Kumbe mtandao wa Twitter unaweza kuhatarisha usalama endapo utatumika vibaya, ndio maana huwa unafungwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,946
141,921
Hapa Tanzania Huduma ya twitter haipatikani kwa uhakika hasa baada ya uchaguzi, inawezekana ni kwa sababu za kiusalama.

Rais Uhuru Kenyatta alifunga akaunti yake ya twitter kwa madai kuwa mambo yaliyojaa huko ni kejeli na kuvunjiana heshima na yeye hana muda na mambo kama hayo.

Nchini Marekani twitter wenyewe wameifunga akaunti ya Rais Donald Trump kwa sababu za kiusalama wa nchi.

Kumbe " kufunga" ni namna bora ya kuhakikisha dunia iko Salama.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimekuelewa sana mkuu. Kama serikali ilivyozima mitandao kipindi cha uchaguzi.

Wamemdhibiti Trump asiendelee kupotosha na kuhamasisha maandamano zaidi ya wafuasi wake wanaoamini kuwa Democrats wameiba kura zake.
 
Kwa nini wanaharakati wa haki za habari hawajalalamika Trump kunyimwa haki ya kutoa mawazo yake au kuwalaumu tweeter kunyima washabiki wa Trump kukosa ujumbe kutoka kwa kiongozi wao?
Naona wamekaa kimya ila ingekuwa huku kwetu wangepanua midomo saaanana vitisho,
Je wanaogopa tweeter au wanapendelea democratic?
Wao si ni bingwa wa haki hawaogopi mambo ya usalama kwa watu kukosa haki ya habari
Iweje wanamfungia Trump?

Hizi nchi ndogo tunaonewa saana.
 
Unasema Twitter wamefungia upatikanaji wa mtandao wa twitter Tanzania kwa sababu za kiusalama?!Unaelewa tofauti ya twitter iliyofungiwa Marekani na twitter iliyofungiwa hapa nchini?Kwa nini unalinganisha vitu viwili ambavyo havifanani?Twitter ya marekani imefungiwa na serekali?
 
Haha mkuu tumtagi Fett na Maria...!!
 
Hapa Tanzania Huduma ya twitter haipatikani kwa uhakika hasa baada ya uchaguzi, inawezekana ni kwa sababu za kiusalama.

Rais Uhuru Kenyatta alifunga akaunti yake ya twitter kwa madai kuwa mambo yaliyojaa huko ni kejeli na kuvunjiana heshima na yeye hana muda na mambo kama hayo.

Nchini Marekani twitter wenyewe wameifunga akaunt ya Rais Donald Trump kwa sababu za kiusalama wa nchi.

Kumbe " kufunga" ni namna bora ya kuhakikisha dunia iko Salama.

Maendeleo hayana vyama!
Trump alikuwa anahamasisha vurugu ili rais mteule asiapishwe.Ikumbukwe malalamiko yake(Trump) ya kwamba kura hazikuwa halali yalikuwa yameshafanyiwa kazi,na kiukweli jamaa alishindwa uchaguzi.Sasa huwezi kulinganisha na hapa Tz ambapo mlalamikaji huanza na kukemewa na kutafutwa kukamatwa,kabla ya kuyafanyia kazi malalamiko yake.Tusitumie uelewa wetu mdogo kuhalalisha TZ kufungia mitandao ya kijamii.
 
Inasaidia kulinganisha na Ushenzi uliofanywa Tanzania kufunga Internet Oct 27 hadi Nov.10?
 
Unasema Twitter wamefungia upatikanaji wa mtandao wa twitter Tanzania kwa sababu za kiusalama?!Unaelewa tofauti ya twitter iliyofungiwa Marekani na twitter iliyofungiwa hapa nchini?Kwa nini unalinganisha vitu viwili ambavyo havifanani?Twitter ya marekani imefungiwa na serekali?
Uwe unasoma na kuelewa bwashee!
 
Trump alikuwa anahamasisha vurugu ili rais mteule asiapishwe.Ikumbukwe malalamiko yake(Trump) ya kwamba kura hazikuwa halali yalikuwa yameshafanyiwa kazi,na kiukweli jamaa alishindwa uchaguzi.Sasa huwezi kulinganisha na hapa Tz ambapo mlalamikaji huanza na kukemewa na kutafutwa kukamatwa,kabla ya kuyafanyia kazi malalamiko yake.Tusitumie uelewa wetu mdogo kuhalalisha TZ kufungia mitandao ya kijamii.
Kwahiyo kuna tofauti kati ya Trump na kigogo wa Tanzania?
 
Kila kitu kinaweza kuhatarisha usalama endapo kitatumika vibaya.Hata wewe,mke wako,hawara wako n.k mnaweza kuhatarisha usalama endapo mtatumika vibaya.
 
Uwe unasoma na kuelewa bwashee!
No!Twitter ya Tanzania imefungiwa na serekali lakini kule Marekani account ya twitter ya Trump imefungiwa na kampuni ya twitter baada ya trump kuvunja policy za twitter.Sasa wewe hapa unalinganisha vitu viwili tofauti kabisa!
 
Kwahiyo kuna tofauti kati ya Trump na kigogo wa Tanzania?
Ipo,Trump alijaribu kukatalia madarakani mahakama na vyombo vingine vya nchi vikamkataza,kwa sababu sheria za nchi ziko imara na haziruhusu mtumoja tu kuharibu taifa.Ila kwetu ni directly opposite.
 
Sio kama serikali, Tangu kuanzishwa kwake Twitter huwa wanafungia baadhi ya watumiaji wake wanaokiuka masharti yao, hata hapa bongo wapo wengi tu waliowahi kufungiwa au kufutwa kabisa. Mlikuwa hamjui kwa sababu ni watu wa kawaida tu, hawa wakubwa wamefungiwa ndio maana mnaona ni jambo jipya.
Nimekuelewa sana mkuu. Kama serikali ilivyozima mitandao kipindi cha uchaguzi.

Wamemdhibiti Trump asiendelee kupotosha na kuhamasisha maandamano zaidi ya wafuasi wake wanaoamini kuwa Democrats wameiba kura zake.
 
Inawapa nafuu kuilaumu Marekani ndo maana KM wenu anatapatapa kufukia mashimo.
Tofauti ipo kati ya wafuasi wao lakini masterling wenyewe Trump na Antipas wanafanana sana.

Sema tu wafuasi wa Trump ni majasiri na wale wa Antipas ni waoga wanaogopa kipigo cha deshideshi kachoka!
 
Back
Top Bottom