Kumbe shule ya Feza Boys hamna kitu

kabingo

Senior Member
Oct 16, 2015
115
118
Kweli hawa wanafunzi huwa wanaibiwa yaani wanapewa majibu wakati wa mitihani leo nilikuwa naangalia kipindi cha sikonga kinachorushwa na EATV, katika maswali waliyooulizwa hakuna mwanafunzi aliyeweza kujibu, yaani mwanafunzi hajui hata uhuru wa Tanganyika ulipatikana mwaka gani, mwingine kaulizwa ziwa tanganyika linapitia mikoa mitatu itaje haijui, sasa ubora wa shule ya feza uko wapi.
 
ficha ujinga wako wewe........unataka shule zianze kukataa kushiriki hcho kipindi???
 
Mkuu tusidanganyane Hawa WA hizi shule ni vichwa kweli
Mimi nimemaliza shule ya kawaida Ila rafiki zangu baadhi waluopelekwa kwenye hizi shule wako vizuri wanafanya vizuri na ushahidi ni Wao kunifundisha nikagundua wanajua Sana WANASOMA pia Sana udanganyifu upo shule nyingi tu za binafsi sio Wao pekee.. Japo uwezo wanao
 
Wanafunzi wa shule sampuli hizi Mara nyingi wakifika vyuoni ndo huwa wanapataga tabu sana
 
Kwa hiyo Mwanaasha Kikwete alienda pale kwa uwezo wake?

Sasa mbona matokeo yake yalikuwa tofauti na ya wenzake?

Ni pesa na status ya wazee tu.
Kwanza hujui hata alikoanzia, yule binti alikuwa Kifungilo Girls then akaenda feza girls baada ya usumbufu wake huko kwa masister ambao hawataki ujinga na kujifanya wewe mtoto wa nani, yeye mwenyewe ndio alikuwa hataki shule ile kabisa na lengo lake lilikuwa ni kwenda UK na sio kusoma necta system kabisa. Na kwa matokeo yake yale mabovu yalimpeleka alikokuwa anaota.
Usije ukadanganya watu kuwa kupata four kidato cha nne inamaanisha uliingia shule kwa kuhonga.
Tujiulize wale wa Ilboru, Mzumbe, Kibaha na Tabora nao wakipata four wamehonga kuingia kule?
 
Back
Top Bottom