Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,352
- 111,633
Bw. Singh mwenye umri wa miaka 65 hajawahi kuoga wala kukata nywele zake tokea mwaka 1974, hiyo ni muda mfupi tu baada ya kuoa. Hii imepelekea kuaminika kwamba pengine Singh ni mwanadamu mwenye kunuka zaidi duniani.
Akielezea azimio lake hilo, Bw Singh anasema ni kuhani wake ndiye aliyempa ushauri huo na kumuhakikishia kuwa atapata mwana wa kiume kama hataoga.
Licha ya mke wake kumtishia kuwa ataacha kulala naye vilevile majirani kumtania na kumdhihaki, Singh hajaweza kubadili maamuzi yake.
Ingawaje jotoridi la mahali anapoishi hufikia 47C, lakini namna pekee bwana huyu huitumia kujisafi ni kuoga kupitia moto "fire bathing" kila jioni, pia wakati huo huvuta bangi na kuomba kwa mungu wa Kihindu aitwaye Shiva.
Pamoja na imani hiyo Singh hata sasa hajaweza kujaaliwa mtoto wa kiume kwani ameishia kupata watoto saba ambao wote ni wa kike.