Kwa sisi Waafrika si jambo la ajabu. Cha msingi familia inajua mke rasmi nani, wengine mtulie
Ni ajabu kwa kweli tunachukulia poa tu ila haya mambo yanaleta mitafaruku kwenye mambo ya Marathi mmoja wapo akifariki.
Nina ushuhuda wa mzee mmoja alipovuta aliibuka mwanamke ambaye kumbe alikuwa na ndoa ya kanisa na marehemu,
Kwenye mstakabali wa kisheria hususani sheria za Marathi hili suala linawezaleta utata.
Wewe mwanaume mkristo unafunga ndoa ya kikristo na mwanamke halafu unamtekeleza kienyeji bila talaka, unatafuta.mwanamke.mwingine mnaishi mnajenga maisha watu wasiokuja zamani wanajua huyo ndio mke wako.
Mnakuwa na mali mwanamke anamuamini mume wake anamuachiq anaandikisha mali kwa jina lake.
Mwanume huyo akifa yule mwanamke mkristo aliyeachwa kienyeji anakuja kuibuka hapo anadai mali zote.zenye jina la huyo mwanaume kwani yeye ana cheti cha ndoa cha kanisani na anapewa wakati hata hakushiriki kuzichuma.
Hili suala msilichukulie kirahisi linaweza leta.utata mkubwa sana .
Kula mbususu mbalimbali hata ikiwezekana kuzaa na wanawake mbalimbali inakubalika ila kwenye kuoa kiholela kwa wakristu ni hatari.
Tatizo watu wanachukulia sifa kuwa na wanawake wengi (mitala) hili suala kisheria halina shida sana kwa waislamu kwani uislamu unaruhusu ndoa zaidi ya moja.
Ila ukristu hairuhusu na hata sheria ya ndoa ya tanzania inatambua msimamo huo wa kanisa
. Ukishafunga ndoa ya kanisani ni suala moja nyeti sana ukizamiria kumuacha huyo mwanamke jitahidi umpe talaka rasmi mahakamani la sivyo anaweza kuja kuibuka wakati umekufa akaleta.mtafaruku