Kumbe anafanya kazi ya kuuza baa.

Kumbe anafanya kazi ya kuuza baa.

Syosaamenye

Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
79
Reaction score
7
Nilikua na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke M1 kutoka kijijini ambako tulikua tukiishi huyo mpnz wangu alikua akiniaga mara kwa mara kua anenda Jijini Dar kumsalimia dada yake na pia alikua akirudi kijiji na kukaa muda wa miezi miwili au mitatu!! kisha anarejea tena DSM nikimuuliza kua anfanya kazi gani alikua ananiambia anamsaidia dada yake kuuza mgahawa. kitu cha ajabu nikihoji sana kuhusu kazi yake alikua anakasirika sana.

kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya kuja kusoma masomo ya juu yaani shahada ya Uzamiri sikutaka kumtafuta kwani nilikua busy sana na masomo lakini kitu cha ajabu alinipigia simu na kunieleza kua amepata taarifa kua nipo DSM aliniomba tuonane tulipo onana akaniambia kua ananiomba pesa kwa ajili ya kulipia pango la nyumba nilishangaa sana kusikia hivyo nilimuuliza kwani nyumbani kwa dada yake amehama akaniambia kua shemeji yake anamtongoza ndio maana ameamua kuondoka na kujitegemea yeye. nilimshauri arudi kijijini kwani kuna nafasi kubwa ya malazi pia na fulsa nyingi za kujiajiri alikataa na kuniambia kua na mimi nimekimbia nini kule kijijini nilimweleza kua mimi nipo hapa kwa muda tu then nitarudi kijijini nikimaliza masomo yangu. nilipomweleza hivyo akaniambia tusitafutane tena na kuniambia mimi ni mshamba nikamjibu kua mi sina tatizo. ukapita muda kama wa mwezi m1 akanitumia ujumbe kua ananipenda na wala hajisikii vzuri kuachana mimi na ananiomba nionane.

Nilikubali kwasababu nilikua nampenda pia tulipoonana akanielezea jinsi maisha yanavyomsumbua hapa jiji DSM nilimuuliza anafanya kazi gani hakutaka kuniambia nilipombana kwa kushawishi aliniambia yeye ni Bar attender nilihuzunika sana kufanya kazi hiyo wakati anafursa nyingi za kujiajiri ambazo ni salama hasa kwa afya yake na lkn yeye hakuonesha wasiwasi wowote. na aliniambia hana mpango wa kurudi kijijini nilipofanya uchunguzi kumbe aliolewa na kua mke wa pili yaani nyumba ndogo. akamtibua huyo jamaa aliemuweka ndani yule jamaa akamkimbia.

sasa ananiomba turudiane wakati nikimwambia tukaishi kijijini yeye hataki anataka tuishi jijini na pia anataka kuendelea na hiyo kazi yake ambayo mimi siitaki.

kitu kingine nikimwambia tukapime yeye hataki hata kusikia suala la kwenda kupima hata wiki inaweza kuisha bila kuwasiliana nae nikimpigia hapokei.

naomba ushauri wana JF.

Tafadhari msitukane!!!!!!!!!!!!!
 
pole inawezekana ashakwambuzi HIV.

mkuu mbona jibu unalo moja tu. piga chini kabiza hata sim no yake block kabisa na wewe delete kabisa no yake.

kuwa makini mkuu chezea dar weee!!!.

kama unampenda na uko tayari kuendelea nae, hata master usisome maana unapoteza resources bule za watanzania au wasaidie ndugu zako.
 
Unampenda mtu au unapenda kazi? Kama umempenda mtafutie shughuli nyingine na uendelee naye. Naamini anafanya kazi hiyo kwa sababu ya shida tu.
 
kapime HIV. kama uko safe toka mbio mkuu, siku nyine kuwa makini ving'ayvo vyote si gold!!
 
Unampenda mtu au unapenda kazi? Kama umempenda mtafutie shughuli nyingine na uendelee naye. Naamini anafanya kazi hiyo kwa sababu ya shida tu.

acha kumpoteza mwenzio. kama kazi nzuri kwanini afiche-fiche??.

pili yeye kashakuwa nyumba "ndogo" na "bar attender"

hapo amna kitu.
 
Jibu lipo mlangoni:

1. Umemshauri jambo la msingi, pima afya hataki
2. Aachana na hiyo kazi kuna fursa nyingine hataki

Sasa unataka upewe ushauri wa kumlazimisha...........Huyo ana maisha yake muache aendelee nayo.
 
yaani mtu kashaliwa mbele yako unataka tukushauri nini?
kamuombe msamaha kwa mume wake basi.............wanaume wengine kama siyo wanaume ,mnaiaibisha tasnia ya wanaume.
 
bomu hilo.ila kazi ni kazi wapo wauza bar wanajiheshimu sana tu.kuna muuza bar mmoja mango garden ni mdada anajiheshimu na yupo pale miaka mingi tu
 
Ushauri wako niu mzuri ingawa unamaana tu kama bado hajaambikizwa. Kama kweli anasoma Masters, huyu ndugu hakuwa na sababu za kutafuta ushauri kwa ishu dogo kama hii ila anaonekena ni mgumu sana wa kufikiri. Inawezekana anasomea cheti cha secretarial huyu. Sijawahi kuona graduate mwenye uwezo mgodo wa kufikiri kama huyu. Eti anauliza afanye nini kuhusu Bar Maid wake ambaye hayuko tayari kwenya kupima? Kwa aina hii ya wasomi Tanzania kazi ipo. Anatudhalikisha huyu

pole inawezekana ashakwambuzi HIV.

mkuu mbona jibu unalo moja tu. piga chini kabiza hata sim no yake block kabisa na wewe delete kabisa no yake.

kuwa makini mkuu chezea dar weee!!!.

kama unampenda na uko tayari kuendelea nae, hata master usisome maana unapoteza resources bule za watanzania au wasaidie ndugu zako.
 
Ina maana hata hili huwezi amua?..hizi masters zingine..lolz
Kikubwa hapo ni kupima afya kwanza, kama hataki kimbia haraka sana
Sehemu zingine u-barmaid ni kazi kama zingine, ila kibongobongo sikushauri!
 
Nilikua na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke M1 kutoka kijijini ambako tulikua tukiishi huyo mpnz wangu alikua akiniaga mara kwa mara kua anenda Jijini Dar kumsalimia dada yake na pia alikua akirudi kijiji na kukaa muda wa miezi miwili au mitatu!! kisha anarejea tena DSM nikimuuliza kua anfanya kazi gani alikua ananiambia anamsaidia dada yake kuuza mgahawa. kitu cha ajabu nikihoji sana kuhusu kazi yake alikua anakasirika sana.

kwa bahati nzuri nilipata nafasi ya kuja kusoma masomo ya juu yaani shahada ya Uzamiri sikutaka kumtafuta kwani nilikua busy sana na masomo lakini kitu cha ajabu alinipigia simu na kunieleza kua amepata taarifa kua nipo DSM aliniomba tuonane tulipo onana akaniambia kua ananiomba pesa kwa ajili ya kulipia pango la nyumba nilishangaa sana kusikia hivyo nilimuuliza kwani nyumbani kwa dada yake amehama akaniambia kua shemeji yake anamtongoza ndio maana ameamua kuondoka na kujitegemea yeye. nilimshauri arudi kijijini kwani kuna nafasi kubwa ya malazi pia na fulsa nyingi za kujiajiri alikataa na kuniambia kua na mimi nimekimbia nini kule kijijini nilimweleza kua mimi nipo hapa kwa muda tu then nitarudi kijijini nikimaliza masomo yangu. nilipomweleza hivyo akaniambia tusitafutane tena na kuniambia mimi ni mshamba nikamjibu kua mi sina tatizo. ukapita muda kama wa mwezi m1 akanitumia ujumbe kua ananipenda na wala hajisikii vzuri kuachana mimi na ananiomba nionane.

Nilikubali kwasababu nilikua nampenda pia tulipoonana akanielezea jinsi maisha yanavyomsumbua hapa jiji DSM nilimuuliza anafanya kazi gani hakutaka kuniambia nilipombana kwa kushawishi aliniambia yeye ni Bar attender nilihuzunika sana kufanya kazi hiyo wakati anafursa nyingi za kujiajiri ambazo ni salama hasa kwa afya yake na lkn yeye hakuonesha wasiwasi wowote. na aliniambia hana mpango wa kurudi kijijini nilipofanya uchunguzi kumbe aliolewa na kua mke wa pili yaani nyumba ndogo. akamtibua huyo jamaa aliemuweka ndani yule jamaa akamkimbia.

sasa ananiomba turudiane wakati nikimwambia tukaishi kijijini yeye hataki anataka tuishi jijini na pia anataka kuendelea na hiyo kazi yake ambayo mimi siitaki.

kitu kingine nikimwambia tukapime yeye hataki hata kusikia suala la kwenda kupima hata wiki inaweza kuisha bila kuwasiliana nae nikimpigia hapokei.

naomba ushauri wana JF.

Tafadhari msitukane!!!!!!!!!!!!!

Sasa wewe ndugu yangu hili suala nalo linahitaji ushauri? Naamini majibu yote unayo wewe mwenyewe! Katika hili hauhutaji kuitumia hata hiyo Masters yako, otherwise umesoma lakini haujaelimika bro...!
 
Hao ndio wasomi wa master wetu
Kama nape vile
 
Back
Top Bottom