Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,955
-
Chanzo ni kukosa mtoto wa kiume, mkewe amkimbia
KUMBE mtu anaweza kupenda uchafu! Jasho la mwilini linaweza kuwa kitu kinachomvutia binadamu. Mzee mwenye umri wa miaka 65, Guru Kailash Singh (pichani), raia wa India, ameweka rekodi ya kunuka.
Habari zinasema kuwa mwili wa Singh haujui maji kwa muda wa miaka 37, hivyo anaandika rekodi ya dunia ya kuwa binadamu aliyekaa kipindi kirefu zaidi bila kuoga.
Inaelezwa kuwa tangu mwaka 1974, Singh aligoma kuoga mara tu baada ya kufunga ndoa na mkewe, Kalavati Devi, 60, kwa madai kuwa hataki tena kuwavutia wanawake.
Baadaye, familia yake iliingilia kati na kumlazimisha kuoga lakini akaendelea kushikilia msimamo wake kabla ya kutoa kisingizio kuwa atafanya hivyo baada ya kupata mtoto wa kiume.
ALIACHA KUOGA AKIWA NA MIAKA 28
Aliacha kuoga akiwa kijana mwenye umri wa miaka 28, sasa ni mzee wa miaka 65, ilisema taarifa hiyo na kuongeza: Kutokana na kutooga kwa miaka 37, mwili wake unanuka, nywele zake ni chafu na zimejisokota dredi zenye urefu wa futi sita.

ANA WATOTO WA KIKE TU
Kwa sasa, Singh ana watoto saba wa kike, kwa hiyo anadai kuwa imani yake inamwambia kuwa asipooga ndipo ataweza kupata mtoto wa kiume.
MTINDO WA MAISHA YAKE
Kwa kawaida, Singh hutumia siku yake kuchunga ngombe kwenye eneo lenye joto kali (nyuzijoto 47). Kila siku jioni huoga kwa mtindo wa kuota moto mkali ambao humfanya atoke jasho jingi (bath fire).
Hujichochea joto zaidi mwilini kwa kuvuta bangi kila jioni sambamba na kusali ibada ya kumtukuza Mungu wa Kihindu, Shiva.
KAULI YA MKE
Kila tukimwambia habari ya kuoga hugombana na sisi kisha huondoka zake. Tumejitahidi mara nyingi sana, tunapotaka kumuogesha kwa nguvu inakuwa ni mshikemshike.
Anasema bora afe kuliko kuoga. Anasisitiza kuwa siku akipata mtoto wa kiume ndiyo atabadili msimamo, alisema mke wa babu huyo na kuongeza:
Nimesitisha kuendelea kulala naye lakini hilo halijamsumbua.
WATOTO WAKE
Watoto wake ni Pooja Singh, 16, Neetu Singh, 25, na Baby Singh, 35 ni watatu kati ya saba wa mzee huyo. Pia anaishi na wajukuu zake, Shradha Singh, miezi 8 months na Mohit Singh, 12.