutokujitosheleza kwa Urusi ktk nyanja fulani kunaweza kueleweka halafu isitoshe sio kwamba Urusi hawawezi kutengeza Meli za kivita!

Ila uchina kama wanashindwa mpaka leo pmj na kuwa na watu wote hao yaani bilioni moja 1.3 wanashindwa kutengeneza tu hata transistor hapo kuna tatizo!
Kumbuka Uchina Mainjinia milioni kumi humaliza Chuo kila mwaka karibu nusu ya Wakazi wote wa Taiwani lkn Taiwani wana Makampuni yao wenyewe kweye hizo key industries zote!
 
Hizo taarifa umezitoa wapi? Tukumbuke pia kuwa kila taarifa hutolewa kwa lengo fulani,bila kujali hiyo taarifa kama ni ya kweli ama ai ya kweli.
 
Computer chip zilizotengenezwa china na kuuziwa jeshi la marekani ina "backdoor" ambayo wachina wanaweza kuangalia chochote hata kama imefungwa na mmarekani, Wachina wako mbali sana
 
Kumbe Nchi ya Uchina pamoja na kelele zoote kupigwa hapa Duniani sijui kwamba Ina uchumi Mkubwa, sijui ni World Power kumbe si lolote katika maswala ya computer, yaani kitu kikubwa lakini kisichokuwa na kitu ndani yake!

Nasema hivi kwa maana sasa hivi Uchina ndiyo inayoongoza kwa kujenga SuperComputer yaani ni computer ambayo ina uwezo mkubwa wa kukokotoa mahesabu kwa haraka kuliko nyingine yoyote ile Duniani, lakini kumbe mpaka sasa hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya bilioni 1.3 haiwezi kutengeza computer chips zake yenyewe, yaani processors zote ambazo imetumia kwenye SuperComputer yake wameagiza kutoka nje, wanashindwa na Nchi ndogo kama Taiwani (watu kama milioni 20 hivi) ama Korea Kusini ambao wanatengeza computer chips zao wenyewe!

Inasemekana itawachukua miaka mingi ili tu waweze kuwa na processors zao wenyewe kama nchi ndogo ya Taiwani ama Korea!

Onyo: Sijalingalisha Tanzania na Uchina!

​

Usisahau kuwa Uchina inanunua maembe kutoka Tanzania!
 
Computer chip zilizotengenezwa china na kuuziwa jeshi la marekani ina "backdoor" ambayo wachina wanaweza kuangalia chochote hata kama imefungwa na mmarekani, Wachina wako mbali sana

Unamaanisha nini unaposema wapo mbali sana? Kwangu mimi wakonyuma sana, kwa maana nchi yenye watu bilioni 1.3 walipaswa watawale kila nyanja ya kiteknolojia ktk Dunia hii, lkn wapi hawawezi hata kutengeza Transistor yao wenyewe wanashindwa na Nchi ndogo kama Korea Kusini yenye watu milioni 50 wana global companies kama Samsung, Hyundai,Kia LG n.k nitajie Technology Company moja kubwa ya Uchina yenye kutengeza products zake yenyewe yenye global dominance!

Kumbuka kwammb Uchina wana watu zaidi ya Milioni 500 wanaoweza kuzalisha lkn hawna high tech Company hata moja, wakati Taiwani wana work force ya kama watu milioni 10 lkn wana global Companies za kuaminika tu...

Hivyo ukichukulia Ukubwa na uwingi wa Watu wa uchina yaani watu Bilioni Moja nukta3 basi ni kama Boya tu!

Tanzania imefanya nini kwenye Jumuia ya Afrika mashariki
 
Computer chip zilizotengenezwa china na kuuziwa jeshi la marekani ina "backdoor" ambayo wachina wanaweza kuangalia chochote hata kama imefungwa na mmarekani, Wachina wako mbali sana

hadi wewe mjinga mwenye low profile hata mtaani kwako umelijua hili sijui kwa nini wamarekani wasilijue kabla yako hili la backdoor. story za saigon unaleta kwa watu wenye akili nyingi.
 
Kumbe Nchi ya Uchina pamoja na kelele zoote kupigwa hapa Duniani sijui kwamba Ina uchumi Mkubwa, sijui ni World Power kumbe si lolote katika maswala ya computer, yaani kitu kikubwa lakini kisichokuwa na kitu ndani yake!

Nasema hivi kwa maana sasa hivi Uchina ndiyo inayoongoza kwa kujenga SuperComputer yaani ni computer ambayo ina uwezo mkubwa wa kukokotoa mahesabu kwa haraka kuliko nyingine yoyote ile Duniani, lakini kumbe mpaka sasa hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya bilioni 1.3 haiwezi kutengeza computer chips zake yenyewe, yaani processors zote ambazo imetumia kwenye SuperComputer yake wameagiza kutoka nje, wanashindwa na Nchi ndogo kama Taiwani (watu kama milioni 20 hivi) ama Korea Kusini ambao wanatengeza computer chips zao wenyewe!

Inasemekana itawachukua miaka mingi ili tu waweze kuwa na processors zao wenyewe kama nchi ndogo ya Taiwani ama Korea!

Onyo: Sijalingalisha Tanzania na Uchina!

​
KWELI?
pitia hii:

[h=3]China's 8-core Godson processor details to be shared at ...[/h]
 
Wakati mwingine unaposikia habari ambayo huna uhakika nayo, kabla ya kukimbilia JF kupost ni bora angalau ukapoteza dkk 5 google kuhakiki. China sio tu wanatengeneza computer chips, bali wanauza hata ktk jeshi la US..
 
Nafikiria kuna haja ya kuwapa ukweli kuwa china ni wajanja wa kimataifa walioshindikana kuthibitiwa.
Siku zote china haisemi kweli katika mambo yake yake ya kimaslahi kwa taifa na inatoa ripoti hafifu sana zisizo na ukweli wowote.

Kulinganisha idadi ya watu na fani ni kosa lako mwenyewe bado china imekuwa msiri wa kimataifa aliebobea katika kudanganya mataifa yote kuhusu ukweli wa taifa lake.

Mimi kuna rafikia yangu kasoma china alirudi na simu ndogo sana kama nokia N110i lakini kina mambo makubwa sana kuliko ipad
 
Wakati wa kufanya production kuna vitu vya kuangalia hasa concept ya absolute na comperative advantage inamaana kama product (let's say computer chip) kuitengeneza china ni dola 15 na kuitengenezea Taiwan ni dola 5(may be kutokana na availability ya materials Au technology) kwa ubora uleule. Kwa nini uingie gharama ya kutengeneza chip kwa gharamaa kubwa wakati inapatikana kwa urahisi hapo Taiwan!
 
Mkuu hakuna nchi inayojitosheleza kwa kila kitu ndio maana kuna biashara za kimataifa,Russia ananunua manuari kwa Mfaransa wakati Russia ni nchi kubwa kuliko zote duniani.

Dogo hajui absolute na comperative advantage! Ndo inatumika kwenye production! Ni ujinga kutumia gharama kubwa kutengeneza product wakati jiran anayo kwa bie rahisi amabyo unanunua na kuendelea na production!
 
Wachina kwenye teknolojia za sasa ni wazuri kwa kuchukua kitu kilichopo, kuki reverse engineer na kutoa chao. Hawana uvumbuzi kwa sana.

Juzi nilikuwa nasikiliza habari ya kwamba Wachina sasa wanataka kujikongoja kuingia kwenye kuvumbua.

Tatizo la kuvumbua kitu inabidi ku invest sana kwenye research and development. Wachina wako cheap sana na wanapenda shortcuts.
 
hadi wewe mjinga mwenye low profile hata mtaani kwako umelijua hili sijui kwa nini wamarekani wasilijue kabla yako hili la backdoor. story za saigon unaleta kwa watu wenye akili nyingi.

Mmarekani anunue computer chips from China kwa matumizi ya Jeshi lake. Amazing.
 
Unamaanisha nini unaposema wapo mbali sana? Kwangu mimi wakonyuma sana, kwa maana nchi yenye watu bilioni 1.3 walipaswa watawale kila nyanja ya kiteknolojia ktk Dunia hii, lkn wapi hawawezi hata kutengeza Transistor yao wenyewe wanashindwa na Nchi ndogo kama Korea Kusini yenye watu milioni 50 wana global companies kama Samsung, Hyundai,Kia LG n.k nitajie Technology Company moja kubwa ya Uchina yenye kutengeza products zake yenyewe yenye global dominance!

Kumbuka kwammb Uchina wana watu zaidi ya Milioni 500 wanaoweza kuzalisha lkn hawna high tech Company hata moja, wakati Taiwani wana work force ya kama watu milioni 10 lkn wana global Companies za kuaminika tu...

Hivyo ukichukulia Ukubwa na uwingi wa Watu wa uchina yaani watu Bilioni Moja nukta3 basi ni kama Boya tu!

Nakubaliana na wewe kuwa china inapofikia suala la core competence kwenye technology hamzidi mmarekani. Hii imechangiwa sana na emphasis yao ya kucopy technology badala ya kuumiza akili namna ya kuinvent (au hata kuinnovate). Lakini sikubaliani na hoja yako kuwa ukishakuwa na idadi kubwa ya watu basi unapaswa kuwa kinara kwenye technolojia. Kwangu mie competency kwenye technology is a function of Reasearch and Development. Hivyo, suala la muda (kwa maana ya experience ya wataalam) ni factor kuu. China imeanza jitihada za economic na technological revolution mwaka 1978 ( ni around miaka 35). Mmarekani ana zaidi ya miaka 125. Kwa namna yoyote huwezi kutegemea mchina amzidi mmarekani. Baba wa technolojia hapa ulimwenguni ni mmarekani. Hawa warusi sijui korea, Japan, Taiwan wamebobea sehemu ndogo tu katika specific areas za technolojia.
 
Yaani hilo tu ndio limekufanya uone China si lolote kwen maswala ya computers?

ANGALIZO:
Isije ikawa ni chuki binafsi.
 
Back
Top Bottom