Kumbe Google Tanzania ndo hivi ?

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Najaribu kutafuta neno fulani ..naandika "Kum..." matokeo ninayopata ina nilazimu kuachana na google search kwa hilo neno ...naingiza "picha za ..khaa.hapo napo balaa tupu. Sijuia TACRA wanafanya ni nini hapa!!.
 
Hah hah hah! inamaanisha kuwa ukiandika KU unaletewa matoke ya vitu ambayo wabongo wengi tunavyo vi-search kwenye google.....vitu ambayo wanafunzi wengi wanaotumia mtandao uanza kwa kujifunza kusearch picha za uchi na madude mengine mengi tu....Ha
 
I'm sure google ndio wana control database yao na sio TCRA. Kinachoweza kufanywa na TCRA ni kuongea nao as the gvt.
 
google washashindwa kazi sielewi maana ya kueka local domain kama google.co.tz na google.co.ke wakati still database ndo ile ile ya google.com mi nafkiri walitakiwa waangalie na sheria za local waweze kutengeneza kitu bora manake kuban maneno kama boga mhogo ndizi kitumbua na nyanya ni rahisi

mi naona muda si mrefu google itaanza kufunikwa manake search engine kama bing zinakuja juu
 
Anayefahamu, mambo ya INTERNET, Yaani DYNAMIC WEB PAGES, zinakuletea Data kama Database ilivyo, yaani inamaana kwamba neno ambalo linakuwa na rank ya JUU katika SEARCH ndilo linakuwa la kwanza.

Na hivyo, kuweka local domain faida yake ni Utilization of Local language in searching... Indexing
 
Ha ha ha nimeiona. Lakini tatizo sio Google. Tatizo ni akili mbofu mbofu za wabongo. Sasa hata na wewe itakuwaje unatafuta "kum.."? Hilo ni neno gani katika lugha ya Kiswahili. Yaani kum..ninhii nini au nani? Unaona sasa, imekula kwakoo!
 
Mkuu Rungu, nilitaka kutafuta "kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwl J.K
 
Anayefahamu, mambo ya INTERNET, Yaani DYNAMIC WEB PAGES, zinakuletea Data kama Database ilivyo, yaani inamaana kwamba neno ambalo linakuwa na rank ya JUU katika SEARCH ndilo linakuwa la kwanza. Na hivyo, kuweka local domain faida yake ni Utilization of Local language in searching... Indexing
kaka ukitaka kujua google kazi imewashinda angalia hizi website kama filebuzz.com dial112.com fileguru.com softwaregreek.com na nyengine kama hizihawa jamaa bwana wana script ambazo incase unasearch kitu automatically inaonekana kama unachokisearch wanacho kumbe hicho kitu hawana then unapo open unakuta advertisement ya software zao. Kama hujagundua anza kuchunguza leo.
 
Yaani hadi aibu...serikali ipo wapi?! Mfano unamfundisha mtoto au mtoto mdogo jinsi ya kusearch harafu akakuta kinatokea hicho...kwa hakika ataacha analokusudia kusoma na kuangalia hicho nini ni nini

Halafu pia eti kuna "safe search" hii ni uzushi tupu hata mtoto anaweza badilisha na kutoa safe search wangeweka limit
 
Teh teh teh..ndiyo kusema ukitaka ku-google hasa ukiwa nyumbani na watoto inabidi kwanza uwatume dukani..!!!!
 
mmenikumbusha image moja jamaa aliandika white people stole my car lakini ktk sujjection ikaleta ..did you mean black people stole your car?. hii inamaanisha wanaotafuta record zaidi ya kuibiwa magari ni white zidi ya black
 
Mimi nadhani google inaleta search history kwenye device husika!
kama computer yako ili search mambo ya ajabu ajabu lazima mtu mwingine akija ku search kwenye computer yako ataletewa high ranked search kwenye computer yako!
Hapo jiulize mwenyewe nini unaki- search zaidi??
 
Bing ndo search engine inayochuja vizuri adult content. Mfano: Ukifanya image search kwenye bing inayohusu mambo hayo zile picha zinakuwa zimefifia hazionekani kabisa tofauti na google.

Google inaendeshwa kwa sheria. Kuzuia kitu kamahi hicho kitawanyima uhuru na habari wateja na watumiaji wa mtandao kwa ujumla. Sio kila mtu ana search kwa lengo baya.

Lakini kwa kuwa Google ina local domain karibu kila nchi basi kuna haja ya mamlaka husika kuongea na google ili kuchuja baadhi ya search results.
 
mmenikumbusha image moja jamaa aliandika white people stole my car lakini ktk sujjection ikaleta ..did you mean black people stole your car?. hii inamaanisha wanaotafuta record zaidi ya kuibiwa magari ni white zidi ya black

Haha mkuu wewe naye usinambie unaamini kua hilo lilikua la ukweli, hizo jokes ambazo mtu yeyote anaweza kutengeneza afu anatuma online usizichukulie serious
 
Nnachoona hapa ni kukaribisha CENSORSHIP maana hao TCRA watatumia nguvu kidogo kuziba hilo tatizo na watatumia nguvu nyingi kulinda wanasiasa mitandaoni kwa kigezo cha maadili na amani ya nchi, viongozi watafanya madudu ila taarifa zao chafu na mbaya hatutazisikia, itakuwa kama magazeti taarifa muhimu zenye maslahi ya wananchi zitakandamizwa.
 
Mi siwalaumu Google hii tabia ni wabongo tulioizaa, kumbuka kuwa Google search ina database ambayo kila neno unaloingiza huhifadhiwa ili siku nyingine mtu anapoingiza herufi za kwanza inafanya indexing halafu inakuletea maneno ambayo huenda ulikuwa unatafuta, sasa ni lini Google wanajua mnachoingiza ni matusi!!?
 
Najaribu kutafuta neno fulani ..naandika "Kum..." matokeo ninayopata ina nilazimu kuachana na google search kwa hilo neno ...naingiza "picha za ..khaa.hapo napo balaa tupu. Sijuia TACRA wanafanya ni nini hapa!!.
we unashangaa hilo andika "university students" uone matokeo alafu andika "wanafunzi wa vyuo" uone matokeo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom