Kumbe Kibonde angepatiwa dawa usiku ule asingefariki dunia

Hospitali ipi hiyo ya uchocho kiongozi?Mwananchi iliyo Jirani /Maeneo ya Makoroboi karibu na ofisi za Tanesco Mkoa wa Mwanza au?Kwani hakufikishwa Bugando moja kwa moja au?
kwanza mgonjwa wa moyo,kapitisha masaa zaidi ya kumi bila dawa,hadi akawa hawezi kutembea,wamempeleka Mz,wakamfikishia hospital ya chocho badala wangempeleka bugando directly,mpaka mtu anazidiwa zaidi na wanampeleka bugando,too late

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo mana nikasema uzembe unachangia
kwanza mgonjwa wa moyo,kapitisha masaa zaidi ya kumi bila dawa,hadi akawa hawezi kutembea,wamempeleka Mz,wakamfikishia hospital ya chocho badala wangempeleka bugando directly,mpaka mtu anazidiwa zaidi na wanampeleka bugando,too late
 
Nimemsikia bwana gadna g.habasi mtangazaji mwenza wa marehemu efrahim kibonde akisema kuwa usiku kule mwanza kuna dawa pale hospital walikosa na akampigia simu dr.isack maro akawaelekeza wakatafute maduka ya mtaani naa usiku ule wakakuta maduka yamefungwa..
Na baada ya kukosa hizo dawa walimjulisha bwana maro kuwa imeshindikana usiku ule,na bwana maro akawaambia kama mmekosa hizo dawa kesho mgonjwa ataamka akiwa hoi zaidi na kweli kesho yake ile alfajiri mgonjwa akaamka akiwa hoi hadi kumpelekea kushindwa kutembea kwa miguu hadi kupandishwa kwenye kile kiti cha matyre (whelchair)..
Hivyo kwa namna moja au nyingine huenda wangefanikiwa kupata hizo dawa usiku ule marehem asingefariki dunia,kuwa ni uzembe wa hospital zetu kukosa dawa au kifo chake ilikuwa ni mipango ya mungu...
R.i.p kibonde mungu akuweke pahala pema
Hapa bongo Vifo vingi asilimia 70 kwa mgonjwa anayepelekwa hospitali huchangiwa na manesi au madokta.
Wengi ni wataalam wa kuzalisha na kufumga vidonda tu.
 
Tunanunua ndege ilhali hospitali hazina dawa. Huyu ni mmoja na anajulikana, wangapi wanakufa kwa sababu kama hii na hakuna anayejua wala kujali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom