Kumbe kumbusu mke makalio ni kosa

Kumbe kumbusu mke makalio ni kosa

nhassall

Senior Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
195
Reaction score
41
Abusu Makalio ya Mkewe, Chupu chupu Kutupwa Jela

Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa kutokana na sababu za kisheria mwenye umri wa miaka 48, alikiri kosa lake na kuomba msamaha na hivyo kunusurika kutupwa jela kutokana na kitendo chake cha kuyabusu makalio ya mkewe

Mahakama ya mji wa Hobart katika kisiwa cha Tasmania nchini Australia, ilimuona mwanaume huyo ana hatia ya kufanya shambulizi la kijinsia kwa mkewe kwa kumvua nguo kinguvu na kuyabusu makalio yake.

Mahakama iliambiwa kuwa mwanaume huyo akiwa amelewa alienda nyumbani kwa mke wake aliyetoroka nyumbani kwake ili waweze kuongea na kumaliza tofauti zao.

Mkewe alikuwa amelala kitandani na mara mbili mwanaume huyo alimwambia mkewe alale kifudifudi lakini alipokataa alitumia nguvu kumpindua na kumvua nguo zake za ndani kabla ya kuanza kuyabusu makalio yake huku mkewe akipiga kelele za "No, No".

Wakati watoto wao walipokimbilia chumbani kuona nini kimemtokea mama yao, mwanaume alitoa maneno ya kashfa.

Wakati alipofunguliwa mashtaka ya shambulizi la kijinsia na mkewe na kuhojiwa na polisi, mwanaume huyo alikiri kosa lake na kumuomba msamha mkewe.

Mwanaume huyo alijitetea kuwa aliamua kumbusu mkewe makalio kwa kufikiria kuwa kitendo hicho huenda kikaamsha tena cheche za mapenzi yao.

Hakimu Olivia McTaggart akitoa hukumu alisema kuwa mwanaume huyo anastahili kutupwa jela lakini aliamua kumhukumu kifungo cha nje cha miaka mitatu kwa masharti ya kutofanya tena shambulizi la kijinsia.
 
Yap ni shambulizi la maungoni kwa mtu kutoridhia unachokifanya hata kama ni mme/mke
 
MMmmmmh haya bhana..........................!!
 
Nafikiri kosa ni kumbusu bila ridhaa yake, ukizingatia walikuwa kwenye mtafaruki. Wewe unaenda kuomba msamaha unalewa kwanza, halafu unamlazimisha mtu kulala kitumbo tumbo sijui unamvua na nguo. Hiyo ni assault hata kama ni mkeo kwa kuwa hamkuwa kwenye terms nzuri na amesema hapana.
Eiyer my husband, come and kiss my backyard! LOL
 
Last edited by a moderator:

Mchana huu? Kaunga....unantia majaribuni:tape2:
 
Last edited by a moderator:
Kosa hapo si kumbusu!
Kosa hapo ni kutumia nguvu!
Hakukuwa na ridhaa ya mwanamke!
(Battery)
Hiyo adhabu alistahili ata kama ange mbusu kwenye paji la uso!
 
hahahaha SMU kwani hiyo imeandikwa apo kwen main article? Jamaa alibusu tu kutaka kuwasha upa penzi lao from 'makalioni' haaa
Nimedhani labda mwandishi ametumia neno makalioni ili kupunguza ukali wa kutumia neno "matakoni" ambalo katika contex kama hii ingeweza kuwa na maana ya 'buttocks' tu au hata 'anus'!
 
Hapa kwetu Tanzania wanaume hawabusu tu makalio bali wanalazimisha tendo la ndoa hata kama mkewe hajisikii, je na wao wakashitaki wapi? ikiwa wakienda polisi wanaambiwa polisi haaingilii mambo ya wapenzi na hata wakipigwa manundu polisi huwa wanasema ugomvi wa mme na mke hawawezi kuingilia. Kuna haja ya kuongelea hili jambo kwenye katiba ili kumlinda mwanamke au mwanaume anayenyimwa unyumba pia na mkewe?
 
Huyu atakuwa mla mavi tu huyu,alikuwa hana nia njema kabisa
 
haki za aina hii ni dhambi zingine hizi ndio mila tunazotaka kabla ya kukaa na zetu
 
Kubusu makalio RUKHSA ila kwa ridhaa ya mwenye makalio.... vinginevyo unaweza kucheza lupango.
 
Tatizo ni kesi ya nyani kumpelekea ngedere. Polisi wenyewe ndio namba one kwenye ku abuse wake zao..nategemea nini toka kwao.

Back
Top Bottom