Kumbe magazeti yanayotumiwa kumpaka matope Dr Slaa hayanunuliwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe magazeti yanayotumiwa kumpaka matope Dr Slaa hayanunuliwi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Sep 11, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Juzi katika kupita pita kwangu nilijikuta kwenye banda la muuza magazeti na nilikuta rundo la magazeti mengi ya kila aina. Mengine hata titles zake ndio mara ya kwanza kuziona, na mimi nilikuwa nikitafuta gazeti la mwana halisi na raia mwema ya wiki hii maana siyapati kirahisi mtandaoni.

  Bahati mbaya sikuyapata. Nilikuta yamekwisha. Nilianza kumlaumu sana muuza magazeti kwa kuleta magazeti hayo kidogo. Lakini alinijibu kuwa si kweli kwamba yanakuja kidogo bali yananunuliwa kwa wingi na haraka.

  Katika mazungumzo yangu huku nikimtafiti aliniambia mpaka leo hajajua kwa nini baadhi ya magazeti mengi anayouza hayanunuliwi kama baadhi ya magazeti ambayo alikiri yananunulika kwa kasi ya ajabu.

  Bila kujua kwamba namtafiti alinitajia magazeti ambayo yana kasi kubwa ya kununuliwa kuwa ni MWANAHALISI, RAIA MWEMA, MWANANCHI, na TANZANIA DAIMA. aliniambia kuwa pia kwa mbali kidogo NIPASHE na MAJIRA yanajikongoja lakini mengine hayana mvuto na anayauza kwa shida sana. Kunithibitishia hilo alinionyesha rundo la magazeti ya mtanzania, rai, tazama, uhuru, daily na sunday news, habari leo na mlolongo mwingi wa magazeti ambayo aliniambia hayaendi kabisa.

  Katika kuendelea kumtafiti alisema hana uhakika kwa nini hayanunuliki vizuri hayo magazeti, lakini akasema anadhani mengi ya magazeti hayo yanaonekana kutumika kumpaka matope Dr Slaa. Mie nilipomuuliza kwamba kwa kumsema ovyo Dr Slaa si basi yangeweza kununulika sana? jibu lake lilikuwa hata yeye anashangaa maana alitegemea hivyo.

  Conclusion yangu ikawa hivi kumbe hata watu wameshavichoka vigazeti hivi ambavyo vinajenga negative image kwa Dr Slaa?! Na hapo kwa nini yale yasiyosema lolote mbona yananunuliwa? nika conclude kuwa watu kumbe wameshachoka na uongo na sasa wanapambanua uongo na ukweli.

  Hii ni indicator kwa waandishi, wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kwamba mnajimaliza wenyewe kwa kutumiwa na vyama vya siasa ili mpake matope vyama vingine. Watu wanaanza kuwabaini na kuyaponda magazeti yenu. Shauri yenu, ingawa kwa sasa mnalipwa na mafisadi, hata baada ya uchaguzi watu hawatayaamini na hawatatamani kuendelea kusoma udaku wenu. Na mwisho mtajimaliza wenyewe kama uhuru na mzalendo walivyokwisha.

  Kama waweza fanya utafiti wako pia katika jambo hili. Utaona ukweli wa jambo nililokutana nalo jana.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135  CCM inawalipa milioni 8 kila wanapochapisha habari za uchafuzi
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  so, hawana hasara yoyote? Je baada ya uchaguzi wataendelea kuwapa hiyo subsidy?
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Thubutu!
  Watawaacha kwenye mataa kama mlevi anavyomuacha baamedi anapopata fahamu alfajiri.
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  :confused2:
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Katika hali ya kushangaza, mwezi mmoja tu uliopita nilimpigia simu shangazi yangu kijijni akaniambia kwamba wapo busy na kura za maoni za CCM. Nikamuuliza atampigia nani kura yake, akanambia hakuna mwinigine ni Kikwete tu hata kama ametuongezea ugumu wa maisha. Sikutaka kusema chochote.

  Leo (jumamosi), nimempigia simu kwa issue nyingine tu, yeye mwenyewe akawa wa kwanza kunikumbusha habari za Dr. Slaa akanambia huko kijijni kila mtu anaongelea habari ya Dr. Slaa. Na akaonekana kabisa kuwa tayari kumpa kura Dr Slaa hata kama yeye ni mwanachama wa CCM. Sasa nikilinganisha na hii habari uliyoiandika ndugu mchukia fisadi, napata picha halisi ya jinsi habari za Slaa zinavyosambaa kama moto wa nyika mijini na vijijni, na namna ambavyo ufahamu wa watanzania ulivyoongezeka kiasi cha kutotaka kudanganyika.

  Ni matumaini yangu kwamba msimamo huu ulioanza wa wananchi kuchukia mfumo mbovu uliopo utaonekana hadi kwenye kupiga kura. Hata ambaye hakwenda shule, sasa hivi anatambua kwamba CCM ni wababaishaji na hawana uwezo wa kuongoza nchi.
   
 7. MAWANI

  MAWANI Member

  #7
  Sep 11, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nikichelewa kununua Tanzania daima ikifika saa tatu, maeneo ya Ubungo haulipati tena. Siku hizi, Ndilo gazeti la kwanza kuisha!! Labda wale wapenzi wa CCM watwambie vipi mauzo ya Gazeti la Uhuru?
   
 8. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Uhuru linafaa zaidi kufungia vitumbua na mihogo ya kukaanga
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nenda kwa wauza magazeti watakwambia ukweli. Uhuru halinunuliki. Mi sijui kwa vipi wanaweza kuliendesha gazeti hilo. Na ngoja tu hizo ruzuku za sisi m zikikatika basi limekwisha hilo. Wengine hawaliweki kwenye vibanda vyao vya magazeti maana haliuziki ni kuongeza mzigo wa kuyatunza hadi wauza vitumbua waje kuyanunua.
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kuna baadhi ya magazeti yameuvaa mkenge bure. Magazeti ya RA huwa hayana shida kwa sababu yeye ndiye analipia gharama zote kwa hiyo wanaweza kuendelea kuwepo hata hizi pesa za msimu zikiisha. Hata hivyo magazeti yale yanayotegemea mauzo tu, yatakuwa yamejitangazia kifo baada ya 31 Oktoba 2010.

  Hata hivyo huwa sipati picha, hivi magazeti ya serikali yanakaa mkao gani endapo linaweza kutokea gharika na serikali kwenda kwa chama kingine?
   
 11. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  On the other side, wanunuzi wakubwa wa magazeti mazuri kama T/D, M/H, R/M na Mwananchi ni CCM wenyewe, for good reasons: Wanataka kujua kama ufisadi wao unajulikana. Huwezi kuwa fisadi ukategemea Uhuru waandike, kwa hiyo ukitaka kujua kama siri yako bado siri au imevuja, soma magazeti ya kweli.

  Nina uhakika vigogo wengi siku ya jumatano kabla hawajafanya lolote lazima kwanza wapate nakala zao za Raia Mwema, Mwana Halisi na T/Daima jumatano.

  Na hakuna siku mbaya kama ya Fisadi kupigiwa simu na mmoja wa waandishi wa magazeti hayo. Of course, kwa waandishi hiyo inaweza kuwa bingo, lakini with TAKUKURU on the vicinity, waandishi wa magazeti haya wanaogopa kuchukua rushwa ya mafisadi kwa hofu ya kutegeshewa.

  Mwisho, mafisadi wanapotaka kumalizana pia, wanapenda kukaa karibu na magazeti haya kwa sababu haya yakikuandika watu wanaamini.
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hii issue CCM wanafikiri itawanufaisha but it may actually backfire Kwa sababu inanfanya Dr Slaa ajulikane zaidi hasa huko vijijini ambapo alikuwa hajulikani. Mtu unaweza kuwa famous kwa mazuri na mabaya.
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda article article yako mkuu. Very analytical and well thought. Watu watafikiri magezeti fulani yanauzwa kwa sababu hayacriticise Dr Slaa, but actually yananunuliwa na watu wanataka kujua kama wameandikwa vibaya.
   
 14. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  CCM wenyewe wanayanunua haya magazeti ili habari zisiwafikie wananchi. Mtu mmoja anaweza kuzurura kila sehemu kuhahakikisha anayanunau hata nakala kumi kwa siku, chukulia watu mia kila sehemu kama mwenge standi harafu wote wanalipwa, why not kuisha hayo magazeti. Ukijumlisha la hiyo ya wananchi yanaisha fasta.
   
 15. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Watu vijijini wanasikiliza sana kipindi cha star TV cha magezeti, na wamemfahamu sana dr slaa kwa baadhi ya magazeti kumchafua.

  Kijijini ninakotoka sasa ni Dr Slaa na CHADEMA sisi M wamebaki na watendeji wezi wachache tu.
   
 16. R

  Reyes Senior Member

  #16
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanweza wakawa wanyanunua magazeti kama MH, RM, na Tanzania Daima na kuyachoma moto
  Mbinu hii wanaweza kuwa wamefundishwa na Aboud Aboud wa Morogoro

  Huyu ni Bingwa wa mbinu hii mana pale morogoro Basi lake likogonga na habari hiyo ikiandikwa gazetini yeye hununua magazeti yote na kuyapiga kiberiti
   
 17. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #17
  Sep 12, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,792
  Likes Received: 6,304
  Trophy Points: 280
  Hivi magazeti ya Uhuru na Mzalendo bado yanachapishwa tu? sijawahi kuyaona kwa muda sasa - labda huwa hata siangalii maana nikifika tu kwa muuza gazeti jirani yangu, mwenyewe anajua ninataka Tanzania Daima na Mwananchi as well as Raia Mwema na Mwanahalisi kila Jumatano
   
 18. 1

  1954 JF-Expert Member

  #18
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,184
  Trophy Points: 280
  Hivi magazeti ya Uhuru na Mzalendo bado yanachapishwa tu? sijawahi kuyaona kwa muda sasa - labda huwa hata siangalii maana nikifika tu kwa muuza gazeti jirani yangu, mwenyewe anajua ninataka Tanzania Daima na Mwananchi as well as Raia Mwema na Mwanahalisi kila Jumatano

  Duh, inaelekea wewe ndugu siyo msomaji wa magazeti. Na inawezekana wewe ni mmoja wa i wale ambao wakifika kwenye ubao wa magazeti wanatumia muda mwingi kusoma vichwa vya habari na kuondoka zao bila kununua. Magazeti ya Uhuru na Mzalendo yapo tena yanaandika vizuri tu. ninachofahamu mimi ni kuwa Tanzania Daima limejipambanua na CHADEMA kwani linamilikiwa na Mbowe.
   
 19. 1

  1954 JF-Expert Member

  #19
  Sep 12, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,184
  Trophy Points: 280
  Nenda kwa wauza magazeti watakwambia ukweli. Uhuru halinunuliki. Mi sijui kwa vipi wanaweza kuliendesha gazeti hilo. Na ngoja tu hizo ruzuku za sisi m zikikatika basi limekwisha hilo. Wengine hawaliweki kwenye vibanda vyao vya magazeti maana haliuziki ni kuongeza mzigo wa kuyatunza hadi wauza vitumbua waje kuyanunua.

  Hivi magazeti ya Uhuru na Mzalendo bado yanachapishwa tu? sijawahi kuyaona kwa muda sasa - labda huwa hata siangalii maana nikifika tu kwa muuza gazeti jirani yangu, mwenyewe anajua ninataka Tanzania Daima na Mwananchi as well as Raia Mwema na Mwanahalisi kila Jumatano.

  Suala la magazeti na uandishi wa habari kwa ujumla wake ni nyeti na ambalo linahitaji mjadala mkubwa.

  KImsingi. Uandishi wa habari wa tanzania kwa ujumla wake unatia kinyaa. Msiangalie magazeti ya UHURU na MZALENDO peke yake. Angalieni Tanzania Daima linavyoandika issues kwa kuipamba CHADEMA na Slaa. Angalieni Majira, Soma Mtanzania. Liichambue RAIA na MwanaHALISI. Magazeti yote yana msimamo au upande. Kama Mwishio alivyomwambia MUNYA kwenye BBA kuwa 'you are finished'. Vivyo hivyo na waandishi wa habari wa Tanzania 'they are finished'. Yaani hakuna maadili kabisa ya uandishi wa habari. Chombo pekee cha habari ambacho kwa sasa, kwa kipindi hiki cha uchaguzi, ambacho kiko kwenye msitari ni TBC. Nao nadhani huenda wamepata msaada kutoka nje na ndio maana wanabalance stories zao kwa kuhofia kunyang'anywa fedha walizopata. Vyombo vingine vya habari vyote vilivyobaki vina upande. Wengine wako kwa CCM na wengine wako kwa upinzani. Na ndio maana wanaandamana mpaka kwenye kampeni za wagombea na kulipwa posho na wagombea. Kuna Mwandishi mmmoja wa habari alienguliwa kwenye msafara wa mgombea mmoja. Si mlisikia kelele zilizopigwa na gazeti analoandikia? Hiyo ni kwa kuwa alienguliwa kupata posho.

  J
  Huu
   
 20. K

  King kingo JF-Expert Member

  #20
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mhh kwani Uhuru linauzwa mitaani au wanagaina kwenye ofisi za chama tu...??
   
Loading...