Kumbe Degree haisaidii ku win Life???

ndugu yangu, samahani, mimi kila nikisoma ujumbe wako sielewi, naomba urudie tena....!!!!!!!!!!!!samahani kwa usumbufu lakini!
 
Jamani jamani
nashangaa sana hawa wenzetu waliofanikiwa kufika vyuo vikuu wanavyo ishi maisha mabovu,mimi sikufanikiwa kufika chuo kikuu niliishia huku chini,nilifikiri waliofanikiwa kufika huko juu mambo yao yatakuwa shwaaari!kumbe hakuna kitu mambo ni ovyo tu yaani mara nyingine najiuliza kulikuwa na haja gani ya wao kulazimisha kwenda chuo kikuu??jamaa wanatembea town na mavyeti yao mpaka yanapauka eti wanatafuta kazi,jamani!mimi nilikuwa najilaumu kwa nini sikwenda chuo kikuu nionekane msomi kama wao kumbe nilifanya uamuzi wa busara bwana,jamaa zangu karibu wote waliokwenda mlimani mwanzoni wa miaka ya 2000 wapo wanasota mitaani na vibarua vya temporary,kibarua kikiisha anakuja kijiweni eti tumpige tough kwa sababu anatafuta kazi nyingine mara ana project anataka kuanzisha,kumbe wao wanafikiri tofauti na sisi,badala ya kwenda pale songea au tunduma na kuanzisha kibiashara kwa kutumia elimu yao waliyopata wanakaa vijiweni na kumba vihela kwa jamaa zao,kumbe hakuna haja ya kwenda chuo kikuu

Elimu ni muhimu ..japo maisha nayo hayana formula ni kama mpira.. hata man u nayo au simba huwa wana mwaka wa kufungwa
 
duh mkuu umekanyaga kwa hasira kweli. btw mbona umepotea sana?
Teh teh te te! Mdau i thought I should tell him simply but strongly........ nipo mdau nimeona nikimbizane tu na vyekundu vilivyo karibu na wanaomaliza rasilimali. Ntashangaa shangaa mara ukute wamemaliza wee umekodoa mijicho tu!
 
Wewe unatakiwa kujiita mwenye bahati kwa kua na maisha mazuri bila ya elimu, nakutahadharisha nenda shule mana mambo yanavyokwenda bila ya elimu utaporomoka muda si mrefu na dharau zako.
 
Elimu utakuwa nayo lakini huwezi kuwa sawa na wa level ya Degree, ni vizuri kujiendeleza ukipata fursa

nyodo ya visenti vidogovidogo huwapa vijana ulimbukeni wa kutotambua dunia ikoje, na pia silika wa sisi waswahili sababu tumetokea kwenye kucheza na nyoka,kwahiyo mtu akipata vijisenti anaona imetosha na hivyo kuwa limbukeni wa kuanza kuropoka kama huyo dogo mleta thread hii;ikumbukwe nchi nyingi zilizoendelea zimepiga hatua kubwa kielimu, na zili weka msisitizo mzuri wa sera na rasilimali , zina nguvu kazi kubwa yenye wasomi ambao ni mchango mkubwa katika nguvu kazi katika kujenga uchumi.Leo hii soko la ajira lingekuwa na wasomi wengi wa chuo kikuu kama sekta binafsi , uchumi ungepiga hatua kubwa.haijalishi ni namna gani sera za serikali ni madhubuti kutoa ajira sitahiki na kwa nguvu kazi kubwa, bali elimu ni rasilimali muhimu ili nguvu kazi iweze kufanya kazi vyema.Kimsingi hata ustaarabu(socialization), ni rahisi kuijenga kwa wasomi, mikakati mbalimbali ya soko la ajira ,ni rahisi kuijenga wa wasomi.aache kuchanganya na sera mbovu za serikali ya sasa kuhusu soko la ajira ambapo limejaa ubabaishaji na kuacha nguvu kazi kwenye mataa bila ajira.Pia wakati mwingi mitaala ni suala lingine lilitakiwa kuangaliwa kiusahihi ili kuwezesha vijana wengi wajiajiri;lakini kulaumu usomi kama si hoja ya mafanikio ni kukwepa kivuli chako.usomi wa chuo kikuu ulikotukuka ni muhimu kwa vijana binafsi kama nguvu kazi, na pia ni muhumu kama taifa ili kujenga uchumu endelevu , makini na madhubuti
 
hatusomi kupata pesa tunasoma kuelimika na kuongeza ufahamu juu ya mambo mbalimbali. sasa kwako kama kipaumbele ni pesa basi tafuta pesa, lakini kama unataka kuelimika nakushauri uende shule kuelimika zaidi.

na si kila mwenye kupita chuo kikuuu kaelimika wengine wamepita vyuo na kupata masters degree lakini ukimtazama hata kifikra bado yuleyule huyu elimu haijamsaidia. tena anahitaji kuelimishwa.
 
Jamani jamani
nashangaa sana hawa wenzetu waliofanikiwa kufika vyuo vikuu wanavyo ishi maisha mabovu,mimi sikufanikiwa kufika chuo kikuu niliishia huku chini,nilifikiri waliofanikiwa kufika huko juu mambo yao yatakuwa shwaaari!kumbe hakuna kitu mambo ni ovyo tu yaani mara nyingine najiuliza kulikuwa na haja gani ya wao kulazimisha kwenda chuo kikuu??jamaa wanatembea town na mavyeti yao mpaka yanapauka eti wanatafuta kazi,jamani!mimi nilikuwa najilaumu kwa nini sikwenda chuo kikuu nionekane msomi kama wao kumbe nilifanya uamuzi wa busara bwana,jamaa zangu karibu wote waliokwenda mlimani mwanzoni wa miaka ya 2000 wapo wanasota mitaani na vibarua vya temporary,kibarua kikiisha anakuja kijiweni eti tumpige tough kwa sababu anatafuta kazi nyingine mara ana project anataka kuanzisha,kumbe wao wanafikiri tofauti na sisi,badala ya kwenda pale songea au tunduma na kuanzisha kibiashara kwa kutumia elimu yao waliyopata wanakaa vijiweni na kumba vihela kwa jamaa zao,kumbe hakuna haja ya kwenda chuo kikuu

soma wewe ujue ata umuhimu wa paragraph ukiandika.
 
Shule moja ilikuwa na wanafunzi 30,wakafanya mtihani wakwanza akapata 27 na wamwisho 10.Wakwanza akawa anajisifu akajisahau kwamba wote walikuwa kwenye daraja moja(F).Sasa je! ni kweli umefanikiwa kiasi cha kusema huoni umuhimu wa kwenda chuo kikuu?
 
Jamani jamani
nashangaa sana hawa wenzetu waliofanikiwa kufika vyuo vikuu wanavyo ishi maisha mabovu,mimi sikufanikiwa kufika chuo kikuu niliishia huku chini,nilifikiri waliofanikiwa kufika huko juu mambo yao yatakuwa shwaaari!kumbe hakuna kitu mambo ni ovyo tu yaani mara nyingine najiuliza kulikuwa na haja gani ya wao kulazimisha kwenda chuo kikuu??jamaa wanatembea town na mavyeti yao mpaka yanapauka eti wanatafuta kazi,jamani!mimi nilikuwa najilaumu kwa nini sikwenda chuo kikuu nionekane msomi kama wao kumbe nilifanya uamuzi wa busara bwana,jamaa zangu karibu wote waliokwenda mlimani mwanzoni wa miaka ya 2000 wapo wanasota mitaani na vibarua vya temporary,kibarua kikiisha anakuja kijiweni eti tumpige tough kwa sababu anatafuta kazi nyingine mara ana project anataka kuanzisha,kumbe wao wanafikiri tofauti na sisi,badala ya kwenda pale songea au tunduma na kuanzisha kibiashara kwa kutumia elimu yao waliyopata wanakaa vijiweni na kumba vihela kwa jamaa zao,kumbe hakuna haja ya kwenda chuo kikuu
hapo kwenye red??? wao hawakulazimisha kwenda bali wewe ulilazimisha kwenda lakini ukashindwa. kwenda chuo kikuu hawalazimishi....sio elimu ya msingi au awali ile mkuu.ivi tangu 2000 mpaka leo unakumbukia? inaelekea uliumia sana
ulipoona wenzako wanaenda chuo then wewe unaanza kuuza mayai
 
Dah!.. Jamaa ananikumbusha Le' Proffesuer Ze comedy...............:A S-rap:
 
Back
Top Bottom