Usikubali kumaliza Chuo bila skills hizi

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Ikiwa ndio kwanza unajiunga na chuo au upo chuo; aidha unaingia mwaka wa pili au wa
tatu, wakati ni sasa na bahati ni yako. Kiukweli ukiwa chuoni huwezi ku “feel” tatizo la
ajira ambalo wahitimu wengi sana wanalipitia kwa sasa, ukiwa chuo kuna ule ulevi wa
boom au ile hali ya kutopitia changamoto za maisha, haukutani nazo. Hii inakufanya u
“relax” kwa kuwa ukilalia double decker yako una uhakika wa kuamka kesho.

Leo nataka uungane na mimi katika kujifunza baadhi ya skills ambazo unaweza kujifunza,
si tu kwa kulipia ada shuleni, kwa sababu nakupa hakika ya kuwa, bila kujali unasoma
kozi gani, uhakika wa ajira mtaani ni mdogo. Ila skills hizi zitakupa fursa ya kujifunza na
kuwa kwenye nafasi nzuri mtaani bila kujali unasoma kozi gani.

Ujuzi ambao naenda kushare nawe leo hii ni ujuzi ambao hautajifunza shuleni, na mfumo
wa elimu yetu hauwezi kukuruhusu uujue, bali utajifunza tuu endapo utakuwa umemlipa
mtu, au kupitia majukwaa ya mtandaoni kama Udemy, Youtube na Coursera.

Hapa mimi
nakupa free course kupitia hii chapisho, lengo langu ni moja, yaani kuamsha uwezo wa
ziada ambao unao wewe kama mwanafunzi wa chuoni, ili utokapo usikae kutafuta ajira
kwa kupigwa na jua na kuzungusha vyeti.

Kwanini ujifunze ukiwa chuo?
Kwa ufupi sana nikuhakikishie kuwa; chuoni ndio pahala unaweza kujifunza, ndio sehemu
ambayo unaweza kuwapa hata wazazi wako excuse ya kuwa upo busy kusoma na
wakakuelewa, lakini ukitoka huku ni suala tofauti.

Basi tuchukue wasaa huu kuziona skills ambazo zinaweza kukuweka kimasomaso mtaani
baada ya chuo. Zingatia;

1. Freelancing; kwanza ni kitu gani? Nisikuchoshe! Freelancing ni kitendo cha kuuza
huduma inayotokana na ujuzi wako aidha mtandaoni au nje ya mtandao na kuingiza
kipato. Kufanya freelancing kumbe unahitaji kuwa na ujuzi fulani.

Yaani watu wakutambue kuwa mjuzi wa jambo mathalani kupiga picha, kufanya graphics,
kutafsiri lugha, kuuza sarafu n.k. hii inafanyika ilhali hakuna kampuni au taasisi
yoyote ikiwa imekuajiri, bali ni wewe mwenyewe. Inaweza kufanyika mtandaoni
pia kupitia majukwaa kama Upwork, Fiver, Microjobs n.k.

usishangae!!

Hizi ni websites pia applicaations ambazo, kwa watu wa fani yoyote wanaweza kutumia
ujuzi wao kuingiza kipato. Yaani mtu kama mwalimu wa somo la Kiingereza
anaweza kujisajili na akapata kazi ya kufundisha Kingereza mtu aliye mbali na eneo
lake, pia mtu kama daktari anaweza kupata kazi inayohusu taaluma yake. Kwa
mfano, mtaalamu wa elimu ya wanyama anaweza kupewa kazi ya kutafsiri nakala
inayohusu kada yake? Kwa mtindo huu unahitaji kuzunguka na bahasha?

2. Graphics and design; mimi nimeshuhudia watu hawa wakiishi vizuri. Je ni wakina
nani haswa? Kwanza nikwambie, ulimwengu tulio nao sasa ni ulimwengu wa
taarifa, ni ulimwengu ambao si biashara ya huduma au bidhaa inahitaji matangazo,
unadhani matangazo ya kuwaambia tu watu wanunue? Hapana, si umewahi kuona
mabango ya wauza simu? Nguo? Keki? Laptop? Watoa huduma za usafiri? MC? Na
wengineo? Basi yale mabango hayawekwi tuu, mpaka unaona linakuvutia vile ujue
kuna mtaalamu ambae amebobea kwenye kazi anayofanya; na huyu si mwingine
bali ni graphic designer, huyu ni mtaalamu wa rangi, muonekano, muundo na hata
picha. Upo? Unamalizaje chuo bila kuwa na huu ujuzi?

Kuna applications kama
Canva, Figma na Adobe ambazo zinakupa fursa ya kuwa graphic designer. Usikae kinyonge.

3. Photography; nadhani kila mmoja anaujua ujuzi huu; kwa taarifa fupi ni kuwa,
Tanzania na Afrika kwa ujumla ni mahala ambapo pana upungufu mkubwa wa
wapiga picha wa kike, Wanawake mpo? Simaanishi kuwa fursa hii ni ya wanawake tuu, bali hata wanaume; huku mtaani watu wana shughuli zao, siku hizi mpaka
misiba inataka picha. Wewe unangoja nini kujifunza?

Yaani mtu akiwa na birthday
kidogo kataka picha, kwa hitaji hili maana yake wanakuhitaji wewe, na namna
mambo yalivyo ni kuwa endapo utaweza kumpiga mtu picha mara moja tuu, na
ukafanya vizuri, basi wewe ndiye mpiga picha wake. Hulali njaa.

4. Copywriting, SEO na SMM; Najua umechanganyikiwa na hivyo vifupisho, usijali,
lakini kwanza tuanze na copywriting. Hivi umewahi kutembea mjini au maeneo
yenye watu wengi ukakutana na mabango makubwa yana maandishi ya kutanganza
biashara, hivi unajua hakuna anayeweka mamilioni yake ya pesa kutangaza biashara
pale halafu tangazo likaandikwa ili mradi?

Basi wapo wataalamu wa kuandika tangazo kiasi cha kuvutia wateja wa bidhaa ama huduma inayotangazwa, hawa
wanaitwa Copywriter na kinachoandikwa pale kinaitwa copy, kuna kozi maalumu
kule Youtube, kama una msuli wa kufikiria vizuri na kuandika basi wakati ni huu.

Hiyo kozi yako ya Ualimu na Business administration huku mtaani haitakiwi,
jifunze kucheza na maneno ya kuvutia wateja kununua bidhaa, watu wana biashara
zao na hawajui namna ya kuandika. Just be one. Halafu kuna hiyo.

SEO basi huwezi kuifanya mpaka uwe copywriter mzuri, kwanza hiyo inamaanisha
Searching Engine Optimization; kwa mfano sasa hivi ukaamua kuingia google
utafute maana ya neno “honey” hivi ujue unaweza kukutana na Zuchu? Eeh!

Unakutana na Zuchu, sasa imagine rafiki yako anauza asali, na unataka kuifanyia
matangazo google, unataka kuiandika kwa Kiingereza, kwani asali nayo si inaitwa
Honey? Sasa hapa ndio tutajua kama wewe ni Optimizer ama sio! Yaani uandike
tangazo ambalo, katika machaguo matatu ya juu ya Google na hilo tangazo la rafiki
yako lipo.

Si unaona kama unapaswa kuwa muandishi mzuri? Mbali na hapo zipo
njia za kunyanyua tangazo, je ni nani anazijua? Unapaswa kujifunza na ndipo
utaweza kuendana na soko.

SMM yaani Social Media Management; huku mtaani bwana watu wenye biashara
wana akaunti za mitandao ya kijamii zaidi ya moja, anahitajika mtu ambae ataweza
kuzisimania zote kwa ufanisi na kuziandikia maelezo?

Sasa huenda haujui ila kuna
applications kama MetaBusiness na Metrocool zinatumika ku operate acconts zaidi
ya moja. Unaweza kujifunza? Basi wakati ndio huu. Usiondoke chuo bila huu ujuzi,
utajuta.

5. Digital sports and entertainment analysis; hivi unajua ka,ma namna unavyofuatilia
michezo na burudani kama muziki unajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na story za
kuwaambia watu? kwa mfano; kwa kadiri unavyofuatilia mpira, nafasi yako katika
kuuchambua inazidi kuwa kubwa, ukikaa kijiweni unakuwa na muda wa kupigisha
watu stori, ebu watazame kwa makini, wanakusikiliza?

Na licha ya kukusikiliza,
wanakubaliana na wewe? Kama jibu ndio, basi booom!!

Umeshapata mchongo, ebu
fanya hivyo hivyo kaama una mastori kuhusu muziki na filamu. Kaa chini utulie,
chimba unachoweza kuchimba, leta stori ya football au mziki kwenye Ukurasa wako
wa mtandao wa kijamii. Lipo kundi kubwa la watu utachukua macho yao, basi
nikwambie siku hizi kuna kitu kinaitwa “attention economy” watu wanapiga pesa
kwa kukusanya macho na masikio ya watu wengine, yaani mimi kama mfanyabiashara
nikishaona una watu wengi wanaokufuatilia, nitakulipa uniwekee tu biashara yangu
kwenye ukurasa wako, huyo ni mimi peke yangu, kama tupo kumi je? Kazi kwako!!
Wakati mwingine watu wenye kipaji cha kuchambua soka wanaajiriwa na media
kubwa nchini, ikiwa unataka kuajiriwa.

Nikusihi kuwa; wakati wote huo uliopo chuoni hakikisha unailinda afya yako, kwa sababu
yote yaliyopo hapo yatasalia kuwa stori tuu endapo hautakuwa na afya njema; epuka ngono zisizo salama, epuka matumizi ya vilezi kama pombe na madawa. Yote kwa yote nakutakia usomi mwema.
 
Na kama unasomea haya masomo hapo chini, hakikisha unajifundisha mwenyewe binafsi kwa muda wako mpaka ujue kibobezi haswa, huko ma lectures wenyewe ni wazugaji anapapasa kutumia kitabu wao wenyewe hawajui vizuri

Electrical/Electronics Engineering - hakikisha unajua kutumia kwa uelewo mkubwa simulation software and CAD(electrical), sio unatoka umepapasasa ukidhani kazini utakuna na maswali ya kirchoffs sijui lenz law, hivi ndio vitendea kazi vya fani yako, utaulizwa unajua kutoa circuit diagram kwenye CAD au Installation nzima ya jengo kutumia CAD electrical, Chagua ile inayotumika sana makazini na jikite uijue kama professinal
1700485891602.png

Mechanical/Structural Engineering - Hakikisha unajua hasa kutumia 2D/3D CAD softaware kama mtaalamu haswa, yaani ujue mpaka kutumia Finite Element Analysis(FEA), sio unatoka na kichwani umejaza calculation ya beam sijui kuderive bernoulli equation, halafu ukifika usaili unaulizwa unaweza kutoa mchoro 3D CAD from scratch unaanza kujiumauma.

1700486000593.png

IT/Computer/Software/Cyber Engineering - Hapa ndio kuna ile dhana ya "huyo ni IT wa kibongo, sababu watu wanasoma na kumaliza anatoka hata kutengeneza software/website na kuiunga na database hajui, unakuta amekariri ma hexadecimal IP address calculation sijui processor power calculation,

kama ni software developer chagua moja au mbili zinazotumika katika soko na jifunze mwenyewe hakuna lectures atakufundisha hizi
1700486939202.png

Kama web/mobile developer, ni pia hivyo hivyo, kamatia unaoona ina soko na jifundishe mwenyewe

1700487220668.png

1700487093523.png
 
Nyuzi muhimu kama hizi huwezi tuona, tumejaa kule kwny kubashiri na kula matunda kimasihara. Mambo ya mustakabali wa maisha yetu wala hatuna muda nayo kabisaa....mleta mada, andiko safi....barikiwa
 
Ikiwa ndio kwanza unajiunga na chuo au upo chuo; aidha unaingia mwaka wa pili au wa
tatu, wakati ni sasa na bahati ni yako. Kiukweli ukiwa chuoni huwezi ku “feel” tatizo la
ajira ambalo wahitimu wengi sana wanalipitia kwa sasa, ukiwa chuo kuna ule ulevi wa
boom au ile hali ya kutopitia changamoto za maisha, haukutani nazo. Hii inakufanya u
“relax” kwa kuwa ukilalia double decker yako una uhakika wa kuamka kesho.

Leo nataka uungane na mimi katika kujifunza baadhi ya skills ambazo unaweza kujifunza,
si tu kwa kulipia ada shuleni, kwa sababu nakupa hakika ya kuwa, bila kujali unasoma
kozi gani, uhakika wa ajira mtaani ni mdogo. Ila skills hizi zitakupa fursa ya kujifunza na
kuwa kwenye nafasi nzuri mtaani bila kujali unasoma kozi gani.

Ujuzi ambao naenda kushare nawe leo hii ni ujuzi ambao hautajifunza shuleni, na mfumo
wa elimu yetu hauwezi kukuruhusu uujue, bali utajifunza tuu endapo utakuwa umemlipa
mtu, au kupitia majukwaa ya mtandaoni kama Udemy, Youtube na Coursera.

Hapa mimi
nakupa free course kupitia hii chapisho, lengo langu ni moja, yaani kuamsha uwezo wa
ziada ambao unao wewe kama mwanafunzi wa chuoni, ili utokapo usikae kutafuta ajira
kwa kupigwa na jua na kuzungusha vyeti.

Kwanini ujifunze ukiwa chuo?
Kwa ufupi sana nikuhakikishie kuwa; chuoni ndio pahala unaweza kujifunza, ndio sehemu
ambayo unaweza kuwapa hata wazazi wako excuse ya kuwa upo busy kusoma na
wakakuelewa, lakini ukitoka huku ni suala tofauti.

Basi tuchukue wasaa huu kuziona skills ambazo zinaweza kukuweka kimasomaso mtaani
baada ya chuo. Zingatia;

1. Freelancing; kwanza ni kitu gani? Nisikuchoshe! Freelancing ni kitendo cha kuuza
huduma inayotokana na ujuzi wako aidha mtandaoni au nje ya mtandao na kuingiza
kipato. Kufanya freelancing kumbe unahitaji kuwa na ujuzi fulani.

Yaani watu wakutambue kuwa mjuzi wa jambo mathalani kupiga picha, kufanya graphics,
kutafsiri lugha, kuuza sarafu n.k. hii inafanyika ilhali hakuna kampuni au taasisi
yoyote ikiwa imekuajiri, bali ni wewe mwenyewe. Inaweza kufanyika mtandaoni
pia kupitia majukwaa kama Upwork, Fiver, Microjobs n.k.

usishangae!!

Hizi ni websites pia applicaations ambazo, kwa watu wa fani yoyote wanaweza kutumia
ujuzi wao kuingiza kipato. Yaani mtu kama mwalimu wa somo la Kiingereza
anaweza kujisajili na akapata kazi ya kufundisha Kingereza mtu aliye mbali na eneo
lake, pia mtu kama daktari anaweza kupata kazi inayohusu taaluma yake. Kwa
mfano, mtaalamu wa elimu ya wanyama anaweza kupewa kazi ya kutafsiri nakala
inayohusu kada yake? Kwa mtindo huu unahitaji kuzunguka na bahasha?

2. Graphics and design; mimi nimeshuhudia watu hawa wakiishi vizuri. Je ni wakina
nani haswa? Kwanza nikwambie, ulimwengu tulio nao sasa ni ulimwengu wa
taarifa, ni ulimwengu ambao si biashara ya huduma au bidhaa inahitaji matangazo,
unadhani matangazo ya kuwaambia tu watu wanunue? Hapana, si umewahi kuona
mabango ya wauza simu? Nguo? Keki? Laptop? Watoa huduma za usafiri? MC? Na
wengineo? Basi yale mabango hayawekwi tuu, mpaka unaona linakuvutia vile ujue
kuna mtaalamu ambae amebobea kwenye kazi anayofanya; na huyu si mwingine
bali ni graphic designer, huyu ni mtaalamu wa rangi, muonekano, muundo na hata
picha. Upo? Unamalizaje chuo bila kuwa na huu ujuzi?

Kuna applications kama
Canva, Figma na Adobe ambazo zinakupa fursa ya kuwa graphic designer. Usikae kinyonge.

3. Photography; nadhani kila mmoja anaujua ujuzi huu; kwa taarifa fupi ni kuwa,
Tanzania na Afrika kwa ujumla ni mahala ambapo pana upungufu mkubwa wa
wapiga picha wa kike, Wanawake mpo? Simaanishi kuwa fursa hii ni ya wanawake tuu, bali hata wanaume; huku mtaani watu wana shughuli zao, siku hizi mpaka
misiba inataka picha. Wewe unangoja nini kujifunza?

Yaani mtu akiwa na birthday
kidogo kataka picha, kwa hitaji hili maana yake wanakuhitaji wewe, na namna
mambo yalivyo ni kuwa endapo utaweza kumpiga mtu picha mara moja tuu, na
ukafanya vizuri, basi wewe ndiye mpiga picha wake. Hulali njaa.

4. Copywriting, SEO na SMM; Najua umechanganyikiwa na hivyo vifupisho, usijali,
lakini kwanza tuanze na copywriting. Hivi umewahi kutembea mjini au maeneo
yenye watu wengi ukakutana na mabango makubwa yana maandishi ya kutanganza
biashara, hivi unajua hakuna anayeweka mamilioni yake ya pesa kutangaza biashara
pale halafu tangazo likaandikwa ili mradi?

Basi wapo wataalamu wa kuandika tangazo kiasi cha kuvutia wateja wa bidhaa ama huduma inayotangazwa, hawa
wanaitwa Copywriter na kinachoandikwa pale kinaitwa copy, kuna kozi maalumu
kule Youtube, kama una msuli wa kufikiria vizuri na kuandika basi wakati ni huu.

Hiyo kozi yako ya Ualimu na Business administration huku mtaani haitakiwi,
jifunze kucheza na maneno ya kuvutia wateja kununua bidhaa, watu wana biashara
zao na hawajui namna ya kuandika. Just be one. Halafu kuna hiyo.

SEO basi huwezi kuifanya mpaka uwe copywriter mzuri, kwanza hiyo inamaanisha
Searching Engine Optimization; kwa mfano sasa hivi ukaamua kuingia google
utafute maana ya neno “honey” hivi ujue unaweza kukutana na Zuchu? Eeh!

Unakutana na Zuchu, sasa imagine rafiki yako anauza asali, na unataka kuifanyia
matangazo google, unataka kuiandika kwa Kiingereza, kwani asali nayo si inaitwa
Honey? Sasa hapa ndio tutajua kama wewe ni Optimizer ama sio! Yaani uandike
tangazo ambalo, katika machaguo matatu ya juu ya Google na hilo tangazo la rafiki
yako lipo.

Si unaona kama unapaswa kuwa muandishi mzuri? Mbali na hapo zipo
njia za kunyanyua tangazo, je ni nani anazijua? Unapaswa kujifunza na ndipo
utaweza kuendana na soko.

SMM yaani Social Media Management; huku mtaani bwana watu wenye biashara
wana akaunti za mitandao ya kijamii zaidi ya moja, anahitajika mtu ambae ataweza
kuzisimania zote kwa ufanisi na kuziandikia maelezo?

Sasa huenda haujui ila kuna
applications kama MetaBusiness na Metrocool zinatumika ku operate acconts zaidi
ya moja. Unaweza kujifunza? Basi wakati ndio huu. Usiondoke chuo bila huu ujuzi,
utajuta.

5. Digital sports and entertainment analysis; hivi unajua ka,ma namna unavyofuatilia
michezo na burudani kama muziki unajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na story za
kuwaambia watu? kwa mfano; kwa kadiri unavyofuatilia mpira, nafasi yako katika
kuuchambua inazidi kuwa kubwa, ukikaa kijiweni unakuwa na muda wa kupigisha
watu stori, ebu watazame kwa makini, wanakusikiliza?

Na licha ya kukusikiliza,
wanakubaliana na wewe? Kama jibu ndio, basi booom!!

Umeshapata mchongo, ebu
fanya hivyo hivyo kaama una mastori kuhusu muziki na filamu. Kaa chini utulie,
chimba unachoweza kuchimba, leta stori ya football au mziki kwenye Ukurasa wako
wa mtandao wa kijamii. Lipo kundi kubwa la watu utachukua macho yao, basi
nikwambie siku hizi kuna kitu kinaitwa “attention economy” watu wanapiga pesa
kwa kukusanya macho na masikio ya watu wengine, yaani mimi kama mfanyabiashara
nikishaona una watu wengi wanaokufuatilia, nitakulipa uniwekee tu biashara yangu
kwenye ukurasa wako, huyo ni mimi peke yangu, kama tupo kumi je? Kazi kwako!!
Wakati mwingine watu wenye kipaji cha kuchambua soka wanaajiriwa na media
kubwa nchini, ikiwa unataka kuajiriwa.

Nikusihi kuwa; wakati wote huo uliopo chuoni hakikisha unailinda afya yako, kwa sababu
yote yaliyopo hapo yatasalia kuwa stori tuu endapo hautakuwa na afya njema; epuka ngono zisizo salama, epuka matumizi ya vilezi kama pombe na madawa. Yote kwa yote nakutakia usomi mwema.
Mkuu umekosea,,,ujuzi pekee ni wa kuchungulia hela ipo wapi fasta unaifuata,,,,mengine hekaya
 
Uzi umekaa vyema mno. Wanachuo hawatakuelewa mpaka watakapokuwa demanded kuonesha level yao ya expertise (kwenye hizo softwares) huko wanakoenda kuomba kazi.
Salute kwa AutoCAD na Circuit Maker. Adruino 💪
 
Back
Top Bottom