Inasikitisha sana.
Si muda mrefu uliopita ilikuwa ni kawaida kusoma humu JF na kusikia kauli za "ukombozi" kutoka kwa baadhi ya watu.
Mimi, kupitia hii hii JF nikasema hiyo ni kauli aliyoitumia Luther alipokuwa anajitenga na RC.
Haikupita muda Mkapa akawapa dozi live pale Jangwani, wale wote wanaosema "ukombozi" kwa kauli ya Mkapa alisema ni "wapumbavu na malofa".
Dozi hiyo ya Mkapa imewaingia vizuri sana na toka siku hiyo sijaliona hilo neno au kama nimeliona tena basi ni mara moja au mbili kwa wale ambao dozi haijawaingia vizuri.
Haikupita muda nikamsikia kwenye video, kupitia hapa hapa JF, Lowassa akiongea kanisa la kilutheri akisema wamchaguwe kwa kuwa yeye ni Mlutheri na hakuna Mlutheri aliyewahi kuwa Rais kwa hiyo sasa ni zamu yao.
Kwa hayo, sasa nnaamini "mabadiliko" wayatakayo UKIWA ndio hayo ya kutaka dhehebu fulani na watu wa kanda ndiyo watawale.
Kwa sababu nimewasoma sana humu JF, wao wanasema wanataka mabadiliko tu, ukiwauliza "ya nini hayo mabadiliko" hawasemi! Jibu lao ni "sisi tunataka mabadiliko tu"!
Magufuli ananadi mabadiliko na anaeleza hayo mabadiliko yatakuwa yepi.
Ukweli ni kuwa hawa wote wanaobwabwaja mabadiliko domo linakuwa zege inapokuja kusema mbele za watu ni mabadiliko yepi wayatakayo na sababu ni hiyo, wanataka mabadiliko ya dhehebu na ukanda. Hata Lowassa alipolisema hilo aliwafukuza waandishi wa habari kanisani akabaki na Walutheri wenzake tu.
Watanzania tusiwasikilize hawa hata kidogo, hiyo agenda yao ya udini na ukanda waliifanya siri lakini Mwenyeezi Mungu hamfichi mnafik, Lowassa alidhani anaongea siri na Walutheri wenzake, kumbe kuna mtu amemrekodi, ni hatari sana.
Tazama list ya ukawa inayoongozana na Lowassa. Wote Walutheri na wote wa Kaskazini; Lowassa, Mbowe, Sumaye, Mbatia.
Nnamuombea salama tu yule mtu aliye mrekodi Lowassa, maana watu wakifikia kiasi hicho wanakuwa ni hatari sana.
Hawa watu ni hatari sana tena sana na ni wabaguzi wa hali ya juu. Tuhakikishe hawapati kura za kila mwenye kujitambuwa.
#HapaKaziTu