Kumbe freemasons ni watu poa sana!

Kumbe freemasons ni watu poa sana!

Iko hivi watu huwa hawaelewi, wanafikiri mtu akishakuwa freemason basi anajua kila kitu kuhusu freemason, si ajabu hata aliyeanzisha uzi huu hana hata degree moja ya masonic kwa hiyo anachojua kwa level yake ndio hicho,lakini kumbuka kuna degree 33 za freemason, na mambo mengine ni ya ndani kabisa hayatoki njee kabisa unless kama uliwahi kuwako ukatoka lakini huwa yanabaki kuwa siri za Master Masons.

Ni sawa na kumuuliza balozi wa nyumba kumi kuhusu mikataba ya siri ndani ya wizara ya nishati na madini ingawa ni serikali moja chama kimoja lakini hajui lolote zaidi sana atasifia au kupondea asichokijua, lakini vipi umuulize katibu mkuu wa wizara husika ingawa hawezi kukuambia maana ni siri lakini anaelewa in and out ndani ya wizara yake, kwa hiyo ndugu kila mtu anakula taarifa kwa urefu wa level yake [emoji16], hata kwenye imani yako au dini yako unakoabudu yapo mambo ambayo yanaishia kwa viongozi tu na ni mwiko muumini kujua unless apande level achaguliwe na hata akijua haruhusiwi na yeye kuyasema, yaani hata kuwe na transparency kiasi gani siri za ofisi huwa hazikosi hususan kwenye taasisi zote secular na non secular.

Ni kwamba hata Mungu ana siri tofauti ni kwamba "siri za Bwana zipo kwa wamchao nae atawajulisha agano lake"[emoji847], ndio maana hata ufahamu kuhusu Mungu hutofautiana kati ya mchungaji na mchungaji kati ya imamu na imamu kulingana na level yake ya ufahamu alionao, ingawa anaweza(anaweza, sijasema ni mmoja) kuwa yule yule lakini mmoja akamjua zaidi ya wengine na hapo haimaanishi huyu anayejua kidogo sio wake, no wote ni wake ila level of understanding zimetofautiana, moja ipo high nyingi ni for beginners

Niwaambie ukisikia mtu anakuambia ni watu poa hata usimshangae na yeye ndio level aliyofikia, ni kama vile kitunguu kilivyo na layers nyingi na kila moja haijui ndani yake kuna nini, ganda la njee halijui katikati kuna nini, ila katikati ndio palitoa kila kitu, kwa hiyo wa ndani anaelewa ya njee lakini wa njee hajui yaliyomo ndani, lakini ukienda mpaka kwenye kiini ndio utatambua ya kuwa haikuwa chama tu cha kusaidiana bali ni imani kamili ya kumwabudu shetani directly na mara nyingi utakuwa umeshachelewa maana hamnaga kusema kwamba mi nilikuwa sijui kama tunamwabudu Master(Lucifer) kwa hiyo sitaki kuendelea na haya mambo, aise hautasahau watakachokufanya, sheria za hawa mabwana ni kwamba once you become masonic your masonic forever.

Master huwa hafanyi kazi za hasara, kwamba akupe fedha magari kupitia chama chake cha kusaidiana [emoji16] halafu ukaja kugundua kumbe nyuma ya huo msaada yupo yeye, halafu ukimbie umtie loss kizembe, ndio maana ukiacha kama kanumba eti unaanza kuomba ushauri sijui kwa nani mara umuulize fulani nifanyeje nijitoe wao walishakuona kwenye radar zao mapema sana with (all seeing eye [emoji2539]) mapema na nia yako ya kusaliti chama ndio kifo cha ghafla hutokea maana umemgundua na unataka kumuacha kwa hiyo wanakutanguliza wewe kwanza kwa sababu ya mkataba ulioingia halafu unataka kuuvunja kinyemela, ndio maana ya ile kauli ya welcome but not return, na siku tukipata muda tutajadili huwa wanaenda kufanya nini baada ya kufa hivyo ghafla maana kiuhalisia huwa hawafi ni kama mazingara anavyochukuliwa mtu msukule ile kumbe kuna sehemu anakula ngese ya kutosha.

Maana yeye anachofanya ananunua nafsi za watu ili wamwabudu kama Mungu wao kwa malipo ya fedha nyumba na magari na mafanikio ya duniani, na kama utakumbuka kuna imani moja inaelezea kisa kimoja ambapo Master (Lucifer) aliwahi kumjaribu mwana wa Mungu akisema kama ukiinama na kunisujudia, nitakupa hivi vyote na fahari yake lakini kwa sharti la kuniabudu, nafikiri kwa wasomaji tunaelewa alichojibiwa. Lakini ndivyo ilivyo hata sasa hivi, yeye hana shida hata ya kukupa ulimwengu wote ilimradi anase nafsi yako, ndio maana Mwana akasema "itamfaidia nini mtu aupate ulimwengu wote halafu apate hasara taslimu [emoji16]ya nafsi yake (uhai wake).

Ndipo utaelewa kuwa Master hafanyi biashara ya hasara maana gharama ya nafsi ya mwanadamu mmoja ina thamani kuliko chochote unachoweza kukiona katika ulimwengu huu ndio maana ukombozi wake haukuwa wa fedha au dhahabu au majumba bali ilihitajika kafara ya damu isiyo na hatia ili kumkomboa, lakini leo shetani anauziwa nafsi kwa bei sawa na Bure[emoji16][emoji847] inashangaza sana, mtu anajitoa kumwabudu shetani kwa fedha isiyofika hata milioni 100 hata kama ingekuwa bilioni moja lakini ukilinganisha na thamani ya nafsi ya mwanadamu ni sawa na wazee wetu walivyokuwa wanatoa dhahabu kwa malipo ya vioo vya kijiangalia na manukato, ingawa tunawaona walikuwa wajinga lakini wao wana afadhali maana walibadilishana vitu kwa vitu, ila hiki kizazi chenye akili tunachosema kimestaarabika tunauza nafsi kwa vitu na sio nafsi zetu tu hata za ndugu zetu na watu wengine wasio na hatia kwa mafanikio ya duniani ya muda kitambo, lakini utambue huwa wana kaulimbiu moja You are welcome but not return, Rahisi kuingia lakini sio kutoka.

Ni kweli Mungu ndie aliiumba duniani (Earth) lakini Ulimwengu kwa maana ya world systems zimetengenezwa na hawa watu ndio maana wanajiita wajenzi huru, kwa maana ya kuwa ndio watengenezaji wa Dunia tunayoiona ya ushoga, vita, majanga, njaa, mabadiliko ya tabia ya nchi, na akitokea mtawala mwenye kuwapinga wanamterminate mapema sana asije akaharibu mipango Yao, utajiuliza mbona tunafanya uchaguzi, huo uchaguzi unaujua wewe wao wana watu wao na wanajua wanatumia njia gani kuwaweka kwenye mamlaka. Ndio maana utashangaa ukitaka haki kabisa au kutenda haki kabisa lazima upate upinzani wa kutosha kwa sababu mifumo haisapoti haki kutendeka ukiamka unapinga ushoga utashangaa unashtakiwa kwa kukiuka haki za binadamu, wakuu wa Dunia yetu kwa sasa wapo chini yake ni kwa vile tu baadhi ya mambo fulani hayapo sawa ndio maana mamlaka yake inakuwa haina nguvu kamili kwa nchi zote, lakini inafanya kazi, ndio maana wakaja na mkakati wa mpango mpya wa Dunia, kwamba dunia ipangwe upya ili iendane na mambo yao, kwa maana kwa jinsi ilivyo kwa sasa kuna baadhi ya mambo hawawezi kabisa kuyafanya katika dunia, kwa sababu engineer wake wa mwanzo(Mungu), hakuipanga kiihivyo, kwa hiyo, wajenzi huru wana mpango mkakati wa kuipanga upya Dunia, kiuchumi, kiafya, kimazingira, kimaadili, kiulinzi, na mwisho kidini ili iendane na utawala wao ndio maana hata saa hizi bado kuna mambo yanayotoka kwao tunaweza yakataa lakini itafika muda pamekaza pote hakuna kukataa ni mbele kwa mbele, kwa wasio na yule Mwana ndio kwisha habari Yao, maana huwa hawazuiriki unless kuwe na opposite power kubwa kuliko yao. Jamani nimechoka kutype asubuhi njema tutaendelea mwakani.[emoji16]

#watupoasana[emoji847].
Maelezo yao na ya hao freemasons hayatofautiana mana unatapatapa tu..huna ulijualo sio upande wowote.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa mfano member gani wa Freemason alikosea masharti yao akanywewea kama supu??
No mercy, unanywewa kama supu ya asubuhi mapema sana, haijalishi ulikuwa nani duniani kwao sio shida watatafuta mtu mwingine wa kureplace.
 
Unamaanisha makanisa yanayofungisha ndoa za jinsia moja ndio Freemason??
FREEMASON
UNA AMBATANA NA:

NDOA ZA JINSIA MOJA
KUUA WATU-KUWAPUNGUZA KWA MAGONJWA YA KUTENGENEZA
 
Hujawahi kufanya kazi na freemason yeyote wewe, ni porojo tu na kutisha watu hapa.
Kaka unaesema ni watu poa unaelewa lakini unachokizungumza, maana... Au basi ngoja nisiseme sana lakini nina uhakika huwajui vizuri unawasikia tu na kusoma habari zao kwa watu wasio wajua pia, ila kwa mtu aliyefanya nao kazi ndio anajua upoa wao ukoje [emoji16], usicheze na moto ndugu these are Monsters bro.
 
Kuna mtoto au mtu mzima yeyote unayemfahamu aliyewahi kutolewa kafara na freemason?
Ila pia mengi ya mafundisho yao na practice zao za kiimani zinakiuka misingi ubinadamu, mfano kafara za watoto wachanga watu wazima na mengine mengi sana kama hayo
 
Acha porojo na kuongea kwa mafumbo kama mganga wa kienyeji, hujawahi kuwa freemason na ni mtupu kuwahusu.
Hapana ndugu yangu [emoji16], ndio maana mpaka sasa nipo hai, wangeshanimaliza zamani kama sio mkono wake aliyejuu kunitetea, I know these Monsters bro, ukisema huku hujajipanga ndio unakuwa supu yao, maana hakuna wakukutea, hata government haina uwezo wa kuwazuia kutimiza jambo lao wakiamua, halafu kuna mtu utashangaa anakuambia wanachafuliwa, unashindwa hata uanzeje kumsaidia maana ki ukweli hajui hata anazungumzia kina nani?
 
Unavyojipapatua kuonyesha kuna tofauti kubwa sana ya satan na satanist unaonyesha wewe ni kilaza na tapeli wa kutupwa[emoji1787][emoji1787]
CHANZO CHA NGUVU YA IMANI YA FREEMASONS.

kwanza inabidi utambue kuwa kuna aina kama tatu za nguvu za imani zinazooperate katika ulimwengu wa kiroho na hizi ndio zinazoongoza matukio yanayofanyika mwilini. na binadamu sisi katika njia moja au nyingine tunahusiana nazo kwa kujua au bila kujua.
na nguvu hizo za imani ni kama vile,
1. satanist( hii ni nguvu ya imani inayotokana na uchifu, mizimu ya ukoo na mababu na uganga wote wa kienyeji na kuagua na uchawi uko hapa na hicho kilichotokea kwa hao baba wadogo kiko hapa hizo tunaita roho zinazofatilia (mikuri na mahurunat) sio babu huyo yeye tayari yupo somewhere else ila hizi ni roho zinazofatilia mateso na vifungo vya ukoo uzuri na mimi ni kabila hilo na hicho kitu sio kigeni kwangu na mara nyingi huwa wanayauliza tufanye nini ili hali itulie yanatoa masharti na yakifuatwa hali huwa shwari ingawa inakuwa ni namna fulani ya utumwa kwa kabila au ukoo husika na hufanya hivi makusudi ili yaendelee kutambulika na kutambikiwa katika kila kizazi hata kama wahusika waliyoyakaribisha wameshakufa,ila mwanzoni sikuelewa mpaka nilipoanza kuchimba kutafuta ukweli wa mambo na nikawaletea sehemu kidogo sana ya nilicho nacho.na aina hii ya nguvu za imani imeenea sana africa na asia
2. satans (hawa ndio wengine huwaita devil worshippers ni wanadamu wenzetu kabisa lakini kwa sababu mbali mbali wao wamejitolea kikamilifu kuwa waabudu shetani kwa asilimia mia, wengi wapo katika secret societies (e.g freemason, Skull and bones society, Jesuit, n.k) hawa hawaruki na ungo hawawangi uchi usiku hawana matunguri wala hirizi, wao ni wachawi wa high level unakuta kapiga suti yake safi huku anasukuma v8 yake, kinachowapa nguvu sana kuliko satanists ni mkataba walioingia katika kumtumikia shetani kama mungu wao na hivyo kupokea uwezo wake moja kwa moja bila kutumia tunguli, na aina hii ya nguvu ya imani imeenea sana katika nchi za ulaya na marekani
3. kafiruna (mtanisamehe wakristo wenzangu maana sijapata tafsiri nzuri ya neno hili) lakini nitalielezea kwa jinsi ya maarifa niliyonayo ila hii ndio nguvu inayotokana na jina la Yesu na watu wote wenye imani hii. Hii kwa sasa imeenea almost ulimwengu mzima isipokuwa baadhi ya sehemu chache kwa sababu fulani fulani.

na katika viwango vya uwezo usatans unanguvu kuliko usatanist na kafiruna ipo ontop of all.(msininukuu vibaya sijaegamia upande wowote mi naeleza ninachokifahamu)

ikumbukwe kuwa satanist na satans zinahusiana kwa namna fulani kwa sababu ya originality kwa kuwa zote zinatoka kwa ancestor mmoja aliyejulikana kama lucifer.

ila ya kafiruna ipo tofauti na ni kinyume cha hizo zote mbili na kama nilivyosema ndio yenye nguvu kushinda zote kwa sababu ina originality ya muumbaji wa vyote mwenye uweza wote .
 
Huyo ni tapeli wale wanobandika mabango barabarani ya kujiunga na Freemason.
Mkuu niseme tu hufahamu unachoongelea. Labda habari hizi ulisikia kwa pastor wako kwenye kanisa la mabati. Satanists na satans ndiyo vitu gani?
 
Unamaanisha makanisa yanayofungisha ndoa za jinsia moja ndio Freemason??
BADILISHA MTAZAMO WAKO, KANISA SIO UTAKATIFU.
HIVYO KANISA KUFUNGISHA HIZO NDOA SIO AJABU.
 
Dah mwamba ulipotaja malango ya kuendea kuzimu na makaburini kunahusika ni kweli

Siku usik moja nililala usingizi kama kawaida,sasa mida ya usiku mnene nlianza kuota lakn sio kuota ni kama nlikuwa nashusika moja kwa moja lakin kwa ufahamu usiokuwa sawa,nlioona naanguka kutoka juu sana naelekea chini na maeneo yale kutoka juu nlikuwa nayajua a to z yaan hakukuwa na errors zozote.Eneo lenyew ni la shule ambayo nlisoma sekondar lakn lilipakana na makamburi.Basi vile nilikuwa nashuka (ilikuwa kama nimebebwa na mtu hivi Mgongoni lakn nlikuwa simuoni)spidi kali sana hadi upepo nilikuwa naufeel machoni na nyumba naziona na kuzitambua vzr kbs.Bwana nkajua tunaangua tunaenda kujibamiza laaahh vile tunakaribia makaburi yale tukalenga kaburi moja lakn badala yake likageuka duara jeusi tiii,na tukapenya katikat ya duara hilo.Muda wote huo tunadrop mi najiskia ok hata hofu sina na hata sijui ilikuwaje lkn sasa wakat tunaendelea kushuka( mle ndani tulikuwa tunshuka straight vilevile lakn ilikuwa ni kama tunapita kwenye pipe fulan).Nisiseme uongo tulufika mahali nkagundua mwendo ulipungua na mahali oale ni kama ilikuwa emptpy space ila giza lilikuwa la ajabu sana.Giza lili kuwa ni kama rangi nyeusi tii bile ilivo.Na hapo aisee nkahisi hali ambayo sjawahi kuhisi kwa kiwango kile.UPWEKE aisee ni upweke ambao hauelezeki yaan emptness,au void naifeel toka ndan ya moyo wangu..nilisikia sauti tofauti tofauti za watu wanalia,nlisika wanawake watoto na wanaume na wengine wanaita jina la Yesu.I was shocked nilitamka YESU WANGU NAOMBA NISAIDIE.Hapo ndio nkajihisi tumeanza kuascend kuja juu hata kabla hatujaibuka nkashtuka nmeloa jasho nahema ovyo ovyo.
The choosen one nisaidie ndg hapo ww unaonaje hili suala.Huwa natafakari sana sipati majibu ni nani alinichukua na kunitisha route ile
Pole sana,.
 
Hapana ndugu yangu [emoji16], ndio maana mpaka sasa nipo hai, wangeshanimaliza zamani kama sio mkono wake aliyejuu kunitetea, I know these Monsters bro, ukisema huku hujajipanga ndio unakuwa supu yao, maana hakuna wakukutea, hata government haina uwezo wa kuwazuia kutimiza jambo lao wakiamua, halafu kuna mtu utashangaa anakuambia wanachafuliwa, unashindwa hata uanzeje kumsaidia maana ki ukweli hajui hata anazungumzia kina nani?

kwa mda mrefu,david icke katika article zake na mijadala mbalimbali anaonekana kuwasagia kunguni waziwazi elites wa dunia hii ambao wapo nyuma ya agenda za freemason, illuminati na secret societies.

hata hivyo kiimani simuoni akiwa muumini wa hizi imani maarufu za abrahamic. nashangaa mpaka leo bado anadunda.

najiuliza anatoa wapi jeuri hii?, ana kwepa vipi mashambulizi ya kimwili na kiroho kutoka kwa hawa mashetani na wakuu wa hii dunia?. haogopi?.

je wamempuuza?, au hawajaamua kudeal nae?, au labda wameamua kumwacha tu awasadie kusambaza agenda zao bila yeye kujua?.

hapa juzi kati nimeona mwanamuziki kanye west na yeye kaanza kuwa expose. wamarekani weusi wana mashaka sana na hatma yake. wanahisi the elite wanam-distract makusudi ili jamaa afilisike, apate depression, aingie kwenye uraibu wa dawa za kulevya, achanganyikiwe na hatimaye ajimalize mwenyewe. na huko ndiko kanye anakoelekea.
 
Comment yenye madini mengi sana
Ukweli ni kwamba freemason hawapingi Mtu kuwa wa dini yoyote na ndio maana moja wapo ya sharti lao kuwa member lazima uwe muumini wa hizi mainstreaming religion na hii ni kwa sababu wanataka watu wanaoamini kuhusu divine being (God or gods) maana kama huamini kuhusu divine being hata wao utawasumbua maana kuna Mambo ya kiibaada za kishetani itabidi itabidi ufanye so kama huamini kuhusu Superior being in spiritual realm hata shetani hutamwamini pia na kinachotakiwa hapo ni imani kwa hiyo huwezi kuendana nao na ndio maana freemason yoyote unayemjua lazima utakuta ni muumini mmoja wapo wa hizi mainstreaming religion kuanzia yule mkuu wao kwa Tz (maana anajulikana wala sio siri) mpaka member wengine wa kawaida, kiufupi ni watu wanaojua nini wanafanya na wameamua kumuabudu Lucifer kama Mungu wao kwa hiari with full understanding wa kile wanachokifanya.

Sasa kuna mtu anashangaa inawezekanaje kusali kanisani au msikitini na bado kuwa Freemason, mpendwa inabidi utambue kuna Dini na Imani, Dini ni mfumo waliojiwekea wanadamu katika kumtafuta Mungu, lakini kumbuka hakuna aliyewahi kumwona Mungu, na ndio maana mfumo wa dini moja ni tofauti na nyingine, maana yake ni nini sasa, maoni na mawazo ya waasisi wa dini zetu (sio imani) katika kumtafuta Mungu ingawa huenda ni kwa nia njema, yalitofautiana kulingana na kila mmoja alivyokuwa na idea yake kumhusu Mungu na namna gani ya kumuabudu kwa kumpendeza.

Lakini imani ina asili ya uungu, au naweza kusema ndio mpango halisi wa Mungu kumtaka mwanadamu amuabudu katika namna gani ambayo inampendeza, ndio maana mtu hata asipokuwa muumini wa hizi mainstreaming religion kuna kitu kingine atakuwa anakiabudu na kukiamini maana ibada na imani ni asili tuliyoumbiwa lakini Dini tumejitengenezea wenyewe (sijasema ni mbaya) kwa makusudi mbalimbali maana kila Dini (sio imani kumbuka) inategemea mwanzilishi wake alikuwa na mtizamo na makusudi gani kuianzisha.

Kwa hiyo inawezekana kabisa akawa muumini mzuri tu wa Dini fulani, na kwa sababu ya nature ya jamii tunazoishi (maana mtu akiwa anaenda kwenye nyumba za ibada hata kwenye jamii ni mtu anaechukuliwa amestaarabika na ana utu fulani), Lakini IMANI yake sasa imejengwa katika kitu kingine tofauti na huko unakomuona kila siku za ibada yupo. Maana freemason ni kama uchawi kwa mantiki ya kujificha (mazingara ombwe) na ndio maana zinaitwa secret societies zikiwemo Skull and bones society n.k). Why they do called secret societies? Kuna siri gani hapo ingawa hili ni somo refu lakini siku nikipata muda nitakueleza sio tu imani yao na siri pia zilizojificha kwao.

Na katika uchawi wenye nguvu kubwa ni wa hawa members ni wachawi wa high quality, hakuna tunguli,sijui kujipaka majivu, masizi, sijui kuruka ungo, wao utawakuta na suti yake safi huku anasukuma v8 yake, kinachowapa nguvu sana kuliko wachawi wengine ni ule mkataba walioingia katika kumtumikia moja kwa moja Lucifer kama Mungu wao huku wakielewa kile wanachokifanya, kwa hiyo hupokea nguvu yao moja kwa moja kwa Lucifer mwenyewe na mashetani wakuu maana tayari waliwahi kuwa waaumini katika Dini zao na walifundishwa habari za Mungu tofauti na Lucifer ila kwa hiari wakamchagua.

Nina mengi ya kusema kuhusu hivi vyama lakini kiukweli kuna ushetani mwingi unafanyika huku,sema watu hawafahamu wao ukiwaambia freemason picha inayokuja ni watu wenye pesa na mafanikio ya kidunia(sipingi kuwa hawana) lakini behind hizo pesa na hayo mafanikio hakuna anayejua nini kinaendelea na hawawezi kujua maana hata member wenyewe wanaviapo zaidi ya vitatu vya kutokutoa siri, ndio maana leo hata umkamate member mmoja umwambie tunakuua au useme kila kitu, nakuhakikishia atakakimbilia kitanzi kuliko kusema, ingawa naonaga humu JF kuna watu wanajaribu kuelezea lakini ukisoma vizuri utagundua, they know nothing kuhusu hawa monsters au wanagusa vitu vile vya juu juu tu ambavyo hata wao huruhusu watu wengine wavijue maana haviathiri maslahi yao, lakini ukipagusa penyewe nakuhakikishia uwe umejipanga vizuri maana hata wao wamejipanga kuilinda siri yao kwa gharama zote na hii niliwahi kusema na ninarudia tena kuwa uchawi una kawaida ya kukosa nguvu kwako unapofunua siri yake maana uchawi ni kujificha (mazingara ombwe) ukiufichua huwa unakawaida ya kupoteza uwezo wake kwa mhusika.

Lakini niwatahadharishe usije kuona mtu tajiri anatikisa jiji au nchi kabisa halafu ni member nyuma ya hizo mali kuna Nafsi nyingi sana,zisizo na hatia zimedhurumiwa uhai, maana watu wanafikiri freemason ni moja, ila ndani kuna vitengo mbalimbali kikiwemo cha machinjo na kusababisha ajali na magonjwa ili kupata damu maana ufalme wa giza umeimarishwa kwa kafara za damu za wanadamu, kuna illuminate ingawa wengine wanafikiri hiki nacho ni chama cha siri lakini sio kweli ila hiki ninaweza kusema ni kitengo cha intelligence na mastermind katika freemason huku ndio utakuta ma genius wanaopanga mikakati ya kidunia, dunia iendeje?, nini kifanyike? ili kipi kitokee na kwanini isiwe vile?, huwa mnasema JF the home of great thinker lakini hamjui msemalo (utani tu [emoji16]) ila maana yangu ni kuwa kule ndio kuna watu ni wanadamu kama wewe ila mpaka leo hata mimi huwa najiuliza hivi ni wanadamu 100% au kuna namna.
Msione sijui matukio ya kigaidi sijui waasi wa wapi sijui pandemic gani ya kiulimwengu ndugu yangu havitokei by nature, kuna watu kabisa wanaopanga nani apigane na nani ili iwe hivi, nani amuue nani ili kitu fulani kitokee, ingawa kuna vingine vinaonekana vimekaa kiimani zaidi (mf.ugaidi) , lakini hiyo ni danganya toto behind the scene kuna mastermind na ma great thinker wameplan ili kije kitokee kitu fulani kwa lengo fulani ili kutimiza matakwa yao ya kuutawala ulimwengu.

Sasa mwingine atajiuliza kama wanauwezo wa kufanya hayo yote wanashindwaje kuutawala ulimwengu, labda hufahamu hiki kitu nikujuze, kiukweli ulimwengu uliumbwa na Mungu pamoja na vitu vyake akiwemo mwanadamu, kwa hiyo ulitengenezwa katika namna ya ku favour utawala wa kiMungu au mamlaka za nuruni ndio maana watu kwenda ibadani kusali akiwa na Bible yake sio shida, kufanya mikutano ya hadhara ya injili nijambo lakawaida ila je uliwahi ona wachawi au freemason wanafanya ibada zao au mambo yao hadharani, hata tu elimu ya giza haipatikani kirahisi kama unavyoweza enda Sunday school ukafundishwa habari za Mungu, hii ni kwa sababu nature ya ulimwengu tuliopo haijaweza kubeba ushetani wa kutosha ili igeuke iwe ya giza ili wao waitawale wanavyotaka maana wao ndio wenye mamlaka ya gizani ndio maana kuna mambo yao kutoka sheol mengine hupingwa na wanakuwa hawana uwezo wa kuforce(mf,ushoga),

Ila mkakati upo wa kuitawala na mpaka saa hizi unatekelezwa ila kuna watu wanazuia kwa namna fulani (ingawa sipo kidini) maana siko hapa kutetea dini yoyote au imani fulani ila naelezea ninachokijua

Kuna watu wa imani fulani huwa wanaomba sana [emoji2960] na kufunga tena wakati mwingine kwa kukemea na kuvunja kabisa kwa jina fulani. Hawa ndio kikwazo kikubwa kwa sababu katika kunena kwao kuna mipango mingi huwa inaharibiwa na hata kama imeanza kutekelezwa huwa inafell na ndio sababu wakaundiwa kitengo maalum katika freemason (sitakitaja kwa jina kwa sababu fulani) ambacho hu deal na watu wa imani hii na katika nyumba zao za ibada kuwaharibu na kuzisambaratisha ili wasielewane na ile nguvu ya maombi yao ipotee ili watimize mambo yao ,usione leo pastor kazini na muumini wake ukafikiri ni tamaa tu ya kawaida ya kibinadamu au anatoa mpaka rushwa ili awe askofu au ana wake wawili, ndugu mambo hayatokei hivi hivi, hapo mtu kaishatumiwa swaibu zinaa [emoji16] mapema sana linamuendesha tu, usione kwaya zinavunjika kwa sababu ya zinaa (something is working behind physical reality).

Sasa utajiuliza mtu wa Mungu inawezekanaje akatumiwa jini likampata, kuna siri kubwa sana hapa unakuta mpaka kufikia kumshinda hivyo wamemuwinda karibu miaka 3 mpaka 5 maana sio kazi rahisi kama unavyofikiri na jini kwa mfano wa zinaa anayetumwa kwa mtumishi fulani wa Mungu aliyesimama ni tofauti na yule anayetumwa kwa kabinti fulani hapo mtaani kwenu maana ingawa kazi ni moja lakini yanatofautiana sana kwa nguvu na uwezo wa kiutendaji(somo lingine), na kibaya anayewindwa hajui kama anawindwa, kwa hiyo kupitia mistake zake ndogo ndogo akiteleza tu wanaye[emoji17], na hakuna kitu kigumu kama kushindana na adui usiemwona na hujui kama akuwinda ndio maana tunatakiwa kuomba toba kila wakati ili Mungu asiondoe ulinzi wake kwa sababu ya dhambi zetu, maana laiti ungeona watumishi wa Mungu waaminifu wanavyowindwa nakuhakikishia usingetamani hata kuifanya hiyo kazi maana wewe ndio unakuwa main target yao, Ndugu usikimbilie kuanza huduma au kanisa kabla hujapokea nguvu ya kutosha labda kama unawafanyia wao (wanangu wa keki ya upako mikono juu[emoji16]), ila Mungu ni mwaminifu anawatetea sana na ndio maana hata katika harakati za kumuangusha au kumuua lazima mnakuwa makini maana kufa ni kugusa Maana Mungu hana utani kwa watu wake potential, Maana kitendo hata cha kumtaja tu jina kilingeni (madhabahu ya kichawi) mnaweza kufa kama mende kwa huo moto utakaowalipukia kwa hiyo ni vita hasa na ni hatari pia kwa upande wa muwindaji.

Na ndio maana saa hizi wanamkakati mpya unaitwa mpango mpya wa Dunia New world order huu ni mkakati wa kuipanga Dunia upya tofauti ilivyopangwa na aliyeiumba ili iweze kubeba ushetani wa kutosha, kuwezesha itawalike na hawa monsters ila shida ndio hao wanenaji ni waharibifu sana [emoji16] wa hizi mambo halafu wao hawajui kama wanaharibu na ndio maana wanawachukia sana kule [emoji23], yaani akisema nasambaratisha, kama yupo muhusika humu nafikiri atakuwa shahidi mzuri wa nini ambacho kinaendelea behind the scene ni kusaambaa haswa hakibaki kitu, maneno ya kinywa ni silaha hatari sana yakitumika kwa maarifa na imani kamilifu sema wengi wao hawajui na ni kwa sababu hawaoni kinachoendelea ule upande mwingine.

Inshort freemason ni pana na wengi wanaojaribu kuilezea wanajua vichache sana kuhusu hawa Monsters, lakini kwa jinsi ninavyowaelewa huwezi toa siri yao hata moja kama navyoona nyuzi za humu JF wakuache uendelee kula ugali[emoji16] hata kama una Mungu lazima watakusumbua mpaka ujute sema ambacho hawataweza ni kukuterminate kwa sababu ya nguvu inayokulinda, tofauti na hapo wewe ni supu yao ya asubuhi.

Lakini utashangaa kuna mtu eti anatoa uzi wa siri za freemason humu na anaandika muendelezo wa uzi wake kabisa, mi huwa nasoma nacheka tu maana hakuna siri yoyote wanatoa zaidi ya porojo nyingi, maana navyowajua wale wadau unatoa siri yao hujajipanga wanakupoteza.

Source: Elimu changa [emoji3]

#Zakuambiwachanganyanazako
T
 
Unaweza kuthibitisha Kanumba na Sharo walikuwa Freemason?
Ukithibitisha mbele ya mahakama jf kuwa bibi yako ndio huwa anakuwangia usiku mpaka ukaugua ugonjwa wa akili, chap na mimi naleta uthibitisho,hapa
 
Huyo David Icke alipaswa awafunguwe akili vilaza wote wanaosema Freemason wanakunywa damu za watu, wajiulize kwa nini hawajawanya damu yake mpaka sasa.
kwa mda mrefu,david icke katika article zake na mijadala mbalimbali anaonekana kuwasagia kunguni waziwazi elites wa dunia hii ambao wapo nyuma ya agenda za freemason, illuminati na secret societies.

hata hivyo kiimani simuoni akiwa muumini wa hizi imani maarufu za abrahamic. nashangaa mpaka leo bado anadunda.

najiuliza anatoa wapi jeuri hii?, ana kwepa vipi mashambulizi ya kimwili na kiroho kutoka kwa hawa mashetani na wakuu wa hii dunia?. haogopi?.

je wamempuuza?, au hawajaamua kudeal nae?, au labda wameamua kumwacha tu awasadie kusambaza agenda zao bila yeye kujua?.

hapa juzi kati nimeona mwanamuziki kanye west na yeye kaanza kuwa expose. wamarekani weusi wana mashaka sana na hatma yake. wanahisi the elite wanam-distract makusudi ili jamaa afilisike, apate depression, aingie kwenye uraibu wa dawa za kulevya, achanganyikiwe na hatimaye ajimalize mwenyewe. na huko ndiko kanye anakoelekea.
 
Back
Top Bottom