Kumbe sababu ya kifo cha Mkapa ni Cardiac Arrest. Asante sana mwanafamilia William Erio kumaliza sintofahamu hii

Cardial Arrest inakukuta uwe ama huna malaria. Na sometimes dawa kali zinaweza kuchangia cardial arrest.

Corona haina tabia ya kuua kirafiki kwamba utaongea na watu kisha unakufa gafla. Corona inakubana upumuaji kwa muda mrefu na mateso ya kupumua hayakupi nafasi ya kupiga hadithi.

Mitazamo tu ... am not mjuaji wala mtaalam
No Sio hivyo ndugu yangu. Covid 19 inaanza kama malaria, uchovu mwingi pamoja na misuli kuuma na homa kwa mbali. Hizi dalili zinaweza kudumu kwa siku 4 mpaka 6 then siku ya 7 mpaka 9 ndio siku za hatari zaidi maana hapa unaweza kuamka asubuhi mbavu zinabana pamoja na kifua kuuma na kupumua kwa shida. Ukifanikiwa kuvuka salama siku 11 za mwanzo then uwezekano wa kupona ni mkubwa sana.
Ndio maana wataalam wanasisitiza ukipata dalili za corona ni vizuri ukajitenga kwa siku 14.
NB: Naongea kwa experience ambayo nilipitia
 
T
Ila wananchi waache uzushi..

Wengine wanasema eti ili kuficha ujio wa lissu,

Nani asiye na ubinadamu afanye haya eti kuogopa lissu.

Nadhani wananchi watulie na wazingatie sababu zinazo elezwa.
Tabu mchokonozimchokonozi mwangalie vile.....
Mkuu wangu ni Malaria Kali na mwili wa kizee Tena(geriatric).
 
Wanabodi,
Kumbe sababu ya kifo cha Mpendwa wetu, Benjamin William Mkapa ni Cardiac Arrest!.

Asante sana Mwanafamilia wa familia ya Mkapa, William Erio, kuusema ukweli huu na kumaliza rasmi ile sintofahamu ya chanzo cha kifo, ambayo imezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo JF.

Kama Tangazo la kifo lingezingatia sheria tangu pale mwanzo, wala kusingetokea sintofahamu yoyote!.

Hivyo japo haijasemwa ni JF, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Japo yanalaumiwa kwa kuonekana watu wana mind vitu vidogo vidogo ambayo sio vya msingi, lakini yanasaidia.

Chanzo cha kifo cha ghafla cha any state leader ambaye hajawahi kutamkwa kusumbuliwa na maradhi yoyote, automatically kita send a shock wave kwenda viral.

Baada ya kauli hii, sasa minongo yote kuhusu chanzo cha kifo imemalizwa rasmi.
Naombeni sana, wanabodi, tuwe na heshima kwa viongozi wetu na tuwe na heshima kwa marehemu, mkiisha ambiwa ukweli wa familia, then tuupokee ukweli huu, tuuamini, na kumheshimu Marehemu kwa kuto toa comments zozote negative based on hisia!.

RIP, Mhe. Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.

Paskali

P

Hii ni elimu tu watu wote wanavyokufa wanapata Cardiac Arrest. Watu ambao watakakiwa kusemwa wamekufa kwa i Cardiac Arrest ni Wale tu ambao walikuwa na matatizo ya moyo lakini Mkapa hakuwa na tatizo hilo na ndiyo maana wanafamilia wamesema kulikuwa na matatizo mengine hayo ndiyo yamemuua na sio iCardiac Arrest. Hata wagojwa wa cancer wakifa mwishoni wanapata Cardiac Arrest Pia. Wakati mwingine kwa cancer inaanza na fiko kufa halafu ile sumu ya uchafu ambayo haitoki inasababisha Cardiac Arrest lakini cause inakuwa cancer na figo sio Cardiac Arrest.
 
Kitendo cha kufa chenyewe ni cardiac arest. Kuna mtu anayekufa na moyo ukabakia kuwa active?

Kuna imani kuwa malaika mtoa roho huwa unamuona wakati wako ukifika. Sasa inategemea utampokea vipi. Na ndio maana wengi wao hupata mshtuko baada ya ku realize kuwa muda wake umefika.
 
Tafasiri ya umbea ni kupokea taarifa au kusambaza taarifa ambayo hukuiomba hata wewe ni mbea kwani unahangaika kukataa siyo corona huo ni umbea pia, maana ya umbea ni kusikiliza kupokea taarifa ambazo hukuziomba zije bali zimeletwa na watu.
Kumbe najibizana na wazushi walozusha ni corona kwaheri sitaki kupoteza muda wangu
 
Tanzania kumekuwa na ongezeko la conspiracy theorists sana siku hizi. Hawamuamini hata ndugu wa marehemu aliyekuwa naye hospitali hadi anapokata roho. Mpaka wanafikia kupinga kuwa mtu hawezi kufa kwa cardiac arrest bila kujua kuwa watu wote waliopatwa na cardiac arrest wakiwa wamelala hufa; wanaopona ni wale wanaopatwa na cardiac arrest wakaanguka ambapo huduma ya haraka ya CPR huweza kuokoa maisha yao. Ndugu anasema marehemu alimaliza kusikiliza taarfa ya habari akalala, na daktari walipokuja kumwangalia akamkuta keshafariki. Ni taarifa gani tunazohitaji ili turidhike?

Zamani kidogo kulikuwa na kijana maarufu akijulikana PDiddy wa Maimartha alipata cardiac arrest akaanguka mtaani na kufa hapohapo
 
Hivi cardiac arrest huwa mgonjwa analazwa hospitali, anapiga stori na wanaomtembelea wee ndipo inamuua? Hapa kuna walakini. Itoshe tu kusema RIP Mkapa. Mambo mengine wanafamilia waendelee kuyafanya siri yao, wasiingie kwenye mtego wa kutuliza uvumi unaoendelea.
Ndugu ansema mzee alilazwa kwa maralia na ndiyo aliyokuwa anatibiwa; cardiac arrest imemkuta akiwa amelala akiendelea na matibabu hayo. Kueneza uvumi wowote bila kuwa na uhakika siyo jambo jema kabisa. Taarifa kamili ni za kutoka kwa daktari wake na ndugu zake wa karibu. Ukishawapinga hao basi unakuwa na ajenda yako tu
 
Tanzania kumekuwa na ongezeko la conspiracy theorists sana siku hizi. Hawamuamini hata ndugu wa marehemu aliyekuwa naye hospitali hadi anapokata roho. Mpaka wanafikia kupinga kuwa mtu hawezi kufa kwa cardiac arrest bila kujua kuwa watu wote waliopatwa na cardiac arrest wakiwa wamelala hufa; wanaopona ni wale wanaopatwa na cardiac arrest wakaanguka ambapo huduma ya haraka ya CPR huweza kuokoa maisha yao. Ndugu anasema marehemu alimaliza kusikiliza taarfa ya habari akalala, na daktari walipokuja kumwangalia akamkuta keshafariki. Ni taarifa gani tunazohitaji ili turidhike?

Zamani kidogo kulikuwa na kijana maarufu akijulikana PDiddy wa Maimartha alipata cardiac arrest akaanguka mtaani na kufa hapohapo

Hakulala alijaribu kuamka na ndipo akakata mawasiliano na kuinamisha kichwa. Change of position yawezekana iliongeza mapigo ya moyo then BP, mshipa pwaaa....
 
Tumetafuna pesa nyingi sana kama taifa kwa Kampeni za kutokomeza Malaria, na hata kufikia hatua ya wagonjwa wengi kupimwa nankukutwa hawana malaria na nafasi yake kuchukuliwa na UTI &/au Typhoid.
Leo hii tena BEN afe kwa malaria!!!! Ajabu gani hii
Kwa kiongozi wa kitaifa kusema aliumwa maralia naona ni sawa na kusema aliumwa kipindupindu- NI AIBU
 
Ndugu zangu wenye chuki mnapata tabu sana, Kwani wewe umeambiwa Shambulio la moyo ni lazima liwe na connection na Malaria. Cardiac arrest inaweza kutokea kwa mtu yoyote hata yule ambaye hajawahi kuwa na historia kuugua Moyo
Umeambiwa hivi ili binadamu afe nilazima pawepo na shambulio la moyo, watu wanachotafta ni hilo shambulio la moyo limesababishwa na nini?
 
Umeambiwa hivi ili binadamu afe nilazima pawepo na shambulio la moyo, watu wanachotafta ni hilo shambulio la moyo limesababishwa na nini?
Mkuu ukweli huyo mzee hakufa kwa shambulio la moyo bali kafa kwa Corona lakini wameamua kufanya siri
 
Mkuu Pascal Mayalla

Kuna makosa mengi yalifanyika mwanzoni na kuwa chanzo cha uvumi. Mkapa ni public figure, na ukiwa hivyo hakuna privacy katika maisha. Familia na Ikulu vilipaswa kuelewa jambo hili mapema na kulieleza kiufasaha. Walishindwa

Rais alisema amefariki bila kusema sababu , tena akisema Hospitali bila kuitaja. Hilo tu linatosha kuzusha uvumi
Rais Mstaafu naye kasema aliongea naye saa 1 Hospitali, hakusema ni ipi.

William Urio naye anakuja na maelezo, sidhani kama alipata ushauri wa Daktari.
Alichokieleza William Urio kinaweza kueleweka kwa baadhi, kwa watu wanaojua haya mambo amekoleza uvumi.

Ukisema Cardiac arrest unazungumzia moyo kupoteza uwezo ghafla ambayo ni chanzo cha vifo bila kujali ni kwanini

Kwa upande wa Heart, ukipata Heart attack mara nyingi hupelekea cardiac arrest

Kuna upotoshaji kuwa cardiac arrest lazima mtu afe, no! ni kwamba moyo unapoteza uwezo wa kazi haraka, lakini kwa kutumia njia tofauti kuna resuscitation zinazoweza kuokoa maisha

Kwa maneno mengine, lazima watu waelewe matumizi ya maneno katika medical.

Sasa tukisikia malaria tena ndipo tunazidi kudadisi kwasababu kuna 'gap' na story ni very convoluted

Hivi Taifa limekosa mtaalam anayeweza kueleza hili jambo na kumaliza hizi habari za kubahatisha zinazozidisha uvumi zaidi! Bila maelezo sahihi uvumi utabaki na huenda ukaonekana ukweli hata kama siyo
 
Kwa kiongozi wa kitaifa kusema aliumwa maralia naona ni sawa na kusema aliumwa kipindupindu- NI AIBU
Malaria inatokana na kuumwa na mbu mmoja tu. Rais Mkapa anaweza kuwa ameumwa na mbu huyo wakati akitoka kwenye mkutano wa CCM; siku hiyo alikuwa amevaa shati la mikono mifupi. Malaria huathiri sana wale ambao huwa hawaumwi na mbu kuliko wale ambao wamezowea kuumwa na mbu kila siku.
 
Back
Top Bottom