CHANZO CHA NGUVU YA IMANI YA FREEMASONS.
kwanza inabidi utambue kuwa kuna aina kama tatu za nguvu za imani zinazooperate katika ulimwengu wa kiroho na hizi ndio zinazoongoza matukio yanayofanyika mwilini. na binadamu sisi katika njia moja au nyingine tunahusiana nazo kwa kujua au bila kujua.
na nguvu hizo za imani ni kama vile,
1. satanist( hii ni nguvu ya imani inayotokana na uchifu, mizimu ya ukoo na mababu na uganga wote wa kienyeji na kuagua na uchawi uko hapa na hicho kilichotokea kwa hao baba wadogo kiko hapa hizo tunaita roho zinazofatilia (mikuri na mahurunat) sio babu huyo yeye tayari yupo somewhere else ila hizi ni roho zinazofatilia mateso na vifungo vya ukoo uzuri na mimi ni kabila hilo na hicho kitu sio kigeni kwangu na mara nyingi huwa wanayauliza tufanye nini ili hali itulie yanatoa masharti na yakifuatwa hali huwa shwari ingawa inakuwa ni namna fulani ya utumwa kwa kabila au ukoo husika na hufanya hivi makusudi ili yaendelee kutambulika na kutambikiwa katika kila kizazi hata kama wahusika waliyoyakaribisha wameshakufa,ila mwanzoni sikuelewa mpaka nilipoanza kuchimba kutafuta ukweli wa mambo na nikawaletea sehemu kidogo sana ya nilicho nacho.na aina hii ya nguvu za imani imeenea sana africa na asia
2. satans (hawa ndio wengine huwaita devil worshippers ni wanadamu wenzetu kabisa lakini kwa sababu mbali mbali wao wamejitolea kikamilifu kuwa waabudu shetani kwa asilimia mia, wengi wapo katika secret societies (e.g freemason, Skull and bones society, Jesuit, n.k) hawa hawaruki na ungo hawawangi uchi usiku hawana matunguri wala hirizi, wao ni wachawi wa high level unakuta kapiga suti yake safi huku anasukuma v8 yake, kinachowapa nguvu sana kuliko satanists ni mkataba walioingia katika kumtumikia shetani kama mungu wao na hivyo kupokea uwezo wake moja kwa moja bila kutumia tunguli, na aina hii ya nguvu ya imani imeenea sana katika nchi za ulaya na marekani
3. kafiruna (mtanisamehe wakristo wenzangu maana sijapata tafsiri nzuri ya neno hili) lakini nitalielezea kwa jinsi ya maarifa niliyonayo ila hii ndio nguvu inayotokana na jina la Yesu na watu wote wenye imani hii. Hii kwa sasa imeenea almost ulimwengu mzima isipokuwa baadhi ya sehemu chache kwa sababu fulani fulani.
na katika viwango vya uwezo usatans unanguvu kuliko usatanist na kafiruna ipo ontop of all.(msininukuu vibaya sijaegamia upande wowote mi naeleza ninachokifahamu)
ikumbukwe kuwa satanist na satans zinahusiana kwa namna fulani kwa sababu ya originality kwa kuwa zote zinatoka kwa ancestor mmoja aliyejulikana kama lucifer.
ila ya kafiruna ipo tofauti na ni kinyume cha hizo zote mbili na kama nilivyosema ndio yenye nguvu kushinda zote kwa sababu ina originality ya muumbaji wa vyote mwenye uweza wote .